Jifunze Kutoka Matukio Ya Zamani


“experience is a best teacher
Uzoefu ni mwalimu mzuri huu ni msemo wa kiingereza ambao binafsi huwa napenda kuutumia. Huwa unanipa nguvu ya kujifunza kutoka kwenye makosa yangu ya zamani, kuyafanyia marekebisho na kuja na kitu kipya Kizuri na bora zaidi.

Usiweke nguvu kubwa sana kwenye makosa yako ya zamani au matatatizo yako ya zamani na kujiona hufai, dunia haikutendei haki na dunia sio sehemu nzuri sana ya kuishi.
Hii itakuzuia kutafuta suluhisho la matatizo ya sasa lakini pia itakuzuia na kukuibia sehemu ya mafanikio yako ya baadae. Makosa ya zamani yatumie kama nafasi ya wewe kujifunza na kukusaidia kuzidi kusonga mbele.

Katika hali mbaya kuna nafasi nzuri ya kufanya vizuri kuna mtu ambaye aliwahi kusema kwamba kama umekumbana na hali mbaya katika maisha yako bila shaka unaandaliwa kuja kufanya jambo kubwa sana kwenye maisha yako.

Vitumie vikwazo vya sasa kama daraja la wewe kujikwamua na kuhakikisha unainuka na kuzidi kusonga mbele.
Tambua kwamba kama wewe umeshindwa zaidi kuna nafasi kubwa ya kwamba unaishi maisha ambavyo unastahili kuwa unaishi.
Ni vizuri kuanza kitu na kushindwa kuliko kutoanza kabisa.

Ni vizuri kutumia maisha yako kwa kutafuta na kufanya zaidi kuliko kutafuta usalama.
Kama unatafuta Uhuru wako binafsi huwezi kuupata kwa kuutafuta sehemu salama! Maana sehemu ambavyo ni salama zaidi ni gerezani lakini watu wa huko hawako huru.


Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X