Yaboreshe Mazingira Yako Fanya zaidi.


Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa blogu ya songa mbele. Karibu sana katika makala ya leo.

Kila mtu kakulia katika mazingira tofauti  na ya mwenzake. Mazingira haya ni kuanzia nyumbani, shuleni na jamii kwa ujumla.
Kama umekulia kwenye mazingira linapotumika jembe la mkono basi utakuwa na utaalamu na ujuzi wa kulitumia jembe la mkono.
Soma zaidi hapa; Mambo Matatu Ambayo Kampuni Yako Inapaswa Kuwa Nayo
Kama umekulia kwenye mazingira ya uvuvi basi utakuwa na utaalamu na ujuzi wa kuvua.
Kama umekulia kwenye mazingira ya wawindaji basi utakuwa na utaalamu na ujuzi wa kuwinda.
Hata kama utakuwa sio mtu unayefanya vizuri sana lakini walau utakuwa unafahamu kitu kizuri sana cha kukusaidia kutoka hapo ulipo kwenda sehemu nyingine
Haya ni mazingira ambayo umeyakuta. Kama ulikuta watu wanalima kwa jembe la mkono sasa ni wakati wako kufanya mabadiliko. Ebu yaboreshe mazingira kwa kufanya zaidi. Buni zaidi ya kutumia jembe la mkonoKama watu walizoea kupanda bila mbolea, kuwa zaidi, fanya zaidi na anza wewe kupanda kwa mbolea. Yaborehe mazingira yako kwa kufanya zaidi.

Kama watu walikuwa hawamwagilii mazao yao kwa kutegemea mvua. Sasa hii ndiyo fursa kwako kuitumia leo. Ebu fikria kuanzisha kilimo cha umwagiliaji.  Ebu fikria kulima mwaka mzima bila kuacha.

Kama watu waliokuwa wamekuzunguka walikuwa wanalima kwa ajili ya chakula sasa ebu wewe fikria kulima kwa ajili ya kuuza hadi nje ya nchi.

Ebu jione ukiwahudumia mabilioni ya watu hapa duniani. Jione kwamba  mabilioni ya watu wanafaidika na chakula chako. Jione kwamba bila ya wewe basi hawa mabilioni ya watu hawana  mwingine wa kuwasaidia. Anza sasa.

Haya yote ni mabadiliko ambayo unaweza kuyafanya sasa. Mabadiliko ambayo unaweza kuyafanya kuanzia leo.

Mabadiliko ambayo unaweza kuyafanya popote pale ulipo. Umetolewa mfano kwenye kilimo lakini bado unaweza kufanya mabadiliko popote pale ulipo, fanya mabadiliko sasa.

Mabadiliko haya unaweza kuyafanya ukiwa kwenye jamii ya wafugaji, wajenzi, wafyatua matofali lakini anza na wewe, kama wewe ni mwalimu, mwanafunzi, daktari n.k. yaboreshe maisha yako fanya zaidi badilika wewe kwanza na wengine watafuata.

Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X