Vutia Kwako Tabia Hizi.


Habari za leo rafiki na ndugu yangu
Karibu sana katika makala ya leo.

Ili kufikia mafanikio na kufikia sehemu ambayo inaonekana iko juu sana katika ulimwengu wa mafaniko unahitaji kuwekeza sana kwa kuweka nguvu, muda, lakini pia kutafuta watu sahihi wa kwenda nao kwenda kwenye mafanikio na kuhakikisha wamekufikisha kule ambapo wewe unataka kufika.

Huwezi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine bila kuwa na mtazamo chanya na watu chanya ambao watakufikisha kule ambapo unataka kufika.

Mtu ambaye anafurahia na kuwa na mtazamo chanya na watu ambao anakutana nao kila siku, anaweza kupata kitu chochote anachotaka kutoka kwa watu hao ambao anashirikiana nao.
Napolleon HilHill

Kama unataka kwenda mbali nenda peke yako, kama unataka kufika mbali nenda na watu


Kama unataka kwenda mbali sana lazima uende na watu ambao watakufukisha kule ambapo unataka kufika na kama unataka kufika haraka unaweza kwenda peke yako.

Mtu ambaye anataka kwenda mwezini hawezi kupanga safari ya kwenda mwezini peke yake bali atwatafuta watu sahihi wa kushirikiana nao ili waweze kumsaidia kufika  mwezini. Hata kwa mawazo

Jinsi ya kuuvutia urafiki wa kweli kwako.

Urafiki  wa kweli ni kitu ambacho kinavutiwa maana huwezi kupata bila kutoa, kitu kizuri chochote lazima kitolewe gharama yake kabla ya kuanza kufanya kazi.

Unahitaji  kuonesha ukarimu.  Siku zote utazungukwa na watu wa aina yako kama wewe, ukiwa mkarimu utavutia watu ambao ni wakarimu kwako, kama wewe na kama wewe ni mwongo utavutia waongo kama wewe kwako.
Ni ukweli kwamba mtu ambaye huwa ana furaha na anawachamgamkia sana watu huwa anapendwa sana na  watu wengi kuliko yule ambaye ni kinyume chake.

Vivyo hivyo mtu ambaye  huwa anavutia watu wa  aina hiyo hiyo kwake.
Hili ni sheria mbayo ni ya asili kwamba vitu vya aina moja vinajivutia kwa pamoja. (“Like attracts like”)
Ndio maana unaweza kushangaa wewe kama hushabikii mpira lakini watu wanaoshabokia mpira wanajuana vizuri sana. Utajiuliza kitu gani kiliwaungamisha hawa watu. Hii ndiyo sheria ya asili kwamba lazima vitu vinavyofanana vitakuja pamojamtu atavutia watu ambao anaendana nao.

Unaweza pia kushangaa unaenda eneo fulani unakuta kwamba watu wanaopenda kuangalia filamu wanajuana na wakikutana lugha yao inafahamika ni lugha ya filamu, wanajua nani kaigiza kwenye filamu gani na ameigiza kama nani? Hii ndiyo sheria ya asili ya kuvutia kwako kila ambacho kinaendana na wewe.

Soma zaidi hapa nguzo unayohitaji ili kufikia mafanikio

Angalia hata mti ambao nao huvutia kwake tabia zile ambazo zinaendana na kile ambacho utakuja kuwa baadae. Ndio maana ukipanda mbuyu hauoti mnazi au mpapai. Hii ni kwa sababu mbuyu utazalisha seli ambazo ni za mbuyu kama ilivyokuwa mbegu ya mbuyu. Na matunda tunayotegemea kupata  baada ya mpapai kukua si tofauti na mapapai ambayo ni yametokana na mpapai kuvutia seli za aina yake kwake.


Lakini pia kutokana na kwamba mti huwa unavutia tabia ambazo zinaendana na kile unachotaka kuwa ndio maana huwa hatusikii kwamba kuna mnazi nusu, kuna mbuyu nusu, au kuna mpapai nusu. Hii ni kwa sababu mbuyu unavutia tabia zote kwake bila kuchoka na kuwa unavyotaka

Sheria hii inafanya kazi asubuhi, mchana na jioni bila ya kuacha iwe umeamua kuitumia au hujaamua kuitumia lakini bado inafanya kazi. Itumie sasa kanuni hii iliunapotaka kufika


 Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii


Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


One response to “Vutia Kwako Tabia Hizi.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X