Kosa Kubwa Kuwahi Kufanyika Duniani


Habari za leo rafiki yangu, imani yangu unaendelea vyema katika harakati zako za kuhakikisha unatoka moja mpaka kileleni.

Karibu sana katika makala ya leo ambapo tunaenda kujifunza kosa kubwa sana ambalo huwa linafanywa na watu wengi sana.
Ndio. Labda hata wewe umekuwa unafanya kosa hili bila kujua lakini sasa unaenda kulijua jambo hili na kuliepuka..
Huu ndio mwisho wako wewe kufanya hili kosa.
Kosa lenyewe ni kutojifunza kutoka kwa watu wengine.
kama unaona umekutana na mtu na hujajifunza kitu kutoka kwa mtu huyo basi jua kwamba unakosea sana. Hakikisha kwamba  kila unapokutana na mtu yeyote basi unajifunza kitu kipya kutoka kwake.

Kamwe, kamwe, kamwe usikubali muda wako utakapokutana na mtu yeyote upite bila kujifunza kitu kipya kutoka kwa huyo mtu. Usipojifunza kitu utakuwa umepoteza sana.
Hata kama utakutana na mtu kwa dakika moja tu basi hakikisha unajifunza kitu kipya kutoka kwa Huyo mtu..
Hata kama umekuwa unakutana naye Mara nyingi sana bado kuna kitu unaweza kujifunza kutoka kwake. Anza leo kujifunza kutoka kwa wale unaokutana nao. 
Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X