Sababu Nane Za Kwa Nini Unahitaji Kuwa Na Malengo


Habari za leo Rafiki na ndugu msomaji wa blogu yako ya SONGA MBELE. Karibu sana katika makala ya leo tunapoenda kujifunza kitu kipya ambacho hatujawahi kujifunza.

Kwanza kabisa tutambue umuhimu wa leo. Leo ni siku muhimu sana kwenye maisha yako. Ni siku ambayo jana ulisema kwamba kesho nitafanya. Na hatimaye imefika. Hivyo ni wajibu wako sasa kuchukua hatua na kuitumia leo. Kikubwa zaidi juu ya leo ni kwamba hii ni siku ambayo haijawahi hata siku moja kutokea, wala haitakuja kutokea. Hautakuja kukutana na siku yenye tarehe ya 20/05/2017 maisha yako yote. Hivyo amua kufanya mambo ambayo unapaswa kufanya leo. Yafanye bila uoga. Maana muda wako ndio sasa.

Sasa turudi kwenye makala yetu ya leo ambapo tunaenda kuona ni kwa nini hatuhutaji kupiga kila mahali.

Mtu akienda msituni kuwinda swala, lazima ajue anakwenda kuwinda aina gani ya mnayama. Kama ni swala basi mnyama huyo atakuwa ni swala, hakuna mnyama mwingine. Akifika msituni na kuanza kupiga tu kila sehemu atajikuta kaua hata wanyama wasiohusika, anaweza kuua hata sungura, chui, simba na tembo anaweza kuua hata miti, hii ni kwa sababu hakuamua kabisa kujikita katika kuwinda  mnayama ambaye alimpeleka msituni ambaye ni suala.

Funzo la kidokezo hapo  juu liko wazi kabisa. Huhitaji kuwa mtu wa kupiga kila sehemu, huhitaji kuwa mtu kushughulika na kila kitu bali unahitaji kuwa na lengo ambalo litakufanya ulifuate na kulifanyia kazi muda wote.

Soma zaidi.  MWELEKEO WA MAISHA YAKO TAREHE 12/05/2017

kuna umuhimu mkubwa sana wa kwa nini wewe unahitaji kuwa na malengo.

1.kukubakiza katika mwelekeo wa maisha yako.
Kutokuwa na malengo kutakufanya uguse kila kitu ambacho unaona kinakuja mbele yako. Utashughulika na kila kitu. Kitu ambacho huwezi katika maisha yako ni kufanya kila kitu, bali ni kufanya kitu kimoja na kuhakikisha kwamba unakifanya kwa ubora zaidi.
Lengo lako litakufanya uwe mtu wa wa kuhakikisha kwamba lengo limefanikiwa.

2. Lengo litakwambia kitu cha kufanya kikiwa cha kwanza.
Unapoamuka asubuhi, akili yako inakuwa na uwezo mkubwa sana wa kufanya mambo makubwa sana, bado akili yako inakuwa na uwezo wa kufanya zile kazi ambazo zinaweza kuwa zinaonekana ni ngumu. Lengo lako ndilo litakalokuambia ni kazi gani ambayo unapaswa kuanza nayo.

3. Lengo lako litakufanya uipangilie siku yako.
Moja kati ya maisha ambayo sio mazuri kuyachagua ni kuishi siku bila kujua unaenda kufanya nini. Yaani unasubiri muda utakapokutana na kitu chochote kile ufanye. Haya sio maisha ambayo unahitaji kuyachagua.  Malengo yako ni muhimu sana kwa ajili ya kukufanya wewe uweze kuipangilia siku yako. Hutakuwa mtu wa kufanya kila kitu kinachokuja mbele yako Bali utakuwa na ratiba maarumu ya siku husika.

.4.  Ukuaji binafsi.
Malengo yanakufanya ukue. Malengo yatakuhitaji uyapitie kila siku na uyasome, huku ukipangilia siku yako kwa namna ambavyo ungependa  hiyo siku iwe. Kitendo cha kupangilia siku yako ni ukuaji tosha kwako, ni hatua ya kukutoa hapo ulipo. Ni rahisi sana kwa kusikia ila kuna ukweli mkubwa sana ndani yake.

5. Kuweka malengo kutakufanya uwekeze nguvu zako katika kazi ambavyo unaifanya. Hii itakusaidia kufanya makosa machache sana, katika safari yako. Lakini pia utakuwa tayari unajua kwamba sasa umetoka nje ya malengo yako. Weka malengo leo hili na wewe uanze kupata vitu kama hivi.

6.kuna mtu mmoja aliwahi kusema kwamba Kile ambacho kinaweza kupimwa lazima kitaongezeka ubora. Kama wewe una lengo la kupungua uzito wa kilo12 baada ya muda fulani. Utaendelea kujipima, kadri unavyoyafanyia kazi malengo yako. Utakuwa unazidi kuona kwamba kuna mabadiliko mazuri katika Kile ambacho unafanya.

7. Ili uwe na maisha yenye furaha. utahitajika kufanya mambo kwa namna ambayo imepangiliwa na unaipenda wewe mwenyewe. Kama unafanya kwa sababu unafanya ila hufanyi kwa sababu unapenda kufanya kitu hicho basi jua kuna tatizo.

Malengo yako yatakufanya ufanye kitu na upangilie siku yako kadri ya vitu vile ambavyo unavipenda

8. Kuweka malengo ni kukataa kuwa mtu wa kawaida sana. Kuweka malengo ni kuamua kuwa shujaaa, Na kufanya mambo ya kishujaa kwa kuzitumia raslimali mubimu sana ambazo zipo ndani yako.

Weka malengo yako leo ili na wewe uweze kufaidika na haya ambavyo nayaandika hapa. Tukutane kileleni.

Ndimi kocha wako
Godius Rweyongeza
0755848391
godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X