Tupo katika dunia ambayo mambo yake yanabadilika kila siku asubuhi mchana na jioni.
Kutokana na mabadiliko hayo basi sisi wenyewe tunahitaji kubadilika. Maana ni asili kwamba vitu lazima vibadilike.
Miaka 20 iliyopita intaneti ilitumika kwa ajili ya kutuma na kupokea e-mail lakini leo mambo yamebadilika.
Miaka 20 kujifunza ilikulazimu uende darasani ukamsikilize mwalimu, leo hii hata ukama upo chumbani kwako unaweza kujifunza kitu chochote unachotaka.
Miaka 20 iliyopita benki zilikuwa mjini hivyo kuweka au kutoa pesa ilikulazimu uende umbali mrefu ili kupata huduma, leo hii benki unatembea nayo mfukoni mwako na unaweza kuweka au kutoa pesa muda wowote.
Miaka 20 iliyopita maktaba zilikuwa chache sana ena zilikuwa kwenye baadhi ya taasisi kama shule, sekondari na vyuo.
Leo hii maktaba unatembea nayo mkononi popoe pale ulipo, uwe nyumbani, kazini, au safarini.
Weka mpango madhubuti sasa kuhakikisha miaka 20 ijayo hauachwi na mabadiliko haya ambayo yanazidi kutokea sasa hivi.
Zama zimebadikika, maisha yamebadilika, ajira hatarini, ebu na wewe badilika.
Miaka 20 ijayo inajengewa msingi mkubwa sana leo.
Miaka 20 ijayo sio mingi kama ambavyo unafikiria lakini usipoiwekea mpango wako leo basi sina uhakika kati ya kauli hizi utaitumia ipi ila wewe unajua
1, maeneo haya yalikuwa yananunuliwa kwa gharama ndogo miaka 20 iliyopita ila leo yamepanda bei.
2. Unamwona JOSE tumesoma wote tangu shule ya msingi mpaka chuo bana. Tulikuwa tunakula wote, na kucheza wote. Ila ona leo hii amefanikiwa.
Kama vile anapotafuta mafanikio sasa hivi amekufunga mikono wewe.
3. Unamwona MUSA darasani alikuwa kiraza ila leo hii anamiliki hoteli kubwa hapa mjini nadhani atakuwa amejiunga freemason au anasukuma madawa.
Hakika hata wale utakaowambia hivi hawatakuvumilia lazima wewe wakuhoji tena kwa nguvu zao zote.
Naamini moja kati ya maswali yatakatojitokeza. Maswali ambayo utaulizwa ni
1. Je hao walipokuwa wanafanya kazi wewe ulikuwa wapi?
2. Je kama wewe hukuwa kiraza kama MUSA mbona leo Musa kakupita kimaendeleo. Kwa hiyo nani kiraza? Wewe au Musa?
Sasa sijui wewe utajibu nini?
Ila jibu zuri na la pekee unaweza kuliandaa sasa. Maana kile unachokifanya sasa kitaongea zaidi ya maneno ambayo ungeongea.
Fanya mambo yako mazuri sasa kwa kuitengeneza baadae yako.
Andika mpango mzuri sasa
Kama kuna jambo la kufanya basi lifanye sasa.
Kama kuna kitu unataka kukifanya basi kiandikie mpango wake sasa. Zingatia mambo yafuatayo kwenye mpango wako.
Mambo muhimu ya kuzingatia kuhusu malengo
1. Andika malengo yako chini. Malengo yako yaandike na yape ukomo. Kama ni pesa andika ni kiasi gani cha pesa ambacho utamiliki kufikia muda huo uliouweka.
Kama ni nyumba andika ni nyumba ngapi utakuwa unamiliki kufikia muda wako wa ukomo.
2. Angalia ni huduma gani utatoa ili kupata kile ambacho unataka. Hakuna kitu ambacho unaweza kukipata tu bila ya kuweka juhudi. Lazima ulipe gharama kwanza kabla ya kupata
Anza kutekeleza mpango wako haijalishi uko tayari au la! Usiseme kwamba nitaanza kesho maana huwa hakuna kitu kama hicho. Kama hutaweza kuanza leo basi itakuwa vigumu wewe kuanza kesho..
4. Soma malengo yako kila siku. Yasome asubuhi mchana na jioni. Wakati unasoma jione kama vile wewe tayari unamiliki hicho kiasi cha pesa
Soma zaidi hapa; Kipaji ni nini?
Anza kutenda.
Malengo tu bila ya kuweka mpango wa kufanya kazi hautoshi. Usiishie kuweka mpango bali anza kutenda kwa nguvu yako yote bila kuacha. Hakuna mafanikio ambayo utakuta njiani. Ijenge miaka 20 ijayo leo.
Jifunze kila siku.
Kuna mtu aliwahi kusema
Miaka mitano ijayo utakuwa hivyo hivyo isipokuwa kwa vitabu unavyosoma na watu waliokuzunguka.
Basi na wewe miaka 20 ijayo utakuwa hivyo hivyo ulivyo isipokuwa kwa vitu viwili vitabu na watu waliokuzunguka. Chagua viabu sahihi ambavyo vinaendana na kile ambacho unataka kupata miaka 20 ijayo. Kama unafanya uwekezaji basi leo hii anza vitabu vya uwekezaji kwa ajili ya miaka 20 ijayo.
Anza sasa
Soma zaidi hapa; Kama Unapanga Kufanya Jambo Rahisi Maisha Yako Yatakuwa Magumu
Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
BONYEZA HAPA KUPATA KITABU CHA BIASHARA NDANI YA AJIRA
Kujiunga kundi la wasapu la SONGA MBELE BONYEZA HAPA