Tumia Muda Na Watu Uwapendao


Habari za leo Rafiki yangu imani yangu umeamka salama na unaendelea vyema sana na kazi zako ambazo umekusudia kufanya siku ya leo. Leo ni siku njema sana, kwetu kwenda kuweka juhudi na kufanya mambo makubwa sana.

Kutokana na kwamba unapangilia ratiba yako kila siku asubuhi, najua wazi kwamba sasa hivi huna muda wa kupoteza hata kidogo. Uko kwenye mapambano makubwa sana. Kuna kitu kimoja ambacho hupaswi kukisahahau wakati unaendelea na shughuli zako za kutafuta mafanikio na kuwa tajiri. Kitu hili ni kuwa na muda wa kufurahi na uwapendao. Hiki sio kitu cha kusahau hata kidogo. Wapo watu wengi waliofikia mafanikio makubwa lakini wakaja kujikuta kuna kitu walipoteza, ndio! Wamegundua kwamba kuna kitu muhimu hawakufanya nacho ni kuwa na watu wawapendao kwa ukaribu.  Hili sio jambo jema ambalo linapaswa kukutokea wewe.

Mwandishi Robin Sharma anasema “kama ungekuwa na dakika thelethini za kuishi hapa duniani basi bila shaka ungetumia muda wako kwa ajili ya kuwapigia na kuongea na watu uwapendao. Ungewapigia wazazi, mpenzi wako, make wako na watoto wako.”

Kazi ya kufanya leo.
1. Wapigie simu watu uwapendao na uwaambie kwamba unawapenda.
2. Watumie meseji watu uwapendao na uwakumbushe umuhimu wao kwako.
3. Tenga muda wa kukaa na watu wako wa karibu mkiongea na kubadilishana mawazo mbali mbali.

Tukutane kileleni.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X