Ijumaa kuu ni siku ambavyo wakatoliki wote huwa wanakumbuka mateso ya Kristo.
Lakini siku tatu baade ambavyo ni Jumapili wakristo hao huwa wanashangalia kufufuka kwa Kristo.
Wahenga walisema mtaka cha uvunguni shafti ainame. Ili Yesu afufuke ilibidi kwanza ijumaa ya mateso ianze ateswe na afe.
Hiyo pia ndiyo siri Kubwa sana ya mafanikio. Ili ufikie hatua kubwa sana ya ya mafanikio, ili ufahamike kama mtu ambaye ameleta mabadiliko huna budi kwanza kuwa na ijumaa kuu kwanza.
Hiyo kanuni inafanya kazi katika sekta zote za ualimu, udaktari, Biashara, uandishi, ukulima, kutaja machache.
Dakatari maarufu aliyefanya upasuaji wa kwanza wa watoto mapacha walioshikana (seamese twins).
Dr. Ben Carson alikuwa anasoma masaa matano kila siku darasani. Alikuwa anasoma zaidi ya Kile ambacho amefundishwa darasani na anasoma kwa undani kabisa. Hii ilikuwa ni ijumaa kuu.
Mgunduzi wa taa za umeme Thomas Edison alikuwa analala masaa manne kila siku huku akifanya masaa 20. Hiyo yote kwake ilikuwa ijumaa kuu kabla ya pasaka.
Usiogope kutoka ijumaa kuu kwenda jumapili ya pasaka ni siku Tatu tu.
Itumie ijumaa kuu kufanya kazi.
Fanya kazi ukijua kwamba kuna jumapili ya pasaka mbele yako inakuja.
Siku ambayo utafurahia kazi ambayo ulikuwa unafanya kwa kupata matokeo bora. Iruhusu ijumaa kuu itokee ili uweze kipata jumapili ya pasaka.
Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA