Hili Ndilo Jambo La Muhimu Sana Ambalo Kila Mtu Anapaswa Kulizingatia


.

Habari za asubuhi ya leo rafiki yangu na ndugu msomaji wa makala za songa mbele, imani yangu umeianza siku yako vyema kabisa na unaenda kufanya kitu ambacho ni bora kabisa. Kuthubutu ni jambo moja la msingi sana ambalo unalihitaji ili kuweza kufikia hatua kubwa sana. Kumbe kitu cha kwanza kabisa leo hakikisha kwamba unathubutu kufanya kitu. Kudhubutu ni jambo muhimu sana ambalo litakufanya uchukue hatua.

Tukirudi katika makala yetu leo, tunaenda kujifunza jambo hili ambalo ni jipya. Likipatikana jambo hili dunia yetu itakuwa sehemu nzuri sana ya kuishi na kila mtu atafurahia maisha.
Kumbe hata leo utakapodhubutu hakikisha kwamba unadhubutu kwa kufanya hili jambo.

Jambo lenyewe ni kuifanya dunia kuwa sehemu bora sana ya kuishi. Ndio. Kila kitu unachofanya leo hakikisha kwamba unafanya kwa nguvu yako kuhakikisha kwamba dunia imekuwa sehemu safi sana ya kuishi.

Ukiwa na tabia ya uchoyo hili jambo huwezi kulifikiria. Utaona ni kama kukupotezea muda wako. Lakini ukweli ni kwamba wewe leo hii upo hapo ulipo kwa sababu tu baadhi ya watu watu waliweza kufanya kazi na kuhakikisha kwamba wanaifabya dunia kuwa sehemu bora sana ya kuishi. Kama mtu aliyetengeneza simu angekuwa mchoyo basi ina maana kwamba wewe leo hii usingekuwa na uwezo wa kuusoma ujumbe huu. Lakini kwa kuwa alikuwa na malengo la kuifanya dunia hii kuwa sehemu bora sana ya kuishi basi ndio maana wewe leo hii unafurahia matokeo bora ya mtu Huyu aliyetengeneza simu na kuifanya dunia kuwa sehemu bora sana ya kuishi.

Kazi ya kufanya leo chagua kitu kimoja ambacho utakifanya na kitakutoa hapo ulipo kwenda sehemu nyingine lakini pia kitakuwa sehemu ya  kuifanya dunia mahali bora sana pa kuishi.

Dunia ikiwa bora na watu wanaoishi watafurahia maisha hapa duniani. Kumbuka huduma zote za kijamii zunahitaji kuboreshwa, na mtu wa kuziboresha ni wewe. Kumbuka kwamba usafiri unahitaji kuboreshwa zaidi, watu wanahitaji kupata chakula safi na bora.  Uamuzi ni wako chukua hatua sasa hili uweze kufika unapotaka.
Tukutane kileleni.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X