Jifunze Kuvua


Kumfundisha mtu kuvua ni njia nzuri ya kumwondoa kwenye kuomba samaki maisha yake yote.” Askofu Oyedepo

Kuna mtu aliwahi kusema kwamba “Afrika ni nchi pekee duniani ambapo mtu unaweza kuokota pesa njiani wakati wananchi wake hawajaiona.”

Kuonesha kwamba wingi, uzuri, ubora wa  raslimali zilizopo mtu anaweza kuzitumia raslimali hizi kusonga mbele.

Hakuna kitu chochote kinachotokea bila gharama. Bila matendo hakuna matokeo na bila kutembea hakuna mwendo.

Maisha sio ajali kwamba inatokea kwa mtu ghafla, Bali ni zawadi  kutoka kwa muumbaji, ndio maana  wale wanaochukua hatua stahiki wanafanikiwa hakuna anayefanikiwa kwa ajali.

Huwa napenda fundisho kutoka kwenye biblia ambayo huwa inaonesha mfano mzuri kwa watu wanaokua na kuelekea kwenye mafanikio ni mfano ambao kila mtu anaweza kuiga. Mfano huu unatoka katika Kitabu cha (mithali 6:6-11)

 Ewe mvivu, mwendee chungu,Zitafakari njia zake ukapate hekima.

 Kwa maana yeye hana akida,Wala msimamizi, wala mkuu,

 Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua;Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.

 Ewe mvivu, utalala hata lini?Utaondoka lini katika usingizi wako?

Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo,Bado kukunja mikono upate usingizi!

 Hivyo umaskini wako huja kama mnyang’anyi,Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.
Mchwa hawana kiongozi lakini huwa wana uwezo wa kuweka akiba.

Mchwa wamejifunza kuvua. Hivyo hawana tena haja kuomba samaki. Na wewe jifunze kuvua.

Kwa maoni yangu kila malalamishi yoyote juu ya uongozi chanzo chake ni wananchi. Kama tutakuwa wananchi wanaotimiza wajibu wao kwa kujifunza kuvua. Kwa kuishi maisha ambayo yana manufaa kwa kila mtu kwenye jamii. Kwa kutoa kile ambacho tunategemewa kutoa basi  tutegemee uongozi unaotimiza wajibu wake. Uongozi ambao unajua kuvua samaki sio uongozi unaoomba samaki.

Kumbe kuna umuhimu mkubwa sana wa watu kubadili mtazamo wa akili zetu lakini pia kubadili mwekekeo. Tuone maisha haya ni wajibu wetu na sio wajibu wa watu wengine, wala sio serikali. Tuamke usingizini na tuige mfano wa mchwa.
Jifunze kuvua samaki.

Mwanzoni mwa makala hii nimeandika  “kumfundisha mtu kuvua samaki ni njia pekee ya kumwondoa kwenye hali ya kuomba samaki maisha yake yote.”

Huu ndio muda wetu sisi kujifunza kuvua samaki. Lakini kwa kuwa mafanikio ni kitu cha
kuwashirikisha na watu wengine basi na wewe ni wajibu wako wa kuwashirikisha watu wengine ili nao wajifunze jinsi ya kuvua samaki.
Tufikie hatua tuanze kuvua samaki wote tuache kuomba msaada nje ya nchi. Tufikie hatua ya kuwa nchi ya viwanda kwa kuvua samaki wetu wenyewe. Hii itawezekana kama Mimi, wewe na yeye tutaanza kuvua samaki leo.

Soma zaidi hapa; Anza ma Moja

Lipa gharama kwanza.
Nakubaliana na sheria ya asili kutoka kwenye fizikia inayosema.
“to every action there us equal and opposite reaction”.
Lazima uwe tayari kulipa gharama ili kupata matokeo bora ( ili uweze kula) ni katika hoteli pekee unaweza kula kabla ya kulipa gharama.

Kumbe kuvua samaki sio jambo la kutaka tu na likawepo bali unahitaji kujua kwamba kuna gharama ya kulipa kabla ya kupata kujia kuvua. Hivyo kuwa tayari kuilipa hiyo gharama sasa.
Naweza kusema kiufupi kwamba lipa gharama upate samaki.

Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


One response to “Jifunze Kuvua”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X