Ifahamu Karatasi Ya Dhahabu


Habari za leo Rafiki yangu, na ndugu msomaji wa blogu yako ya songs mbele. Karibu sana katika makala yetu ya leo ili tujifunze kitu kipya kitakachotufanya tuendelee kuwa vijana hata kama tuna miaka zaidi ya 80 kama anavyosema Dharma “kusoma kunaweza kukufanya kuwa kijana hata kama una miaka 80 na kukufanyabkuwa mzee hata kama una miaka 20″

Najua kwamba kuna mambo mengi sana ya kufanya kila siku,  na katika kila sekunde yako ambavyo unaipata. Huwezi kufanya kila kitu kwa wakati huohuo.

Lazima uwe makini sana katika utendaji wako. Usiwe mtu wa kufanya kila kitu kinachokuja mbele yako.
Waswahili wanasema njia mbili zilimshinda fisi.
Njia nzuri ambayo itakufanya uweze kufanya kazi zako kwa wakati na kumaliza Kile ambacho unapaswa kufanya ndani ya siku husika ni kutembea na karatasi ya dhahabu au notebook ya dhahabu.

Notebook ya dhahabu inakuwa na malengo yako kwa ufupi sana.
Hii utakusaidia sana kutembea na malengo yako popote pale uendapo na utayasoma muda wowote ule ambao utakuwa umetulia au muda ambao utaona unafanya kitu ambacho hakiendani na malengo yako basi itakuwa rahisi sana kwako kujikumbushia.

Notebook hii ni ya kutembea nayo na unakuwa nayo popote pale uendapo na unaweza kuitumia hasa pale utakapokuwa safarini,
Kuanzia leo tengeneza notebook ya dhahabu yenye malengo yako kwa ufupi.
Lakini pia anza kuitumia popote pale uendapo safarini, kazini au sehemu ambapo utakuwa mbali kidogo na nyumbani.

Mambo ya kufanya leo.
1. Andika malengo yako kwenye karatasi ya dhadhabu kwa ufupi.
2. Anza kutembea nankaeatasi ya dhahabu kila siku.
3. Washirikishe wengine juu ya hili ili nao wajifunze

Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii


Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X