Watu Sita Waliokuzunguka


Wewe ni tofauti na mtu mwingine yule kwa wastani wa watu sita waliokuzunguka.  Kwa lugha nyingine naweza kusema kwamba maisha yako ni wastani wa maisha ya watu sita waliokuzunguka.

Tabia zako, kipato chako, na matendo yako yote ni sawa na kuchukua wastani wa wa tabia, matendo, na kipato cha watu sita waliokuzunguka.

Kumbe kama umezungukwa na watu ambao wanafikiri kawaida, wanafanya kwa mazoea, na kutenda kwa kawaida sana. Basi na wewe maisha yako yatakuwa ya kufikiri kawaida,kufanya kwa mazoea, kutenda kwa kawaida sana.

Kumbe watu waliokuzunguka wanaweza kuwa mchango mkubwa sana kwenye mafanikio yako au wanaweza kuwa kikwazo kikubwa sana cha wewe kufikia mafanikio.

Hiki ni kipimo ambacho kinefanyiwa utafiti na kugundulika kwamba maisha ya mtu mara nyingi hayatatofautiani na wale watu sita waliomzunguka.

Sasa nifanyeje?

Ili uweze kuondokana na maisha haya ambayo ni ya kawaida sana. Maisha ya mazoea ya kufanya kitu kilekile kila siku. Unahitaji kufanya kwa tofauti.
Unahitaji kuwa na nguvu kubwa sana (msukumo wa ndani) ambayo itakusuma wewe kufanya kile ambacho unahitajii kufanya.

Unahitaji kukuza kujiamini ndani yako. Jiamini kwa kazi ile ambayo unaifanya. Jiamini kwamba wewe ndiye mwenye uwezo wa kufanya mambo makubwa. Fahamu kwamba dunia nzima inahitaji sana msaada wako. Wewe ndiye rubani na shughuli ambayo unapaswa kuifanya haijafanywa na mtu yeyote tangu dunia imekuwepo. Usipoifanya leo basi utakuwa umekwamisha zaidi ya watu bilioni saba wanaosubiri msaada wako.

Usikubali kuendeshwa kwa matendo ya watu wengine bali wewe unatakiwa kuwa kama chumvi, popote pale utakapokuwa basi kila mtu anafahamu kwamba wewe upo. Kama ambavyo chumvi huwa ikiwekwa kwenye chakula na kugundulika kwamba imo, kwenye hicho chakula au pale isipowekwa lazima inagundulika kwamba haimo basi vivyo hivyo wewe ndivyo unatakiwa kuwa. Wafanye watu wabadilike kwa matendo yako sio wewe ubadikike kwa matendo yao.

Soma zaidi; Kama Unapanga Kufanya Mambo Rahisi Maisha Yako Yatakuwa Magumu, Kama Unapanga Kufanya Jambo Gumu Maisha Yako Yatakuwa Rahisi

Lakini pia unahitaji kuchagua marafiki sahihi wa kujuzunguka kuendana na kile ambacho unafanya. Watafute marafiki sahihi watakaokupa mtazamo chanya. Hakikisha kwenye timu yako ya watu sita wa karibu sana wanakaa watu ambao wana mtazamo wa kusonga mbele sio watu wa kukurudisha nyuma.

Jiondoe kwenye makundi ya mitandaoni ambayo kwa sasa hayana msaada mkubwa kwako badala yake jiunge na makundi ambayo yataendelea kukukwamua kukutoa sehemu moja kwenda kwenda sehemu nyingine.

Soma zaidi hapa; Kwa Nini Maisha Yako Umeyaweka Mtandaoni?

Mwisho chagua orodha ya watu fulani ambao ungependa kukutana nao maishani mwako. Hawa ni watu ambao unapenda sana matokeo waliyosababisha. Watu ambao ungependa kujifunza kutoka kwao.watu ambao wamefikia mafanikio makubwa.
Sheria ya asili inasema unajivutia kwako kile ambacho unapenda kuwa, unajivutia kwako kile ambacho umelenga.

Huwezi kupata kile ambacho hutaki hata kuona wala kusikia habari zake.

Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X