Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa makala za songa mbele blog, imani yangu umeianza siku yako kwa namna ya tofauti sana leo na unaenda kufanya kitu cha tofauti sana kadri ya falsafa ambazo umechagua kuishi.
Falsafa ni kitu ambacho watu wengi sana wanakiogopa kwenye maisha yao. Ila kwa namna yoyote ile jinsi unavyoendesha maisha yako leo hii ndivyo ambavyo tunaweza kugundua na kujua falsafa zako za maisha. Jinsi utakavyoishi maisha yako leo, inafaa tu kusema kwamba una falsafa fulani ya maisha.
Falsafa hii ya maisha ambayo tunaenda kujifunza, anza kuitumia leo kwa ajili ya manufaa yako.
Falsafa yenyewe inasema nilikuja duniani mtupu na nitarudi nilipotoka na nafsi yangu. Hii falsafa ambayo unaweza kuwa nayo maishani mwako.
Ukijua kwamba hukuja duniani na kitu chochote basi utakuwa na uhakika kwamba hakuna kitu ambacho kinaweza kukuzuia wewe kusonga mbele. Hata kama watu watakuwa wengi kiasi gani hawatakuwa tayari kukuzia.
Lakini pia ukijua kwamba utarudi ulipotoka na nafsi yako utahakikisha kwamba siku ya leo unafanya, kile ambacho unapaswa kufanya leo na utakifanya kwa wakati.
Hakikisha kwamba hauachi kitu bila kufanywa leo.
Anza kuishi falsafa hii leo.
Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
One response to “Falsafa Muhimu Ambayo Kila Mtu Anapaswa Kuiishi.”
Asante mkuu