Kioo Hakidanganyi


Tunapoangalia kwenye kioo tunajiona sisi wenyewe. Itaonekana ajabu pale utakalalamika kwamba juu ya kile unachokiona kwenye kioo. Ni ajabu pia kubadili kioo ili upate picha ya tofauti. Kama tunataka kubadili picha ya kweye kioo lazima tujibadili sisi wenyewe. Kwa maneno mengine ni kwamba kama hutaki matokeo ya kile unachopata kwenye maisha basi unahitaji unahitaji kujibadili wewe kwanza ndani yako. Usiweke nguvu katika kutafuta kwa nini wewe umeshindwa Bali tumia kuangalia in kwa jinsi gani kushindwa kutakufikusha kukyfimisha kwenye mafanikio. Tatizo litajitokeza pale utakapotaka kuwa mtu mwingine. Pale utakapojiangalia kwenye kioo na kuona kwamba SIO WEWE Bali ni mtu mwingine. Hapo utakuwa umeamua kuwaona WATU WENGINE. Kama nilivyotangulia kusema hapo juu kwamba utavuna kile ambacho umepanda Kama unataka uwaone watu wakikuchangamkia basi wewe anza kuwa changamkia. Kama unataka kuwaona watu wakifurahia uwepo wako basi anza wewe kufurahia uwepo wao. Kile unachotoa ndicho utakachopokea. Mazingira yaliyokuzunguka hayatatoa matokeo tofauti na kile ambacho umwewekeza. Mtazamo mzuri, matokeo mazuri, matazamo hafifu matokeo hafifu. Matazamo mbaya basi huleta matokeo mabaya. Kumbe wewe ndiye unayetengeneza mazingira yako. Wewe ndiye unayebadili mazingira yako. Hakuna mtu mwingine. Anza kubadili mazingira ya ndani mwako ili upate matokeo bora. Usibadili kioo bali jibadili wewe mwenyewe. Siku zote unapaswa kuwa na mwelekeo. Usiwe kama kinyonga kwamba unasubiri kitu chochote kitakachotokea ufanye. Unapoanza siku yako ianze kwa kuwa na mwelekeo mzuri wa kukupeleka pale unapotaka. Anza kuandika mambo ambayo utayafanya ndani ya siku. Usisubiri kupeperushwa kama bendera ambayo hufuata upepo. Anza kwa kuilisha akili yako kilicho bora ili upate kilicho bora. Anza siku kwa kujenga mtazamo chanya. Badili kioo sasa upate kilichobora maana kioo hakidanganyi

Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X