Watu wengi wanatumia muda mwingi sana katika mitandao ya kijamii. Kati ya masaa nane ya kazi basi unakuta anatumia masaa matatu mpaka manne kwenye facebook.
Kati ya masaaa kumi ya kuwa darasani ya mwanafunzi wa chuo basi matano anayatumia katika mtandao.
Baada ya hapo mtu anatumia muda uliobaki katika kuangalia tv na kuangalia filamu.
Wanavutiwa sana na habari za hivi karibuni. Habari za vita vinavyotokea nchini Syria, habari za majambazi waliosababisha maafa, au ndege iliyopotea.
Ni bahati kuwa katika ulimwengu ambao kila mtu anaweza kuweka chochote anachojisikia mtandaoni. Lakini bahati hii inageuka kuwa bahati mbaya pale ambapo marafiki wako wengi sana wanakuwa wanakuwa wanaandika (wanaposti) vitu vya kawaida sana ambavyo haviwezi kukutoa sehemu moja kwenda sehemu nyingine.
Vitu ambavyo haviwezi kukufanya kusonga mbele.
Cha kufanya ni kupunguza muda wako unaokuwa mtandaoni. Punguza muda wako wa kuwa facebook, punguza sana muda wako wa kuwa you tube. Punguza muda wa kufuatilia habari hasi kama sio KUACHA KABISA.
Soma zaidi hapa; Wiki Moja Bila Habari
Watu wengi wamechagua kuishi maisha ambayo ni ya kawaida sana, kwa sababu kawaida ni kitu ambacho KINAVUMILIWA NA JAMII.
Ile jamii ya watu waliokuzunguka wakiona wewe unafanya kazi kubwa sana, wakiona wewe ni mjasiliamali, mtu anayechukua fursa. Watakuona kama mchoyo, mtu mwenye matatizo asiyetosheka, mtu asiye makini.
Wengine watadhubutu kukuambia kwamba
Punguza kidogo
Furahia maisha
Usifanye kazi kubwa sana
Chukukia maisha kawaida sana
Ridhika
Kula ujana
Pesa sio kila kitu.
Kama unataka ukubwa utafute mwenyewe.
Kuwa na ndoto kubwa sana ya kukufikisha unapotaka. Usiwasikilize watu wa aina hiyo. Usiwasikilize watu ambao hawatendi ila wana maneno zaidi ya matendo.
Soma zaidi hapa; Mlango Mmoja Ukifungwa, Saba Hufunguliwa
Vunja pingu hizi kwa kwenda kinyume na matarajio ya watu, wanaotaka uendelee kuishi maisha ya kawaida. Vunja pingu za kufuatilia habari hasi.
Vunja pingu za za kutaka mambo madogo maana weee tayari ni mtu mkubwa kwa hiyo lazima ufanye mambo makubwa.
Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
BONYEZA HAPA KUPATA KITABU CHA BIASHARA NDANI YA AJIRA
Kujiunga kundi la wasapu la SONGA MBELE BONYEZA HAPA