Unayofikria Hayawezekani Yanawezekana


Je, unaamini katika miujiza? Je, unaamini kwamba mambo ambavyo unafikiri au watu wengine wanafikiri hayawezekani yanawezekana?
mimi naamini hivyo? Yasiyowezekana yanawezekana. Hivi ushawahi kujiuliza ni kitu gani kinafanya watu zaidi ya 1000 wanaingia kwenye ndege na kupaa? Au kwamba upo nyumbani kwako umekaa na unamtumia mtu meseji aliye mamilioni ya kilomita kutoka ulipo na inamfikia? Yasiyowezekana yanawezekana. Hayo yote ninayosema hapo kama ungeyasema miaka kadhaa kabla ya kuwepo ungeonekana kichaa. Lakini leo tunayaona yapo na tunafurahia.

Mpaka mwanzoni miaka 1900 dunia nzima iliamini kwamba haiwezekani kitu chochote kurushwa angani na kukaa kwa muda mrefu bila kuanguka.
Walijitokeza vijana Wawili wanojukikana kama WRIGHT BROTHERS  ambao ndio walikuwa wa kwanza kuirusha angani ndege na kuonesha kwamba inawezekana.

Badilisha imani za watu sasa rafiki. Ebu waoneshe wale wanaosema kwamba haiwezekani wewe kufanya Biashara ukiwa ndani ya ajira kwamba inawezekana.
Ebu waoneshe hao kwamba huwezi kuwa chuoni na kufanya shughuli nyingine za kimafanikio kwamba inawezekana.
 Kuwa kama hao vijana hao Wawili ambao waliweza kuibadilisha imani za watu. Kama hawa waliweza kwa nini wewe usiweze, inawezekana.

Mpaka 2004 dunia haikuwa na habari za kitu kinachoitwa mtandao wa kijamii ambao ungeweza kuwaunganisha watu wa dunia yote kwa wakati mmoja. Mtandao ambao ungeweza kumfanya mtu maarufu ndani ya dakika tano.

Kijana mmoja anayejulikana kama Mark Zuckeberg ndiye aliyebadikisha mtazamo wa dunia nzima kwa kufanya maajabu ya tofauti. Akaiunganisha dunia kama sasa mbavyo kila mmoja wetu mpaka sasa  anaweza kuona.

Na wewe unaweza kuiunganisha dunia kwa bidhaa au huduma zako ambazo utaanza kuzitoa sasa. ANZA NA MOJA.

Miaka mitano iliyopita hakuna mtu ambaye angeweza kuiambia dunia  kwamba mfanya biashara anaweza kuwa raisi wa nchi  kama Marekani.
Kinyume ma matarajio ya wengi baada ya kupitia nyakati ngumu kwa muda mrefu ameweza kuingia ikulu na kuwa raisi wa nchi yamarekani.
Yasiyowezekana yanawezekana.

Miaka 6000 iliyopita dunia nzima iliaamini kwamba huwezi kulima wala kipanda kutu chocjote sehemu ambavyo ni name. Lakini watu wa babiloni waliishangaza dunia kwa kufanya kitu ambacho kilikuwa hakiwezekani kwa wakati huo na waliweza kupanda mazao sehemu ambavyo ni Kame. Kwa kujenga mifereji na kufanya Kilimo cha umwagiliaji.
Yasiyowezekana yanawezekana.

Fanya mapinduzi yako kwa kuionesha dunia kwamba inawezekana na wengine wataiga kwako.

Wakati unafanya yote hata kumbuka kwamba dunia haisimami. Kwa hiyo ufanye kazi au usifanye bado dunia itaendelea na mzunguko wake bila ya kuathiriwa na wewe.
Kumbe na wewe fanya kazi maana dunia yenyewe ipo kazini.


Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii


Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X