Ni rahisi sana kuwalalamikia watu wengine juu ya kile ambacho wamefanya
Lakini kumbuka kwamba watu wote duniani hawawezi kufikiri na kutenda kama wewe.
Lazima iwepo tofauti na Mara nyingi tofauti hizi ndizo huleta maendeleo.
Ni kwa sababu ya tofauti zilizopo kati ya mataifa makubwa ambazo zimeleta maendeleo na ugunduzi mkubwa wa vitu mbali mbali hapa duniani.
Kama watu wote wangegikiri na kutenda kwa namna ileile basi dunia ingekuwa sehemu ambayo inachosha sana kuishi..
Soma zaidi; Acha Kulalamika Anza Kuishi
Unapoamua kuanza kulalamika kwa nini watu hawajafanya kitu fulani maana yake umeamua kutoona ubora ambao ni zaidi ya asilimia 80% na kuweka nguvu kwenye ile asilimia 20%, ambavyo inaweza kuwa ya ubaya.
Kitu chochote hata kama ni kidogo ukikifuatilia Mara kwa mara hatimaye kitakua na kuonekana ni kikubwa.
Kwa hiyo hilo jambo ambalo linaoonekana ni dogo ukizidi kulifuatilia na udogo wake, ukizidi kulipa nafasi akilini mwako litakua na kuonekana kubwa sana.
Ili kuanza kishi maisha ya furaha anza kuuona utajiri wa jamii zetu umelala katika tofauti zetu.
Kuanzia leo acha kulalamika, kubali, kubeba majukumu ya maisha yako.
Jibadili mwenyewe kabla ya kutaka kuwabadilisha wengine
Ni vigumu sana kuwabadili wengine ila ni rahisi sana wewe kujibadili.
Ukitaka uwabadili watu, anza kwa kujibadili mwenyewe wengine watafuata.
Vutia kwako tabia unazotaka na wengine wataiga.
Chukua maisha yako mikononi mwako. Usibebe maisha ya wengine.
Utaelemewa maana ni vigumu Kuyabeba maisha ya wengine na kutaka kuyabadilisha.
Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA