Kosa Ambalo Watu Wengi Hufanya


Habari za leo Rafiki yangu, karibu sana katika makala yetu ya leo ambapo tunaenda kujifunza kitu kipya, kitu ambacho ni cha tofauti sana.

Moja kati ya vitu ambavyo huwa nasisitiza kila siku kwa kuwaambia watu wengi sana ni kwamba wewe ni kiongozi. Huu ni ukweli ambao huwa napenda kuuongea kila siku. Wapo watu ambao huwa wanaupokea kwa namna ambayo ni chanya, na wapo ambao huwa wanaupokea kwa namna ambayo ni ya hasi. Msimamo Wangu ni uleule, wewe ni kiongozi. Naongea hivi kwa bila kujali wewe utajisikiaje. Naongea hivi bila kwa sababu huwa siogopi kusema ukweli na nitaendelea kusimamia ukweli kqa ujasiri.

Kitu gani kinanisukuma mimi kusema kwamba wewe ni kiongozi.

1. Kwa sababu wewe una ratiba ambazo unajipangia na kuzitimiza.
2. Kwa sababu wewe kuna watu ambao wanapenda kuishi maisha kama ya kwako. Kuna watu ambao wanakufuatilia wewe na kuiga mifano yako.

Kumbe unapaswa kuishi kama kiongozi, unapaswa kuishi kama meneja tayari na kuna watu wengi chini yako ambao wamesubiri mwongozo wako. Usisubiri uingie ikulu ndipo uanze kuishi maisha ambavyo unayataka. Kumbuka kwamba muda wako wa kuishi ni leo..

Moja kati ya kosa kubwa sana ambalo watu huwa wanafanya ni kutaka kuongoza watu wengine, wakati wao hawawezi hata hawawezi kujiongoza. Hili ni kosa moja ambalo wewe unahitaji kuliepuka kila siku. Kosa hili sio jema sana kwako kulifanya.

Kumbe moja kati jambo moja la muhimu ambalo unahitaji kulizingatia ni
 Kujiongoza mwenyewe kabla ya kutaka kuwaongoza wengine. Ndio huu ni ukweli ambao hauepukiki. Huwezi kuwalazimisha watu kwenda sehemu, wakati wewe unaogopa kwenda huko.

Hatua ya kuchukua leo.
1. Anza kufuata ratiba zako.
2. Weka malengo yako na uyatimize.
3. Ahidi kile ambacho una uhakika utatimiza.
4. Tenda zaidi ya kuongea.

Kumbuka kwamba wewe ni kiongozi. Kumbuka wewe ni kioo cha jamii. Jamii inapojiangalia kwako lazima Kuna kitu fulani Kizuri tunategema kiakisiwe kutoka kwako.
Anza sasa


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X