KONA YA SONGA MBELE; Hili Ndilo Jambo Linalolipa Sana.


Habari za leo Rafiki yangu imani yangu siku ya leo umeianza vyema sana ukiwa mwenye furaha na amani. Na unaenda kufanya maku wa sana siku ya leo.

Karibu sana katika makala za kona ya songa mbele ambazo huwa zinakujia mara moja kwa wiki siku kama ya leo.
Leo tuangalie kwa umakini kitu ambacho kinachopatikana katika vitabu.

Kusoma kuna kufanya uwe kijana hata kama una miaka 80 na kutosoma kunakufanya mzee hata kama una miaka 20
Sharma.
Tupo katika ulimwengu ambapo kila kitu kinabadilika kwa kasi kubwa sana. Mabadiliko haya yanakuhitaji na wewe uwe mtu wa kubadilika ili uweze kuendana na hali hii
Nilipogundua kwamba mabadiliko yanatokea kwa kasi kubwa sana niliongeza muda wangu wa kufanya kazi mara dufu
Donald Trump

Wakati mabadiliko haya yanaendelea kutokea dunia ipo katika mizunguko yake ya kawaida bila kubadilika. Bado dunia inaendelea kujizungusja kwenye muhimili wake na kulizunguka jua.
Kutokana na mabadiliko haya basi tunahitaji kujifunza mambo mapya kutoka kwa watu ambao wamewahi kufanya kitu kama kile ambacho na
tunataka  kufanya. Hivyo hatuna budi kusoma ili kujifunza kutoka kwao ili tujue na wao waliwezaje kufanikisha kile ambacho walikifanya.
Ni wazi kwamba tuna ndoto tofauti na za wale wengine ambao tutasoma vitabu vyao lakini utoafauti huo hauwezi  kutufanya tusijifunze kitu kutoka kwa watu maarufu waliofanikiwa
Ni ajabu sana kwa sasa kufanya kazi na kurudia kosa ambalo lilifanywa na watu wa karne ya 20. Kosa ambalo ungeweza kuliepuka ila kwa sababu tu hujasoma basi umerudia kosa lilelile.

