*Sikati tamaa kwa sababu kila kosa ambalo Mimi nafanya, ni hatua ya kunipeleka Mimi mbele* alisema Thomas Edison.
Asubuhi ya leo maneno haya ya mgunduzi mkubwa sana wa dunia yameninijia katika tafakari yangu. Nikagundua kwamba ili kuuona ukweli ambao THOMAS EDISON ameuongelea unahitaji kuwa umevaa miwani chanya. Au miwani ambayo Fr. Faustine Kamugisha anasema *ni miwani ya Yesu* (ameandika katika Kitabu chake cha _umevaa miwani gani?_)
Kumbe kuona chanya katika vitu mbali mbali inasaidia sana. Lakini pia inahitaji moyo.
Anza kuona chanya katika kile ambacho wanasema. Usikate tamaa kwa sababu ulichotegemea kupata ni tofauti na Kile kilichopatikana. Siku zote kumbuka maneno ya Thomas Edison *
*Sikati tamaa kwa sababu kila kosa ambalo Mimi nafanya, ni hatua ya kunipeleka*
Usikate tamaa kwa sababu unafanya Biashara kwa hasara sasa hivi, hiyo nayo ni hatua nzuri kwako kusonga mbele. Jifunze kutoka hapo. Itumie hiyo na hakikisha kwamba unaitumia kutoka hapo ulipo kwenda unapotaka.
Jifunze kutokana na hilo jambo dogo ili uweze kufikia kubwa sana. Kumbuka kwamba
*Sikati tamaa kwa sababu kila kosa ambalo Mimi nafanya, ni hatua ya kunipeleka Mimi mbele*
Siku zote utakapoona kwamba umekwama na huwezi kupiga hatua simama wima na sema
*Sikati tamaa kwa sababu kila kosa ambalo Mimi nafanya, ni hatua ya kunipeleka Mimi mbele*
Ukiona watu wanakataa Kile ambacho unakifanya, wanakukatisha tamaa, wanakurudiaha nyuma, wanakucheka, simama tena sema
*Sikati tamaa kwa sababu kila kosa ambalo Mimi nafanya, ni hatua ya kunipeleka Mimi mbele*
Wapo walioambiwa hivyo kakini bado hawakukata tamaa Bali walisema
*Sikati tamaa kwa sababu kila kosa ambalo Mimi nafanya, ni hatua ya kunipeleka Mimi mbele*
Laiti watoto mapacha (wright brothers) wangekata tamaa baada ya kuambiwa kwamba hawawezi kutengeneza kitu chenye uwezo wa kupaa angani basi leo hii tusingekuwa na kitu kinachoitwa ndege ulaya, ila hawa vijana walijisemea kila mmoja wao kwamba *Sikati tamaa kwa sababu kila kosa ambalo Mimi nafanya, ni hatua ya kunipeleka Mimi mbele*
Na wewe leo sema hivyo hivyo.
Siku zote mabadiliko ni magumu sana kupokelewa na watu maana watu wengi sana wamezoea kuishi kwa kawaida sana. Watu hawataki mabadiliko. Hivyo kama, unataka kufanya mabdiliko makubwa sana basi kumbuka kwamba usikate tamaa. Hata kama watu watakuvuta, kataa na waambie kwamba
*Sikati tamaa kwa sababu kila kosa ambalo Mimi nafanya, ni hatua ya kunipeleka Mimi mbele*
Kumbuka kwamba mtu ambaye anaweza kukutatisha wewe tamaa ni wewe mwenyewe. Hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kukuvuta chini aua ambaye anaweza kukuinua juu isipokuwa wewe. Kumbe amua sasa maana mafanikio unayo mikononi mwako. Usikate tamaa, maana kila hata ambayo unapiga ni hata moja ya kwenda kileleni