Mambo Ya Kuzingatia Ili Kutengeneza Mwelekeo Bora Wa Maisha Yako.


Zitoe ndoto zako ambazo umeficha na uzilete katika uwazi ili tuweze kuziona. Ndoto lazima tuwe tayari kuzifanyia kazi.

Kuna mtu mmoja ambaye alikuwa anadaiwa na Rafiki yake. Rafiki yake alimuuluza, utanilipa lini deni langu?
Yule MTU alisema. Nitakulipa nitakapouza kitabu changu.
Rafiki yake akamjibu aya poa haina shida.
Yule mtu akaendelea! Kitabu chenyewe sijakiandika, nikikiandika, nikakichapisha nikauza nitakulipa pesa yako.
Lakini pia hii inategemea kama nitapata wazo la kuandikia Kitabu. Mawazo yanahitaji kufanyiwa kazi.

Mara nyingi wewe unakuwa jinsi unavyofikiri mara nyingi sana.

Huwezi kupata kitu cha tofauti na Kile ambacho umekifanya au ambacho unafikiri.

Kumbe unahitaji kuwa na malengo ili uweze kufikia kule ambapo unapaswa  kufikia.
Hapa kuna mambo ya muhimu sana kukutoa hapo ulipo na  kukufikisha sehemu unapotaka.

1. Amua haswa Kile ambacho unataka kufikia, haswa katika maeneo ya kipesa, kiafya na kimahusiano. Watu wengi huwa hawafanyi hivi.

2. Andika malengo yako kwa umakini. Na yaelekeze haswa katika Kile ambacho unataka kufanya au kupata. Kuna kitu kinatokea pale unapoweka wazi malengo yako.

3. Weka mwisho katika kuufikia malengo yako.

4. Andika ambavyo utayafanya ili kuweza kufikia malengo yako. Kila Ukipata wazo jipya liandike, mpaka pale utakapokuwa umepata kile ambacho unahitaji.

5. Weka mpango kazi. Andika ni kitu gani unapaswa kufanya kwanza na kitu gani kitafuata baadae.

6. Chukua hatua kwenye mpango wako sasa! Ni ajabu sana watu huwa hawafikii Kile wanapotaka kufika kwa sababu tu hawana mpango.

7. Anza kuanya kitu hata kidogo walau kila siku. Fanya kitu ambacho kitakufanya uzidi kusonga mbele kuelekea kwenye lengo lako kila siku.

Kazi ta kufanya leo.
Andika chini malengo yako ambayo unapaswa kuwa nayo kwenye maisha yako. Andika chini vitu ambavyo unataka kuvimiliki.
Achana na watu ambao wanasema kwamba haiwezekani. Achana na wale ambao hawana malengo, ambao ndio wanaunda asilimia 97%. Ungana na asilimia 3% ya watu wenye malengo.

Anza safari yako ya kutoka sifuri mpaka kileleni leo


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X