Endelea Kupiga Hatua


Habari za leo rafiki yangu na ngugu msomaji wa makala za songa mbele. karibuni sana katika makala ya siku ya leo ambapo tunaenda kujifunza kitu kipya ambacho hatujawahi kujifunza kwa namna yoyote ile. hata kama utakuwa umekiona mahali basi leo unaenda kujifunza kwa namna ya tofauti kabisa, hivyo naomba tuweze kusafiri kwa pamoja mpaka mwisho wa kipindi.

Kuna wakati umesikia watu wanasema kwamba ukifika kileleni au ukipata mafanikio basi huo ndio utakuwa umefika mwisho. na hapo utakuwa umeanza kufurahia maisha.

kwanza kabisa leo ningependa ujue kwamba kipimo cha mafanikio yako unakipima kila siku katika yale ambayo unayafanya. Hivyo usisubiri kwamba mpaka ufike kileleni ili uje uanze kufurahia maisha, hapana anza leo hii kufurahia maisha na anza kuishi maisha yako sasa.

Usisubiri watu waseme kwamba sasa umefika kileleni, unaweza kuanza kufurahia maisha. Kiufupi ni kwamba hakuna mtu yeyote yule ambaye anaweza kukupimia kipimo cha maanikio yako mwenyewe bali wewe mwenyewe unweza kufanya hivi. mafanikio yako hayapimwi na mtu yeyote yule bali wewe mwenyewe. kumbe amua leo kuanza kuishi maisha ambayo unapenda kuishi na hakikisha kwamba umeyaishi.

ukifanikiwa kufanya kile ambacho ulipaswa kuwa umefanya basi hakikisha kwamba unajipongeza kwa kile ambacho utakuwa umefanya, kama wakati wa kufanya utakutana na changamoto jifunze kutokana na hiyo changamoto, itumie hiyo changamoto kama daraja la kwako kuelekea kwenye mafanikio.

kamwe, kamwe, kamwe usikubali kusema kwamba leo hii nimeshindwa. bali jifunze kutokana na kile ambacho unakutana nacho kila wakati; kila saa. jifunze kutokana na kilke ambacho unafanya kili siku. 

anza sasa
badilika sasa
muda ni sasa 
toka hapo ulipo 
anza kuelekea kileleni

 
 

Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


One response to “Endelea Kupiga Hatua”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X