Katika ulimwengu wa sasa ambao unakua kwa kasi kubwa sana, mambo yanazidi kubadilika kwa kasi kubwa sana.
Tupo katika ulimwengu ambao mtu analipwa kwa thamani anayoitoa kwa watu sio kwa kiwango ambacho amefanya kazi.
Kama kwa sasa unalipwa laki tatu kwa mwezi, haulipwi laki tatu kwa sababu ya masaa uliyofanya kazi bali kwa thamani unayoitoa.
Vivyo hivyo anayelipwa milioni moja. Halipwi kwa sababu ya masaa aliyofanya bali kwa thamani aiyoitoa.
Ndio maana unaweza kukuta watu wawili wanafanya kazi ile ile muda huohuo lakini bado wanalipwa mshahara tofauti.
Sasa thamani inauzwa wapi?
Nani anagawa thamani?
Thamani ni kitu ambacho huwezi kupewa na mtu yeyoye wala kuinunua kokote bali unaweza kuiongeza kwa kufanya yafuatayo;
1. Kujitofautisha mwenyewe.
Jitofaurishe mwenyewe au kufa. Huu ni msemo ambao huwa unatuhitaji kufanya kitu cha tofauti katika kila jambo.
Msemo huu unazingatia mantiki ya kwamba biashara moja inaweza kuwa na watu wengi ambao wanaifanya lakini unaweza kuwa wewe ambaye unafanya cha tofauti
Wateja wakaja kwako hata kama kuna watu wengine wanafanya biashara hiyo.
Wateja wakaendelea kuja kwako hata kama kama utaongeza bei ya bidhaa yako Mara mbili, hii ni kutokana na kwamba wana uhakika na kitu chako ambacho unakifanya kina thamani.
Ongeza thamani thamnai yako kwa kufanya kitu cha tofauti.
Thomas Edison ni mtu ambaye alijiyofautisha mwwnyewe kwa namna hii na kuwa mvumbuzi mkubwa sana wa karne ya 20, akimpita mpinzani wake Nikola Tesla.
2. Nenda hatua ya ziada.
Jijengee nidhamu ya kwenda hatua ya ziada kwenye kazi zako ambazo unafanya. Yaani, kama mafanikio yangekuwa yanapimwa kwenye kipimo wakati wenzako wako kipimo cha kwanza wewe kuwa kiwango cha Tatu au cha nne.
Nenda hatua kubwa zaidi mbele. Nchi ya Ujerumani ni nchi ambayo ilikuwa mfano mzuri sana wakati kwenye karne ya 20. Inasemekana kabla ya vita kuu ya pili ya dunia Ujerumani ilikuwa na teknolojia ambayo ilikuwa miaka 15 mbele ya wengine. Na wewe unaweza kufanya hivi kaa kihakikisha unafanya cha tofauti nabkwenda mbele zaidi.
3. Jenga nidhamu.
Ukiahidi kufanya kitu kifanye, ukianza kufanya kitu kimalize.
Hiyo ni nidhamu muhimu ambayo unahitaji kuwa nayo kwenye kazi yako. Hakuna mafanikio makubwa yanayojengwa nje ya nidhamu na uadilifu.
4. Acha mazoea.
Mambo ynabadilika kila siku na wewe unahitaji kubadilika.
Kama untaka kufanya Biashara au tayari umeshaanza wafahamu wenzako wanafanya nini? Na wamepiga hatua gani? Kama wao wamepiga hatua sana basi wewe jipange. ili uweze kuibuka mshindi. Zingatia na hayo ambavyo tayari tumeyazumzia hapo juu na haya hapa yanayofuata
7. Weka nguvu zako sehemu muhimu
Kuna sehemu muhimu ambazo zinakuzalishia na kukuongezea thamani zaidi ya nyingine. Kuna mambo madogo ambayo unayafanya na yanachangia kwa kiasi kikubwa sana kwenye mafanikio yako. Yafahamu hayo, na yafanye kwa nguvu kubwa sana.
8. Kuwa na mpango mzuri.
Mpango wako usome kila siku asubuhi, na usiku kabla ya kulala.
Usipokuwa na mpango itakuwa rahisi kwako kuacha kufanya maana utajuwa hujui wapi unapaswa kuwa.
Mpango wako ufanyie kazi, asubuhi mchana na jioni.
9. Panua wigo.
Ongeza idadi ya watu wanaokufahamu kila siku. Wachangamkie watu unaokutana nao. Hakikisha umejifunza kitu unapokutana na mtu Mpya. Ukiona umekutana na mtu na hujajifunza kitu chochote basi jua kwamba umepoteza sana. Jifunze sana kutoka kwa watu.
Sharma anasema kwamba watu ambao wamefanikiwa ni wanyenyekevu maana huwa wanapenda kujifunza kuyoka kutoka kwa watu kuliko ambavyo unaweza kutegemea.
Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA