Wiki Moja Bila Habari


Tupo katika ulimwengu ambapo habari zinasambaa kwa kasi kubwa sana. Tupo katika ulimwengu ambapo habari inaweza kuizunguka dunia nzima ndani ya dakika tano jambo ambalo halikuwahi kutokea miaka ishirini iliyopita.

Gazeti lenye habari hasi linauza sana kuliko gazeti lenye habari chanya, au gazeti lenye historia ya mtu maarufu sana

Gazeti lenye habari inayoeleza janga fulani la hivi karibuni litauza sana kuliko gazeti lenye utafiti wa kisayansi.

Ukweli ni kwamba ni rahisi sana kuzoea kuwa mtu wa kufuatilia habari na kusoma magazeti kuliko kusoma habari za maana. Kitu cha msinhi ni kwamba usisome gazeti bila kuwa na sababu za msingi za kusoma.

Njia nzuri sana ya kuondokana na kufuatilia habari hasi ni kupitisha wiki moja bila habari. Ndio namaanisja pitisha wiki moja bila ya kufuatilia habari kwenye redio, tv, au gazeti.  Kama utaamua kufanya hivi kuna mambo kadhaa ambayo utagundua.

1. Hutapitwa na habari yoyoye wala hutapitwa na kitu chochote. Badala yake utazipata habari hizo kutoka kutoka kwa watu wengine waliokuzunguka. Habari zote zinazotokea utazisikia kutoka kwa watu mbali mbali utakapokuwa ofisini, kazini, au hata darasani. Kumbe hili ni jambo la kwanza ambalo utaligundua.

2. Utkuwa na amani ya mwili na roho. Hii  itatokana na kwamba hutakuwa na kitu hasi kinachokusumbua. Zile habari zinazoweza kukufanya mwenye hasira. Kama vile habari za watu waliouawa, watu waliopata ajari  hutazisikia .

Soma zaidi hapa; Kwa Ninj Umeyaweka Maisha Yako Mtandaoni?

Hii itakufanya kuweza kufanya kazi zako kwa umakini mkubwa sana bila ya kuwa na mawazo  ambayo ni hasi yanayopelekea kukurudisha nyuma

Kumbuka kwamba  sio kwamba napiga vita vyombo vya habari, maana kuna kazi nyingine nzuri zinzofanywa na vyombo vya habari

Kuna vipindi mbali mbali vya tv na redio naaangali na kusikiliza vinavyoelimisha
Kipindi kama cha TEMINO CHA CLOUDS FM. Vifahamu vipindi hivyo vichache na uvifuatilie.

Lakini pia fahamu kwamba sio lazima ufuatilie kila habari na sio lazima usome kila habari zilizo kwenywe mitandao ya kijamii. Chagua habari sahihi. ambazo utahitaji kuzipata na kusikiliza .

Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii


Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X