Kilichofanywa Na Huyu, Nami Naweza Kufanya.


Habari za leo rafiki yangu na ndugu msomaji wa blogu yako ya songambele karibu sana katika makala ya leo .
Tunaenda kuijifunza kitu kipya chenye manufaa mamkubwa sana kwetu.

Kuna mtu mmoja ambaye alikuwa ameandika kwenye ubao maneno fulani na maneno hayo aliyaonesha  kwa kila mtu aliyekuja kwake ma maneno ya kukatisha tamaa. Meneno hayo yalikuwa katika nyumbabyake ukutani. Na yalisomeka hivi

Alishindwa katika biashara mwaka 1831

Hakuchaguliwa kuwa mmoja wa watunga sheria mwaka 1832

Alishindwa tena katika biashara Mwaka 1833

Alichaguliwa kuwa mmoja wapo wa watunga sheria Mwaka 1834

Mke wake alifariki Mwaka 1835

Alichanganyikiwa mwaka 1836

Alishindwa kuchagukiwa kuwa “elector” mwaka  1840

Alishindwa kuingia kwenye congress mwaka 1843

Alishindwa kuingia kwenye congress mwaka  1845

Alishindwa kuingia kwenye congress mwaka 1848

Alishindwa kuwa seneta 1855

Alishindwa kuwa makamu wa rais 1856.

Alichaguliwa kuwa raisi mwaka  waarekani mwaka  1860

Huyo anazungumuziwa hapo sio mwingine bali ni raisi wa 16 wa marekani Abraham Lincoln.

Sasa mbali na kushindwa mara nyingi lakini bado raisi huyu hakukata tamaa, bali aliendelea kupambana bila kuogopa.

Kumbe usiogope hata kidogo unaposhindwa mara moja au zaidi mara moja bali endelea kwa nguvu zako ili uweze kufikia kwenyeafanikio.

Mwandishi Napoleon Hill aliwahi kusema mafanikio huwa yanakuja kama mtego mara nyingine yanaweza kuja katika mfumo wa kushindwa.

Na mtu mwingine aliwahi kusema kwamba
Watu waliofanikiwa tunawafahamu kwa jambo moja ambalo wamefanikiwa, lakini hatuwafahamu kwa yale mengi ambayo wameshindwa.

Rafiki yangu najua mpaka hapo ushaona mwelekeo wangu wa kile ambacho nataka kusema.

Kumbe kushindwa ni tuta katika barabara kuu. Kushindwa ni hakukuzuii wewe rafiki kusonga mbele bali kunakupa mwanya wa kutulia kidogo ili uweze kuendelea tena mbele.

Kushindwa naweza kusema kwamba ni kama refa kapuliza kipenga cha mapumuziko  baada ya dakika 45.

Refa anapopuliza kipenga cha mapumuziko hamaanishi kwamba mpira umeisha. Bali ni muda wa kujipanga kabla ya kuingia kipindi kingine.
Raisi Abraham Lincoln anatupa mfano mzuri wa jinsi gani kushindwa ni kama mapumziko kabla ya kurudi cha pili?
Wewe kushindwa kwako ni muda wa mapumziko?

Kushindwa ni kama giza la usiku linapoingia. Giza linapoingia linakusaidia kuziona nyota. Vivyo hivyo kwa raisi Abraham Lincoln wa marekani. Kushindwa kwake kulikuwa ni giza ambalo lililkuwa linamsaidia kuziona nyota. Alikuwa akiona nyota zaidi na kuzidi kusonga mbele. Kushindwa kusiwe tatizo Bali kuwe fursa kubwaa sana ya wewe kuzidi kuendelea mbele.
Lincoln alikuwa akiziona nyita pale alipokuwa anashindwa na baadae sasa kuamua kuchukua hata kubwa zaidi.

Mara nyingi wengine wakikutana na kikwazo au kizuizi huwa wanaacha kwa kutegemea watakuja kufabya baadae.
Hii sio kweli.
Kizuizi kione kama Giza la kukuonesha nyota.

Ukishindwa furahi maana baada ya hapo kuna ushindi mkubwa sana unakuja mbele yako.

Kuna mtu aliwahi kusema “ Njia ya kwenda kwenye mafanikio haikunyooka. Kuna kona inayoitwa kushindwa,  sura ya kitanzi inayoitwa kuchanganyikiwa, matuta ya kupunguza sipidi yanaoitwa marafiki, taa nyekundu zinazoitwa adui, taa za kutoa onyo zinazoitwa familia

Utakuwa na taili za pancha zinazoitwa Kazi, lakini ukiwa na taili ya akiba inayoitwa kupania kitu, na injini inayoitwa uvumilivu, dereva  anayeitwa nguvu ya nia, utaweza kufika panapoitwa mafanikio”

Hivyo usiogope vitu vinavyojitokeza njiani  ili kupunguza spidi yako wala usiogope milima mabonde, njia zilizopindapinda, mapango, mashomo marefu, matuta, vipangamizi na matuta.

Kwa  sababu unayo taili ya akiba inayoitwa kupania, nguvu ya akiba inayoitwa uvumilivu, dereva  anayeitwa nguvu ya nia”
Ni kwa msingi huo namalizia kwa kusema maneno ya baba wa taifa hili la Tanzania Mwalimu Nyerere anasema “Uwezo tunao, sababu tunazo na nia tunayo”

Sasa na wewe sema kwamba uwezo wa kupambana ninao kama Abraham Lincoln hata kama nitashindwa mara
 kadhaa,
Sababu za kupambana kama Abraham Lincoln ninazo.
Na nia ya kupambana kama Abraham Lincoln ninayo.
Usikate tamaa kushindwa sio mwisho

Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X