nitawezaje kusoma vitabu wakati kusoma sio hobby yangu
Hili ni swali ambalo watu wengi sana wamekuwa wanauliza. Nimeona ni bora sana nilijibu hapa ili kila mmoja apate kufaidika.
Kusoma hakuhitaji kuwa hobby. Ila kwa kuwa wewe upo katika dunia hii na kuna kazi au shughuli yoyote unafanya. Iwe upo shuleni, umeajiriwa, umejiajiri, , una mpango wa kuajiri, kujiajiri au kuajiriwa. Basi wewe fahamu kwamba sio wa kwanza kufanya shughuli hiyo. Kuna watu wengi sana ambao wamewahi kufanya shughuli hiyo hiyo kama ambavyo na wewe unafanya au unataka kufanya. Sasa waliwezaje?  Jifunze kupitia hao.
Soma zaidi hapa: Huu Ndio Ujumbe Aliouandika Raisi Wa Marekani
Naomba nikuulize maswali yafuatayo na unijibu kwa umakini.
1. Je umewahi kukaa na kufikiria juu ya kufanya jambo fulani ambalo dunia nzima itasimama na kuanza kuliangalia kwa jicho la pili?
2. Je umewahi kufikiri jina lako likiongelewa basi kila mtu anamfahamu nani anaongelewa?
3. Je, ungependa kuingia kwenye chumba ambapo kila mtu akikuona basi anajua wewe ni nani?  Anasimama kuushangilia ushindi wako?
4. Je umewahi kufikiri juu ya kusafiri kwenye ndege au  kuwa na ndege binafsi ukisafiri kwa raha zako?
.
Kama umejibu
ndio kwenye mojawapo ya maswali hapo juu basi wewe huna budi kujifunza kutoka kwenye listi ya watu maarufu. Watu waliofanya vizuri kwenye maisha katika dunia hii.
Lakini kabla sijaendelea zaidi naomba naomba tena ujibu hata maswali ya hapa chini kwa umakini.
Je, kwenye ratiba yako ya kila siku huwa unasoma Kitabu kitakatifu? 
Je kuna kitu huwa unaandika wakati unasoma?
Je, huwa unajisikiaje wakati unasoma?
Je, huwa unasoma kitabu Kitabu chochote kingine tofauti na Kitabu kitakatifu? 
Je, Kitabu hili ni cha kuelimisha kuhamasisha, kutia matumaini, au cha kisayansi?
Je huwa unaandika kitu wakati wa kusoma?
Je huwa unajisikiaje wakati unasoma?
Kama sehemu ya kwanza ya maswali ulijibu ndio na sehemu ya pili ya maswali kuna sehemu umejibu hapana basi jua kwamba hapo kuna tatizo.
Anza kuongea na watu maarufu, anza kuongea na wanamziki maarufu, ongea na maraisi mashuhuri kwa kusoma vitabu.
Sasa nitaupata wapi muda wa kusoma vitabu?
Hili ni swali ambalo huulizwa na watu wengi sana.
Huwa mtu akiniuliza swali kama hili basi huwa na Mimi namuuliza huwa anapata wapi muda wa kupiga mswaki?
Au huwa anaupata wapi muda wa kula?
Huwa anaupata wapi muda wa kulala?
Kama vitu hivi vyote vinaweza kipatiwa muda wake basi kumbe muda wa kusoma unaweza kupatikana!!
Ukitaka kupiga mswaki huwa huanzi kuuliza “leo nipige mswaki au niache? 
Huwa huulizi leo nile au niache?
Huwa huulizi leo nilale au nihairishe?
Hivi ni vitu ambavyo huwa unafanya bila shuruti
Kumbe maneno hayo yanatuleta kwenye pointi ya kwanza ambayo ni.
1. Tabia.
Kila kitu ukikijengea mazoea ya kukirudia Mara kwa Mara kwa muda mrefu kinafikia hatua tunasema kimekuwa tabia.
Kumbe kusoma ni tabia ambayo tunapaswa kuijenga.
Ifikie hatua uwe unafanya kama ambavyo huwa unaweza kwenda kupiga mswaki bila kuuliza.
Ndani ya masaa 24 ya kila siku tenga dakika 20 ila za kusoma kitabu.
.kati ya dakika 1440 ambazo unazo kila siku utakuwa umebaki na dakika 1420.
Hapa Nina hakika hata kama utakuwa umebanwa kiasi gani huwezi kukosa dakika 20 tu za kusoma Kitabu.
Ukijijengea tabia hii na kuirudia  mara kwa mara utakuwa na uwezo kusoma kitabu kimoja kwa mwezi sawa na vitabu 12 kwa mwaka. Hii siyo hatua ndogo sana.
Kumbuka kwamba dakika 20 kiwe kiwango cha chini kabisa lakini sio kikomo chako.
Unaweza kuongeza kuda kadri uwezavyo.
Na ninaposema kwamba usome Kitabu kimoja kila mwezi simaanishi kwamba kiwango hicho ni kiwango cha kimataifa Bali ni kiwanho cha chini kwa msomaji anayeanza..
2. Kulala mapema kuamka mapema.
Early to bed early to rise makes a person healthy wealthy and wise. Huu ni msemo wa kiingereza unaomaanisha kwamba 


Kulala mapema, kuamka mapema kunamfanya mtu mwenye afya njema, tajiri na mwenye busara.

