Maeneo Mawili (02) Ambayo Hayahitaji Bajeti


Katika maisha ya kila siku mambo yetu mambo mengi sana yanakwenda kwa bajeti. Ukipata mshahara au kipato chako kikiingia kitu cha kwanza unachokifanya ni kuweka bajeti.
Hii inakuhakikishia kwamba umeitumia vizuri kila senti inayoingia kwenye mfuko wako

Ukinunua chakula chako unakiwekea bajeti kwa kuhakikisha kwamba chakula Fulani kitatumika siku fulani na kingine siku nyingine. Unakuwa una uhakika kwamba chakula changu nitakitumia baadae kwa siku kadhaa.

Hivi ndivyo ambavyo mambo yamekuwa yakienda kila siku,

Kumbe bajeti ni kitu Kizuri sana ambacho tunakihitaji.

Lakini ushawahi kujiuliza wapi sipaswi kuweka bajeti?
Unaijua mipaka ambavyo bajeti haipaswi kuvuka?
Sehemu ambavyo kama utaiwekea bajeti basi utakuwa umejiwekea mipaka mikubwa sana ya kimaendeleo.Je ni wapi huki?

Usiweke mipaka kwenye vitu hivi

1. Kipaji.
Kipaji chako kipo ili kitumike. Kipaji chako kipo kwa ajili ya kuwasaidia watu wengine. Ni kwa kutumia kipaji chako unaweza kufahamika dunia nzima, unaweza kutatua shida za watu.

Unaweza kuhakikisha huweki mipaka hata kidogo kwenye kipaji chako. Kama una uwezo wa kuigiza fanya hivyo, kama unaweza kupika Fanya hivyo. Yaani wewe fanya bila kuogopa ili mradi hakikisha hauvunji sheria za nchi.

Kwa kuwa hakuna mtu wa kukuzuia na kukuwekea mipaka kwenye kipaji chako jitahidi sana kadri ya uwezo wako kukitumia kipaji chako.
Usijali wengine wanasemaje wala usianze kusema kwamba kwa kuwa watu fulani walishindwa basi siwezi, hapana sio hivyo pambana.

Kitumie kipaji chako kufanya mambo makubwa . usifanye kwa sababu umeona wengine wanafanya,  Fanya kwa bidii kubwa sana na kwa akili yako yote

2. AKILI
hili ni eneo jingine ambalo huitaji kuliwekea bajeti. Kama umeanza kufanya hivyo, basi kuanzia leo iondoe bajeti hiyo maana ni kikwazo kikubwa sana.
Akili yako itumie kubuni vitu vipya, itumie kufikria mbinu Mpya za kutatua matatizo,  itumie kuongeza MAUZO kwenye Biashara.

Ubora wa vitu hivi viwili ni kwamba hakuna hata kimoja ambacho unaweza kusema kwamba nimekitumia mpaka mwisho.
Kadri unavyotumia vitu hivi viwili vinazidi kutanuka na kujua zaidi.
Anza leo kuvitumia.

Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii


Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X