Sasa tuangalie leo kwenye kona ya songa mbele kuna nini?.
Zaeni muongezeke mkaijaze nchi.
Baada ya Mungu kumuumba mwanadamu alimwambia maneno hayo. Maneno ambayo Mungu alilenga juu ya suala zima la kuendeleza kizazi. Katika suala zima la kuzaa na kuongezeka naweza kusema binadamu amefaulu kwa maksi za juu sana mpaka sasa hivi ninapoandika makala hii.
Lakini tatizo linakuja katika kauli hii ya pili ambayo Mungu aliisema.
Mkatawale samaki wa baharini na ndege wa angani
Hapo ndipo bado kuna shida. Tena shida kubwa sana.
Mungu aliposema mkatawale alikuwa anatutaka tuvitumie vizuri vitu vilivyotuzunguka kwa manufaa yetu. Shukrani nyingi sana ziwaendee baadhi ya watu ambao wameweza kuitiisha dunia kwa mambo ambayo hapo awali yaliaminika hayawezekani.
Watu ambao waliweza kugundua na kutengeneza ndege wakati dunia nzima kabla ya hapo iliamini ni jambo ambalo haliwezekani kifaa kupaa angani.
Walionzisha mitandao watu mpaka sasa hivi wanaweza kuwasiliana wakionana
katika mitandao kama _Skype_ _Facebook mmuda
Lnger_ n.k kutokea kwenye kila kona ya dunia wakati dunia nzima iliamini kwamba barua ndio nusu ya kuonana.
Wameweza kwa namna fulani kuitiisha dunia lakini bado. Tena bado sana.
Profesa William aliwahi kusema kwamba kulinganisha na Kile ambacho mwanadamu anapaswa kuwa nacho watu wameamka nusu
Kumbe kulinganisha na kile ambacho unapaswa kuwa umeifanyia dunia bado, tena bado sana. Yaani bado
haujaitiisha nchi na kuitawala
Bado hujazitumia raslimali zilizokuzunguka inavyotakiwa.
Acha kuishi kwa kutumia mawazo ya watu bali kuwa tayari kuzalisha mawazo yako kila kuchao.
Ulipo hapo unatumia mawazo ya watu mengi sana ( watu waliojaribu kuiitisha dunia).
Najua utaanza kujiuliza mawazo gani?
Ni mengi siwezi kutaja yote ila kwa kuanzia nitataja baadhi na wewe utamalizia kutaja mengine?
✔Naomba nikuukize hiyo simu unayotumia ni wazo lako au la mwingine?
✔ eti hizo nguo ulizovaa ni wazo lako au la mwingine?
✔ na nyumba ulimo hapo ni wazo lako au la mwingine?
✔hujaamini bado kwamba mpaka hapo unatumia mawazo ya watu na kwako halionekani. Upo unatumia mawazo ya watu walioitiisha dunia na wewe la kwako tunalitafuta hatulioni.
Amka ndugu yangu, wakati ndio huu.
Hata aliyetengeneza kiti hicho ulichokalia alianza kwa kujifunza na kusoma mambo yanayohamasisha kama haya na baadae akachukua hatua.
Kwa nini usiwe wewe?
Kwa nini usiwe wewe ambaye ameitiisha dunia.
Dunia imejaa watu kadhaa waliofanya Kazi kwa bidii ili waitiishe. Historia zao zimejaa tele kwenye vitabu. Ila watu hawa sio wengi sana kama ambavyo idadi ya ambao hawajaitiisha ni nyingi.
Na wewe unaweza kujiingiza kwenye upande wa watu ambao wameitiisha dunia.
Umaqeza kuamua kuungana na watu maarufu ambao hata wengine hawakuwahi kwenda shule.
Mtu kama Aristotle hakwenda shule lakini kwa mambo aliyoyafanya ataendelea kubaki kwenye vitabu vya historia kwa miaka mingi sana ijayo. Na wewe unaweza kufanya hivyo. Kama utachukua hatua sasa.