Watu wengi maarufu ni watu ambao huwa wanaamka mapema kabla ya kelele za dunia kuingiza vitu vipya vizuri.
Ndani ya muda huu unaweza kufaya tafakari, lakini pia ni nidhamu kubwa sana unakuwa unajijengea.
Kuna mtu alisema kwamba “ukilipoteza SAA moja la asubuhi basi utakimbizana siku nzima kulitafuta” 
Moja ya njia ya kuepuka kukimbizana siku nzima ukiutafuta muda kusoma ni kuamka mapema.
Thomas Edison alikuwa analala masaa manne alipoulizwa kwa nini?
Alisema
Kikubwa ni ubora wa usingizi sio muda wa kulala.
Ili kuamka unajitaji kulala mapema. Haya mambo yanaendana.
Soma! soma! soma!
Soma vitabu ambavyo watu wengine hawasomi.
Haruki Murakani aliwahi kusema 
Kama unasoma vitabu ambavyo kila mtu anasoma utafikiri kwa namna ambayo kila mtu anafikiri .
Soma vitabu vikubwa ambavyo watu wengine hawasomi, soma vitabu ambavyo wengine wanaogopa kusoma.
Kama unataka kuishi kwa namna ya tofauti sikia anachosema Groucho Marx
Nimekuta TV inaelimisha. Kila muda mtu akifungulia TV Mimi naenda chumbani kusoma kitabu.
Utumie muda wako vizuri kusoma vitabu. Kitabu ambacho wenzako wanaogopa kukiona hata kwa macho chukua hicho ukisome. Wenzako wakianza kusikiliza na kuangalia habari chukua Kitabu ukasome. Kumbe huna budi kufuata msemo wa wahenga waliosema “ndugu wakipigana chukua jembe ukalime, wakipata chukua kapu ukavune’
3. Sikiliza vitabu vilivyosomwa.

Nyumba ambavyo haina Kitabu ni sawa na mwili ambao hauna roho alisema Marcus Tukius Cicero.

Kwa sasa maisha yamerahisishwa zaidi nyumba yako yenye kitabu unaweza kutembea nayo popote. Nyumba yako kwa sasa ni simu yako au kompyuta.
Katika simu yako unaweza kujaza vitabu vya kila aina na unaweza kuvisoma ukiwa safarini au nyumbani.
Kumbe kwa sababu hiyo maneno ya Cicero kwa sasa tunaweza kuyabadili na kuyasema kwa namna hii. Simu au kompyuta ambayo haina Kitabu ni sawa na nyumba ambayo haina roho.

Kikubwa zaidi katika ulimwengu wa sasa unaweza kutembea na vitabu vilivyosomwa, unaweza kusikiliza vitabu ukiwa safarini, wakati unaenda kazini hii itakusaidia kufika ukiwa na hamasa kubwa sana na bila kuchoka.
Kwa nini usijaribu hii leo. Anza sasa.

Kumbuka kwamba vitabu vipo vingi ila muda upo kidogo alisema Frank Zappa.
Kumbe wewe unaweza kujitahidi kuvitafuta vitabu ambavyo unaona vinakufaa katika sekta yako ambayo unashughulika na kila kitu.

4. Utumie vizuri muda wa safari.
usisahau kitabu Kitabu unapokuwa safarini. Badala ya kuingia kwenye gari na kuanza kulala, kulalamika kwamba haufiki unapotaka kwenda! Tembe na Kitabu popote pale ulipo.
Anna Quindlen anasema kwamba “vitabu ni ndege, garimoshi na barabara.”
Haya aliyaandika katika Kitabu chake cha How Reading Changed my life. Jinsi Kusoma Kulivyobadili Maisha Yangu.

5. Punguza Muda Wa Kuangalia TV.
Punguza muda wa kuangalia vipindi vya TV ambavyo having manufaa makubwa sana kwako.
Punguza sana vipindi vya redio ambavyo havina Tina kubwa sana kwako. Ben Carson anasema “nilikuwa naangalia vipindi viwili vya TV kila wiki”
Kumbe na wewe unaweza kufanya hivyo ili update muda zaidi wa kusoma vitabu na kufanya shughuli zako nyingine.

Soma zaidi; Wiki Moja Bila Habari

Kuna mtu mmoja aliwahi kusema “mtu mmoja, mwalimu mmoja na mtotommoja wanaweza kuibadili dunia”

Na Mimi huwa naamini kwamba kama Kitabu kimoja kinaweza kuibadili dunia. Basi makala moja, insha moja, sentensi moja inaweza kumbadiki mtu. Na neno mojaboia linaweza kumbadiki mtu.

Makala zaidi; Umuhimu Wa Kusoma Vitabu Na Makala Za Kuelimisha

Utumie vizuri muda wa safari

Vitabu vitatu vya kusoma kabla Mwaka Huu haujaisha

Hii ni sentensi iliyonichekesha

Tukutane wiki ijayo kwenye makala ya KONA YA SONGA MBELE.

Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii


Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X