Maswali Mawili Ya Kujiuliza Kabla Ya Kuacha Kufanya Unachofanya


.

Habari za leo rafiki yangu na ndugu msomaji wa makala za songambele, imani yangu kwamba siku mpya ya leo umeianza vyema sana ukiwa na nguvu na unakwenda kufanya mambo makubwa sana siku ya leo.

Mara nyingi unaweza kuwa unafanya kitu ukagundua kama vile unataka kuacha kufabya Kile ambacho unafanya. Unaweza kuona kama vile kinakuchosha, au kama vile kinachelewesha mafanikio. Ukishafikia hatua kama hii kinachofuata ni kuacha kabisa.

Sasa leo naomba nikupe maswali mawili ambayo unahitaji kujiuliza kabla ya kuacha. Lengo langu sio kukukataza kuacha bali nataka ujihoji maswali hata kabla ya kuchukua hatua. Inawezekana ukawa unachukua hatua ambazo sio sahihi. Waswahili wanasema kwamba fikiri kabla ya kunena. Unahutaji kufikiri kabla ya kuamua. Hata maswali yatakusaidia kufanya hivyo.

1. SWALI LA KWANZA
Je hili tatizo litadumu kwa mwaka mmoja kuanzia leo?
Kama tatizo halitakuja kudumu kwa zaidi ya mwaka mmoja kutoka sasa basi hakikisha kwamba huachi kufanya kitu hicho. Endelea kupambana zaidi utabadilisha kila kitu. Maisha yako umeyabeba mkononi mwako.

2. SWALI LA PILI.
Je, kuna mtu amekufa kwa sababu ya kufanya hili?

Hili pia ni swali la muhimu sana ambalo unahitaji kujiukiza pale unapokuwa unataka kuacha. Kama hakuna mtu ambaye amewahi kufa kwa kufanya Kile ambacho unafanya basi hapo usitoke. Endelea mbele maana hicho kitu kitakutoa na kukufikisha kileleni.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X