Kitu Kimoja Ambacho Unapaswa Kukitafuta Kila Siku


Mithali 3, 13/14

Heri mtu yule aonaye hekima. Na mtu yule apataye ufahamu,

Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi.

Katika mistari hii nimeilinganisha na umuhimu wa mtu kusoma vitabu. Maana amaenndika hivi

Na mtu yule apataye ufahamu.

Kumbe kupata ufahamu ni kitu cha muhimu sana. Na faida yake ni kubwa sana kuliko hata dhahabu safi. Ukiipata dhahabu bila kuwa na ufahamu unaweza kuipoteza na kurudia katika hali yako ya kawaida. Lakini kama una ufahamu hata bila ya kuwa na dhahabu bado unaweza kuitafuta dhahabu na kuipata. Kumbe maarifa ni kitu cha muhimu sana kwenye maisha yako. Kuna watu ambao wamesemekana kwamba wameweza kupata pesa katika mambo ya bahati na sibu na kuwa mamilionea ndani ya siku moja lakini hatimaye kiasi hicho cha pesa wamekipotezakwa sababu ya kukosa ufahamu wa jinsi ya kuitumia hiyo pesa. Kumbe ni muhimu sana ukayatafuta maarifa sahihi kila siku juu kile ambacho unakifanya. Usikubali kufanya kitu ambacho hauna uhakika nacho. Usikubali kufanya kitu ambacho hujatafuta maarifa ya kutosha juu ya kile kitu ambacho unataka kufanya. Usikubali watu wakukimbize katika kufanya kitu ambacho una uhakika kwamba hauna ufahamu wa kutosha.

Moja kati ya vitu ambaavyo nimekuja kugundua hivi karibuni ni kwamba watu wenye maarifa sahihi ndio ambao wanazidi kutafuta maarifa na kuongeza ufahamu kila siku na ambao hawana maarifa wanazidi kuyakwepa maaarifa hayo na hawataki kabisa kusikia juu ya habari ya kusema kwamba wanatafuta maarifa. Ukitafuta maarifa yatafuata mkondo na kukujia na usipoyatafuta basi na maarifa yenyewe yatakukwepa.

Dahabu ipo popote pale ambapo upo. Na imesubiri kidogo tu uchukue jembe na kuanza kuichimba ili iweze kutoka. Ukigusa tu kidogo dhahabu hiyo inakuja haichelewi kuja.

Chimba dahahabu kwa kuhakikisha unatafuta maarifa sahihi. Tauta maaria sahihi maana ni chanzo  kizuri cha wewe kutoka sifuri mpaka kilelleni. Maarifa mazuri yatakubeba.

1.      Tafuta dahabu kwa kusoma vitabu vya kuhamasisha na kuelimisha kila siku asubuhi na jioni

2.      Tafuta maarifa kwa kusoma makala zinazoelimisha kila siku.

3.      Tatufa maarifa kwa kukaa na watu sahihi katika kile ambacho unafanya kila siku.

4.      Tafuta maarifa sahihi kwa kusikiliza vitabu vilivyosomwa kila siku.


2 responses to “Kitu Kimoja Ambacho Unapaswa Kukitafuta Kila Siku”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X