Najua hapo utauliza swali jingine
Nitaanzaje?
💧Unazo raslimali nyingi sana ambazo zimekuzunguka,
Kwa kuanzia kabisa ni AKILI yako.
Akili yako ndio raslimali nambari moja kati ya raslimali zote ambazo unazo. Na kadri ya tafiti zilizofanywa ni kwamba mpaka sasa mwanadamu anatumia chini ya asilimia kumi ya akili yake . Yaani namaanisha CHINI YA ASILIMIA KUMI YA AKILI YAKE.
Hivi kwa mambo ambayo unayafanya sasa kama ungeweza kuongeza nusu ya nyingine unadhani ungekuwa wapi?
Kama unatumia asilimia tano ya akili yako na ukaanza kutumia asilimia kumi unadhani utafika wapi?.
.
Kumbe hapo naanza kukubaliana na kauli ya profesa William kwamba kulinganisha na Kile ambacho mwanadamu anapaswa kupata watu wameamka nusu
Itumie akili yako tena itumie vizuri sana bila kuogopa.
Kadri utakavyoanza kuitumia ndivyo utakavyogundua ni kwa namna gani inazidi kukua. Fikria jinsi utakavyotatua matatizo ya watu. Fikria jinsi utakavyoitiusha nchi.
Yaani akili IPO ili itumike.
Narudia tena kwa msisitizo na kwa herufi kubwa AKILI IPO ILI ITUMIKE
Kama unataka kuitiisha nchi na hutaki kuitumia akili yako utasubiri sana.
Kama unataka kufanikiwa na hutaki kuitumia akili yako utasubiri sana.
Kama unataka kufaulu darasani na hutaki kuitumia akili yako utasubiri sana..
Kama unataka ufahamike dunia nzima na hutaki kuitumia akili yako utasuburi sana.
Changamka! Ni sheria ya asili kwamba kama kiungo kitatumika basi kiungo hicho tunategemea kikue na kukua zaidi.
Darwini alielezea vizuri jambo hili kwenye utafiti wake alioufanya.
Kumbe na akili yako kama utaitumia sasa itazidi kuimalika na kuweza kuwa ya kuzalisha mawazo zaidi.
Itakua zaidi na kuweza kuingiza vitu vingi zaidi na zaidi.
Najua baada ya kusoma hapa utasema kweli GODIUS RWEYONGEZA (songambele)
Anasema ukweli na hutaanza kuitumia akili yako. Sasa sijui utawezaje kuiitiisha dunia bila ya kuanza kuitumia akili yako sasa.
Wapo watu wanalipwa kwa sababu tu wametumia akili yao.
Hivi unamfahamu HARRY LORAYNE
mtu ambaye ameitumia akili yake na kuijengea kumbu kumbu ya ajabu sana. Mtu ambaye ukimpa gazeti ndani ya dakika tano na kumnyanganya anaweza kukwambia gazeti zima lina vichwa gani?.
Anaweza kukwambia kichwa fulani cha habari kipo ukurasa wa ngapi na mwendelezo wake uko ukurusa wa ngapi?.
Mtu ambaye ukimwambia namba yako ya simu basi umemaliza
Haitaji tena kuiandika kwenye simu yake.
Mtu ambaye anaweza kukumbuka majina na sura za zaidi ya watu elfu kumi wanaotambulishwa kwake mara ya kwanza na kwa mfululuzo.
Najua utaanza kujiuliza kwa nini nimemweleza jamaa huyu sana, ndio nimemuzungumzia sana kwa sababu ametumia akili kwa manufaa. Ameitiisha nchi.
Sasa wewe umefanya hivyo.
Kama hujafanya umesubiri nini?
Anza sasa..
Najua unamjua BILL GATES. Tena utakuwa jana au leo asubuhi umegoogle kuangalia historia yake.
