Habari za leo rafiki yangu na msomaji wa blogu yako ya songa mbele karibu sana katika makala ya leo ambapo tunaenda kuzungumzia somo ambalo watu wengi sana huwa hawapendi kuliongelea, watu wengi huwa wanaogopa kulitaja lakini wanatumia muda mwingi sana kufikiri juu yake. Leo tunaenda kuzungunuzia kuhusu pesa.
Robert Kiyosaki anakwambia kwamba huwezi kusema kwamba wewe hupendi pesa wakati unapoteza muda mwingi kazi ni kuzitafuta, huwezi kusema kwamba hupendi pesa wakati unapoteza muda mwingi sana shuleni ukisoma ili uje uajiriwe. Kumbe pesa sio kitu ambacho tunaweza kusema kwamba tutakiepuka kukiongelea kwa namna moja au nyingine, bali ni kitu ambacho lazima tukiongelee. Mimi binafsi nimemua kuandikia juu ya somo hili ambalo watu wengi hawapendi kulizungumzia na nitaendelea kulizungumzia kila siku mpaka siku ambapo nitaingia kaburini. Maana kazi yangu kubwa sana hapa duniani kuhakikisha kwamba watu wanaishi maisha bora. Hatuwezi kusema kwamba tuna maisha mazuri wakati bado tunahangaika kupata pesa. Wakati hatuna uhakika wa kuishi siku hiyo, kumbe hapo somo la pesa lazima tu liongelewe.
Hata ukiangalia mlolongo wa siku yako, tangu unpoamuka asubuhi mpaka jioni vitu ambavyo unatumia ni pesa tu. Ukiamka kitandani, kitanda chenyewe kimenunuliwa kwa pesa. Ukivaa nguo ni pesa, ukivaa kiatu ni pesa, mswaki ni pesa, ukitumia simu ni pesa. Yaani kiufupi ni kwamba kila hatua ambayo unapiga kila wakati pesa inahusika.
Kumbe hapo Nina kila haki kuliongelea suala hili zima la pesa kwa ujasiri wa hali ya juu sana. Kama watu wote wataacha kuongelea kuhusu pesa. Basi mimi nitakuwa wa mwisho.
Sasa turudi kwenye makala yetu ya leo ambapo tunaenda kujifunza mambo manne muhimu sana kuhusu pesa. Haya hapa, jifunze, uchukue hatua ili uweze kufikia hatua kubwa sana.
1. USIRUHUSU WATU KUCHUKUA TAARIFA ZAKO ZA SIRI.
Kuna taarifa ambazo unahitaji kuwa nazo kubusu akaunti zako za benki, kuhusu akaunti zako za Mpesa, Tigopesa, Airtel money. Usiruhusu kila mtu kuziona taarifa hizi maana ni taarifa zako binafsi. Namba zako za siri ziache zibaki siri kwa ajili yako.
Hata kama utakuwa na haraka kiasi gani, usikubali, kumpa namba za akaunti yako ili atoe pesa mwenyewe. Tunza namba hizi kwa ajili yako.
2. USINUNUE KILA KITU KINACHOKUJA MBELE YAKO.
Katika kutembea kutoka hatua moja kwenda nyingine utakutana na vitu vingi sana vizuri sana. Kabla hujanunua kitu chochote jiulize Je hiki kina umuhimu gani kwangu? Je, nisipokinunua nitakosa nini?
Baada ya hapo hairisha kufanya ununuzi wa kitu hicho kwa wiki nzima. Baada ya wiki jiulize je, bado nakihitaji kitu hicho? Utagundua kwamba Kile kitu ulikuwa hukihitaji.
Hairisha maamuzi ya haraka yanayoihusu pesa. Mtu kwako anataka kukuuzia kitu haraka, mwambie asante sana. Kama atalazimisha mwambie awatafute watu wengine. Kama ataendelea kulazimisha mwambie utamtafuta mwenyewe siku nyingine.
3. USINUNUE KWA DALALI.
Mara nyingi sana madalali huwa wanapenda sana kuongeza kiasi kikubwa sana cha pesa katika kile ambacho wanataka kukuuzia. Pigana kwa ajili ya pesa yako. David Batch aliwahi kusema kwamba Ukipoteza elfu kumi leo itakuchukua tena miaka kumi kuirudisha, kumbe jitahidi sana kuepukana na watu ambao wanalenga kukuongezea bei ya bidhaa ambavyo unataka kununua. Nenda moja kwa moja kwa wauzaji wa kutu Kile. Kama ni kampuni linauza hakikisha kwamba unaenda pale ambapo wanauza kile kitu. Kama uko mbali na kampuni husika hakikisha unajua mawakala wao wako wapi, ambao wanasambaza bidhaa zao. Nunua kwao. Epukana na watu ambao hawaeleweki katika kuja kukuuzia kitu unachotaka kwa bei ya juu sana.
4. TAFUTA TAARIFA SAHIHI.
Kabla ya kufanya ununuzi wowote ule hakikisha kwamba una taarifa sahihi juu ya Kile ambacho unataka kununua. Usikurupuke na kufanya ununuzi ambao sio rasmi bila ya kuwa na taarifa sahihi. Kwa kuwa pesa imo mikononi mwako, hakikisha kwamba huitoi mpaka pale utakapokuwa umekuwa na uhakika juu ya kile ambacho unaenda kununua. Ngoja nikupe taarifa sahihi ni kwa jinsi gani kutokuwa na taarifa sahihi kunaweza kukufanya upoteze pesa zako. Unapoenda kwa dalali na unataka nyumba ya kupangisha, atakwambia kwamba umlipe ili akupeleke kwa yule mwenye nyumba, baada ya kuhakikisha amekufukisha kule utalipa gharama ambayo inahusisha gharama yake ambaye amekuleta hapo. Tafuta taarifa sahihi.
Kabla ya kununua kitu tafuta taarifa za kutosha kuhusu kitu hicho, angalia kitu cha aina hiyo ambacho kipo sokoni na jaribu pia kufuatilia habari zake. Usinunue kitu bila kukijua nje ndani.
Jua hata ukitaka kukifanyia ukarabati utaenda wapi, vifaa vya ukarabati vipo au havipo, jua gharama za kusafirisha mpka nyumbani kwako ni za kwako au za yule anayekuuzia. Taarifa sahihi zitakupeleka sehemu sahihi. Ukiwa na taarifa sahihi hutapotea.
Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA