HAWA NDIO WATU WA KUOGOPA
Habari za leo rafiki yangu na ndugu msomaji wa blogu yako ya songa mbele. Imani yangu ni kwamba unaendelea vyema katika kuhakikisha kwamba unaweza kupiga hatua na kutoka hapo ulipo kwenda mpaka kileleni. Kumbuka kwamba wewe ni kiongozi wa nafsi yako na maisha yako hivyo unahitaji kuipangilia siku yako ili iwe bora sana. Kama ulikuwa bado hujaipangilia basi kumbuka kwamba huu ndio muda muafaka wa wewe kuhakikisha kwamba unaipangilia siku yako. Andika chini mambo ya msingi ambayo unaenda kuyafanya asubuhi ya leo ambayo yataongeza thamani kwenye maisha yako na ya watu wengine.
Katika mazungumzo yetu ya leo tunaenda kuangalia nai watu gani ambao unahitaji kuwaacha wewe kama kiongozi. Watu ambao huhitaji kuambatana nao, maana wanaweza kukupoteza na kukuharibia malengo yako.
1. WATU AMBAO HAWAKO TAYARI KUBEBA MAJUKUMU.
Kuna watu ambao hawapo tayari kubeba majukumu yao. Kila linapotokea suala fulani wao wanachokifanya kuwatupia watu wengine mpira ili wao waonekane kwamba hawakuhusika hata kidogo yaani wapo salama. Watu kama hawa sio wazuri wa kuambatana nao. Watu wa aina hii wapo tayari kupoteza muda wao kuanza kuzunguzia wewe na ili wawavute watu wengine ionekane kwamba wewe ni mtu mbaya sana. Mfano wa watu hawa ni wale ambao mnakuwa mmepewa jukumu moja la kiofisi au kamati fulani. Mnajitahidi kwa pamoja kuhakikisha kwamba mmefanya na kutimiza majukumu yenu. Lakini kinachotokea pale ambapo kazi inaonekana ina kasoro kidogo wao hawapo tayari kuhakikisha kubeba jukumu hilo. Wanakutupia wewe mpira. Watu kama hawa tajiri mkubwa sana ambaye amewahi kuishi duniani ambaye ni mfalme Solomon alikuwa akiwaita wajinga.
2. WATU AMBAO WANATAKA KULA KABLA YA KULIPA GHARAMA.
Kuna watu ambao wanafurahia kupata ila hawafurahii kutoa. Watu ambao wao muda wote wapate kitu kutoka kwako hasa pale unapokuwa nacho , kikiisha basi hawaonekani tena mpaka pale utakapokuwa nacho tena. Mfano kama wewe ni mfanyakazi. Unapoingia mshahara kuna watu fulani unakuta wanaanza kukupigia simu, kujisogeza karibu yako ili waweze kupata kitu fulani kutoka kwako. Lakini mshahara wako ukiisha huwaoni tena. Huwasikii tena wakikujulia hali, hawapiti tena karibu yako wala hawajihusishi na kile ambacho unafanya. Wakwepe sana watu wa aina hii.
Hawa ndio watu wambao tajiri mkubwa kuwahi kuishi duniani anawaita wajinga.
Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha kutoka kwenye blogu hii
Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391