Hili Ni Jambo Moja Ambalo Unahitaji Kulitunza Sana


Habari za leo rafiki yangu na ndugu msomaji wa makala za songambele. Imani yangu unaendelea vyema katika kuhakikisha kwamba unapiga hatua na kutoka hapo ulipo kwenda kileleni.

Siku ya leo leo tunaenda kujifunza jambo moja ambalo unahitaji kulitunza sana, na kuhakikisha kwamba liko salama kila siku hasa katika safari yako hii ya kuhakikisha kwamba unatoka hapo ulipo kwenda kileleni.

Moja kati ya vitu ambavyo watu wanaogopa sana ni kushindwa katika safari ya mafanikio yao.

Lakini kitu kimoja ambacho ninakijua kwa uhakika ni kwamba huwezi kufikia mafanikio makubwa sana bila ya kushindwa. Huwezi kupiga hatua kubwa sana bila ya wewe kukutana na changamoto kubwa sana katika safari yako. Kushindwa sio tatizo Bali kushindwa ni sehemu ya mfanikio.

Sasa hapa ndipo tunakuja kuangalia ni jambo moja ambalo unahitaji kulitunza.

Yaani kiasi kwamba kama utashindwa maeneo mengine  haupaswi kushindwa katika hili. Ukishindwa katika eneo hili basi utakuwa umepoteza sana na hapo ndipo tutakaposema kwa msisitizo wa hali ya juu sana kwamba UMESHINDWA.  Tofauti na hapo utakuwa hujashindwa bali utakuwa unajifunza kutokana na makosa.

Soma zaidi ubongo ni bustani

Eneo lenyewe ambalo hupaswi kushindwa ni kwenye AKILI yako.
Hakikisha kwamba muda wote akili yako unailisha kile kilicho bora hakikisha kwamba akili yako ina Maarifa ya kutosha. Unaweza kufanya kitu kwa nje kikaonekana kimeshindwa lakini kama akili haijashindwa basi wewe bado una nguvu kubwa sana ya kuendelea. Kama ulikuwa bado haujawekeza kwenye akili yako anza leo hii kwa kuwekeza huku maana hili ndio eneo muhimu sana kwenye maisha yako la kuhakikisha kwamba linakutoa sifuri mapaka kileleni

Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii


Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X