Maamuzi Matatu Ambayo Unapaswa Kuyafanya Leo


Habar za leo Rafiki yangu na ndugu msomaji wa blogu yako ya songa mbele, imani yangu umeuanza siku yako vyema kabusa huku ukiwa unaenda kufanya mambo makubwa sana siku ya leo. Leo  hii tunaenda kujifunza kitu chenye umuhimu mkubwa sana kwetu, kitu ambacho kitatubadilisha kwa kututoa hapa tulipo na kutupeleka kileleni. Ndio haya ni maamuzi muhimu sana ambayo unahitaji kuyafanya leo. Amua sasa kufanya maamuzi hata muhimu ili siku moja tuweze kufika kileleni.

i) Uamuzi wa kitu ambacho unapaswa kufanya..
Kumbuka kwamba kila mtu hapa duniani anapaswa kuacha alama kwa  kufanya kitu ambacho kitadumu milele.
Unahitaji kufanya kwa namna ya tofauti. Kumbe uamuzi wa kitu ambacho unapaswa kufanya ni muhinu sana. Kumbuka kwamba haujazaliwa hapa duniani kwa ajili ya kuanza kujiandaa kuishi bali umezaliwa ili kuishi. Anza kuishi leo kwa kufanya kitu muhimu sana kwa kuanza kuutumia uwezo mkubwa sana ambao umo ndani yako.

ii) Uamuzi wa kuvipa vitu maana.
Falsafa yangu inasema kwamba hakuna kitu chochote kile ambacho kina maana isipokuwa tu kama wewe utakipa maana. Ni uamuzi wako ambao unaweza kuufanya leo kwa kuanza kuvipa vitu maana tofauti, tofauti. Unaweza kuvipa vitu maana ambayo inakuinua binafsi au unaweza kuvipa vitu maana ambayo itakuangusha.

iii) Maamuzi ya kitu cha kufanya leo.
Lengo lako kuu ndilo ambalo litaamua kitu gani ambacho unapaswa kufanya. Kitu unachofanya leo ndicho kitakachokufanya ulivyo miaka mitano au kumi ijayo. Amua kufanya kitu muhimu sana kwa siku ya leo ambacho kitakutoa hapo ulipo kwenda kileleni.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X