Na siku ile mlikuwa mmekaa na jamaa zako mnabishana hivi kweli Bill Gates ni tajiri nambari moja au?
Sasa hapo sikuulizi maswali mengine.
Lakini ukweli ni kwamba usingemjua kama asingetumia akili yake vizuri.
Sasa na wewe kuanzia leo anza kujijengea msingi mzuri.
Mwaka mmoja au baada ya miezi kadhaa na wewe tuanze kukugoogle kuangalia historia yako kwa umakini huku tukihamasika. Yaani tuseme kwamba kweli huyu jamaa ametumia kweli akili yake.
Autuseme kama vijana wa siku hizi wasemavyo jamaa huyu ni jembe
Najua nimeeleza vya kutosha kuhusu suala zima la kuitumia akili yako na wewe utachukua hatua stahiki maana mwenye macho haambiwi tazama.
Lakini pia jua kwamba ukiona vitu vimeelea vimeundwa na vimeundwa na watu.
Na wewe anza kuunda. Itiishe nchi.
Katika suala zima la kuitumia akili naweka kalamu chini📝📝
💧 NGUVU
Yaani unayo nguvu tena nguvu ya kutosha sana. Sheria ya asili inasema kwamba kila kitu kipo tena kipo cha kutosha sana.
Katika suala zima la nguvu naenda kulizungumzia kwa namna mbili.
🔥aina ya kwanza ya nguvu ni ile ambayo wewe unayo na unaweza kuitumia kuiitiisha dunia kwa kufanya kazi, kulima, kuvua samaki. Nguvu ya kubeba mizigo.
Nguvu ya wewe kushiriki kwenye mashindano makubwa na kushinda. Nguvu ya kucheza mpira, n.k
Hii ni nguvu ambayo unayo na ni ya bure. Itumie tena itumie kweli.
Nguvu yako ndio inaweza kukufanya uitiishe nchi.
Angalia watu wa babiloni walitaka kujenga mnara ambao ungefika mbinguni. Moja ya kitu ambacho wangetumia ni nguvu. Walipaswa kufyatua matofali kwa kutmia nguvu, kusomba maji kwa kutumia nguvu, kusomba matofali kwa kutumia nguvu. Kwa nini sasa wewe hutaki kuitumia nguvu yako?
Hiyo nguvu yako usikubali ipotee tu. Maana nguvu huwa inapotea kwa kutoka katika mfumo mmoja kwenda mwingine.
Bali itumie na ikusaidie kuitiisha nchi.
🔥 aina ya pili ya nguvu ambayo unayo ni nguvu ile ambayo unatuma kwa watu na vitu vingine vinavyoishi.
Unapofikiri unatumia nguvu.
Unapopanga kufanya kitu unatumia nguvu. Japo yawezekana muda mwingine hauongei, au haufanyi kazi yoyote lakini bado nguvu inatumika.
Ukianza kumfikiria mtu au kitu nguvu inakuwa inatumwa katika mfumo wa mawimbi ambayo humfikia yule mtu na kukurudia wewe.
Ndio najua utashangaa sana juu ya hili lakini iko hivyo.
💫Hivi ishawahi kukutokea unamfikiria mtu Mara anatokea! Hivi hiyo unafikiria nini?
💫Au unawaza kumpigia mtu simu mara anapiga? Hivi unajua hiyo ni nini?
Naam hayo ni matokeo ya nguvu ambayo umetuma kwa mtu huyo na nguvu hiyo ia kurudia katika mfumo kama huo.
Kumbe nguvu yako itumie vziuri.
Sheria ya asili inasema kwamba mtu utavutia kwako Kile ambacho unafikria sana
Yaani utavutia kwako kile ambacho umeweka nguvu kubwa sana kwake.
Utavutia kile ambacho kipo katika akili yako.
Unavutia kwako kile ambacho unapenda. Sio ambacho hupendi.
Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA