Kitakachokutoa Sifuri Mpaka Moja


Habari za leo rafiki yangu, imani yangu siku ya leo  umeianza vyema sana. Karibu sana katika makala yetu ya leo tunapoenda  kujifunza kitu kipya ambacho kitabadilisha maisha yetu na kutuinua kututoa sifuri mpaka kileleni. Ndio namaanisha kutoka sifuri mwaka kileleni.

Kitu hiki kimo ndani yako na hiki ni kitu ambacho umezaliwa kufanya hapa duniani yaani ni kusudi la maisha yako.

Ukikifahamu kitu hiki basi utakuwa  katika njia ya kutoka sifuri mpaka kileleni

Muda mwingine inaweza kuwa vigumu kulifahamu jambo hilo hapo basi hapo utahitaji marafiki, wazazi, walezi, walimu, washauri au hata makocha wako waweze kukusaidia juu ya hili suala.
Watumie vizuri sana hawa watu kwa ajili ya manufaa yako. Wasikilize wanasema nini ili upate kitu bora sana cha kujifunza kutoka kwao.

Kila siku, kila muda jiulize hili swali. Mimi……….(weka jina) nmekuja hapa duniani kufanya nini?
Andika kinachokuja kichwani mwako na jaribu kukifanyia kazi.

Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X