Maisha ya mafanikio ni kama kupanda ngaziMaisha ya kuelekea mafanikio ni kama kupanda ngazi. Kama unapaswa kupanda ngazi kutoka chini kwenda ghorofa ya juu kabisa, basi hakuna jinsi utapaswa kuzipanda ngazi moja baada ya nyingine.
Ukitaka kuruka ngazi hizi unaweza kujikuta ukiumia mwenyewe au huwezi kabisa kufika unapotaka.
Chukulia mwanafuzi ambaye amekwepa mahesabu ya awali kabisa ambayo yanahusisha kujumulisha, kutoa, na kuzidisha lakini mwanafunzi huyo huyo akakimbilia mahesabu ya maumbo bila shaka mwanafuzi huyo atapata shida sana katika kufanya hesabu hizo za maumbo kwa sababu tu hajajenga msingi mzuri sana tangu mwanzoni.
Au kijana ambaye amekutana na msichana maara ya kwanza na akataka kumbusu palepale alipotambulishwa kwake bila shaka atampoteza palepale
Vivyo hivyo wakati unapanda ngazi ya kutoka sifuri na kwenda kileleni hauna budi kupanda ngazi moja baasa ya nyingine. Hapa ambacho kinaweza kuku tofautisha wewe na watu wengine ni uharaka wako wa kupanda ngazi, wapo watu ambao wana uwezo wa kupanda ngazi haraka wakati wengine wanapanda taratibu. Lakini ngazi zipo pale pale.
Kumbuka kwamba ghorofa nyingine zina elevator ya kukupeleka kileleni. Lakini ubovu wa hizi elevator ni kwamba huwa haiendi hatua kwa hatua kuhakikisha zinakufikisha unapotaka, tunaweza kusema kwamba elevator zinaruka ngazi hivyo hazifai,
Mimi ninachohitaji ni kwamba uchukue hatua moja baada ya nyingine  katika kuhakikisha unafikia unapotaka. Na hizo hatua zipo sita amabazo unahitajo kuchukua wakati unapanda ngazi zako. Hatua zenyewe ni ngazi tosha kuhakikisha zinakufikisah kileleni.  Ukizifahamu hatua hizi na kuzifuata basi utakuwa unaelekea kwenye maisha yaliyo bora na maisha ambayo siku zote umekuwa ukiyataka.
Hatua zenyewe ni hizi hapa.
1.     Kuwa na picha ya afya njema. Kumbuka kwamba mwanadamu huwa anakuwa kile ambacho huwa anakifikria. Katika maisha yako ondoa kabisa picha ya magojwa,  mwenywe kwamba magojwa sio sehemu ya maisha yako. Jisemee mwenyewe kwamba  mimi ni mtu mwenye afya njema sana.  Kumbuka kwamba huwezi kufanikiwa huku ukiwa katika kitanda umelala wala sijawahi kumsikia mtu akiwa amefanikiwa akiwa amelala kwenye kitanda hivyo huna budi kuhakikisha kwamba afya yako unaitunza. Huwezi kusema kwamba unawajali watu wengine na kuwaapenda wakati wewe mwenyewe hujipendi.
2.     Kubali kwamba kuna umuhimu mkubwa sana wa wewe kushirikiana na  watu wengine ili uweze kutoka sifuri mpaka kileleni. Utambue mchango wa watu wengine na kuwa tayari kuutafuta kwa ajili ya manufa yako. Huwezi kutoka chini mpaka kileleni peke yako. Muda mwingine wakati unapanda ngazi zako utahitaji msaada wa watu wengine angalia hao watu ni akina nani na watafute katika kuhakikisha unafikia kileleni.
3.     Unahitaji msingi mzuri wa kuhakikisha kwamba umefika pale ambapo unataka kufika. Kama ambavyo mjenzi wa nyumba huwa anahitaji kuwa na mpango wa nyumba yake kabla ya kuijenga, anahitaji pia kujua kwamba atatumia kiasi gani katika kuijenga hiyo nyumba yake. Atahitaji vifaa gani na vitapatikana wapi na nani atamuuzia vifaa hivyo. Kumbe  na wewe unahitaji kuvijua vifaa hivi ni vipi kwenye maisha yako. Weka mpango wako ambao utakuongoza kwenye hatua kwenye mafanikio.
4.     Kuwa na mtazamo chanya na kuwa tayari kufanya kazi bila kushurutishwa na mtu yeyote. Jua kwamba maisha haya ni wajibu wako na hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kukuamulia wewe kwamba sasa unapaswa kupata kitu fulani, kumbe fanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi ambayo yatakutoa sifuri kwenda kileleni na kuhakikisha yamekupandisha ngazi za mafanikio.
5.     Kuwa tayari kulipa gharama na furahia sana kulipa gharama ya mafanikio. Gharama ya unayolipa kupata mafanikio ni ndogo sana ukilinganisha na  unachopata baada ya kufanikiwa. Lakini gharama ya kurudi nyuma, kuyakataa mafanikio ni kubwa sana, kama unahisi nakudanganya jaribu sasa utanipa majibu.
6.     Mwisho kabisa kuwa na msukumo wa ndani. Nguvu ambayo inakusukuma wewe katika kufanya kazi na kuhakikisha inakupaisha. Nguvu ambayo inakusukuma kufanya bila kujali watu wengune wanasemaje.
Kwa bahati njema sana hizi ni vitu ambavyo tayari ushaanza kuwa navyo , kama bado hujawa na tabia hizi basi anzisha tabia hizi ndani yako na hakikisha unazikuza ili kuweza kufikia kileleni
Kumbuka kwamba gharama ya kufika kileleni ni ndogo sana  kulingaisha na gharma ya kushindwa.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X