.
Habari za asubuhi ya ya leo mpendwa msomaji wa makala kutoka katika blogu yako ya songa mbele. Imani yangu umeianza siku yako kwa namna ya tofauti sana huku ukiwa unaenda kufanya kitu kingine kikubwa sana. Kumbuka kwamba hapa duniani hutakuja kukutana siku nyingine ambayo itakuwa kama ya leo. Yaani kiufupi ni kwamba hakuna siku nyingine itajitokeza ambavyo itakuwa ni tarehe 27 may 2017 maishani mwako. Kumbe itumie vizuri leo, maana ni fursa nzuri ya wewe kuishi. Kama kuna kitu ambacho unapaswa kufanya leo kiandike chini na anza kuchukua hatua.
Katika makala yetu ya leo tunaenda kujifunza hatua tatu ambazo zitakutoa hapo ulipo na kuhakikisha kwamba zimekufikisha kileleni.
Kuna watu wamekuwa wakilalamika kwamba maisha haya hayana huruma, yaani kuna watu wanazaliwa wanakuta kila kitu kipo na wengine wanazaliwa hawakuti kitu cbochote.
Ni ukweli usiopingika kwamba kuna baadhi ya watu wanazaliwa na kukuta kwao Mali, pesa, na vitu vingine vikiwepo wakati wengine hawakuti kitu. Lakini ukweli huo haumaanishi kwamba tuseme dunia haina huruma.
Hatuwezi kusema kwamba dunia haina huruma kwa sababu wakati huo huo watu walipozaliwa kwenye familia zenye utajiri, wewe ulizaliwa na utajiri ndani yako. Sasa hapa zipo hatua tatu za ambazo zitakuhakikishia unautumia utajiri wako kuweza kufika kileleni.
1. JENGA PICHA YA KILELE CHA MLIMA AMBACHO UNATAKA KUFIKIA.
Hapa anza kuandika vile vitu ambavyo unataka kufikia, jiulize Je nisipovifanya nitakosa nini? Je, nikivifanya na kufanikiwa kutakuwa na manufaa gani kwangu? Je nitaanza kwa kufanya nini ili niweze kufika kule ambapo nataka kufika? Haya ni maswali ya muhimu sana ambayo unahitaji kujiuliza.
Andika chini ni kitu gani ambacho unahitaji kufikia baada ya miaka mitano. Kumbuka kupata kunatanguliwa na kupanga.
Andika vitu ambavyo wewe binafsi unasimamia na visimamie.
Kumbuka kwamba kupanga kunatangulia mafanikio kama ambavyo kujielewa kunatangulia mabadiliko.
2. ANZA KUPANDA.
Anza kuchukua hatua ndogo leo hii ambazo zitakufanya wewe uweze kupanda na kutoka hapo ulipo kwenda kileleni. Kuna nguvu kubwa sana katika kuanza. Hatua ndogo ambayo unaichukua leo hii inaweza kuleta matokeo makubwa sana hapo mbeleni.
Ukianza kufanya kitu kidogo utajikuta nguvu ta kuendelea kufanya zaidi. Unaenda kufanya nini leo hii ambacho kitafanya mabadiliko makubwa baadae.
3.CHUKUA HATUA NDOGO.
Huwezi kufika kileleni mwa mlima Kilimanjaro kwa kuruka kutoka chini mpaka kileleni. Lakini unaweza kufika kileleni kwa kuchukua hata ndogo ndogo.
Kwa kulifahamu hilo, lakini pia kwa kuufahamu ukweli kwamba siku hutengeneza wiki, na wiki hutengeneza mwezi hatimaye miezi hutengeneza mwaka, basi utachukua hatua ndogo ndogi leo. Haikisha kwamba mpaka unakuja kufikia hatua ya uzee wako, hatua ndogo unazochujua leo zinaanza kukulipa.
Tukutane kileleni