Asubuhi ya siku hii ya leo ni njema sana na ni ya kumshukuru Mungu. Leo ikiwa ni tarehe 9 juni 2017. Huku siku za mwaka huu zikizidi kusonga mbele. Hapo ndipo ninapokumbuka maneno yanayosema kwamba “poteza sekunde moja leo hii, utaililia maisha yako yote”.
Lakini hapo hapo nakumbuka msemo mmoja wa China unaosema kwamba “ukipoteza pesa utaipata, lakini ukipoteza muda, hautaupata maisha yako yote”. Hivyo ndani ya siku ya leo nimeamua kuutumia vizuri sana muda wa leo, na kila dakika nimeipangilia vilivyo. Bila shaka na wewe utaipangilia siku yako ya leo ili uhakikishe unaenda kufanya Kile ambacho ni chema sana.
Katika makala ya leo tunaenda kuzungumzia sifa ambayo kila mtu anayo. Hii ni sifa ambayo ni njema sana, sema tu, kuna watu ambao wanaitumia vizuri wakati huohuo kuna watu ambao wanaitumia vibaya.
Laiti kama kila mtu angeitumia vizuri sifa hii, basi maisha yangekuwa ni rahisi sana maana kila mtu angetambua wajibu wake na kuutimiza. Ndio, huu ndio ukweli.
Kila mwanadamu ni kiongozi. Na kiongozi ni mtu ambaye anaweza kupangilia vitu vyake na kuhakikisha kwamba anatoka sifuri, (yaani hapo alipo) mpaka kileleni.(yaani hatua ya juu ambavyo anataka kufikia). Kiongozi pia ni mtu ambaye anabeba maono ya watu na kuwainua ili kutoka hapo walipo kwenda hatua ya ziada mbeleni. Kiongozi ni mtu ambaye anaona mbali na kufika huko wakati wengine hawajapaona na wakati wengine hawajafikiria hata kidogo kuhakikisha kwamba, wanaweza kufika huko. Huyo ndiye kiongozi. Na hii ndiyo sifa moja muhinu sana, ambayo kila mtu anayo.
“Kila mtu ni kiongozi lakini sio viongozi wote ni sawa.” Haya ni maneno ya Robin Sharma.
Kama ilivyo kwamba ili kampuni bora iweze kuwepo inahitaji watu ambao wanajituma katika kufanya kazi na shughuli bora ndivyo ilivyo katika hali ya kwaida ya maisha. Hapa sio kwamba najaribu kusisitiza juu ya umuhimu wa kila mtu kuwa na kampuni najaribu kusisitiza maneno ya baba wa taifa letu la Tanzania mwalimu Julius Kambarage Nyerere abaye alisema kamba “play your part”. Akiwa anamtaka kila mtu abebe majukumu yake na kuhakikisha kwamba ameyatimiza.
Jua wajibu wako, kila mtu akijua wajibu wake na kuhakikisha kwamba ameutimiza basi, ni hatua nzuri sana ya kuhakikisha kwamba maendeleo yanakuwepo. Haijalishi unafanya kazi gani, lakini ukweli kwamba unapaswa kutimiza wajibu wako ni suala la msingi sana.Uongozi
Kila mtu ni kiongozi, lakini tofauti inayowatofautisha viongozi mbalimbali ni utendaji wa kazi. Kila mtu ana namna yake ya utendaji. Hakikisha kwamba unakuwa na misingi mizuri sana ya kufanya kazi. Maana wewe ni kiongzi. Hii ni sifa ambayo unayo hivyo usikubali uipoteze.
Tukutane kileleni.
MUHIMU SANA;
Kuna semina ya ambavyo nimeipa kichwa cha TIMIZA MALENGO YA MWAKA MZIMA NDANI YA MIEZI SITA. Ndio namaanisha miezi sita. Ndani ya semina utapata kujifunza mambo mengi sana yatakayokusaidia sana wewe kutimiza malengo yako mwaka huu. Kikubwa zaidi katika kutekeleza na kutimiza malengo yako nimekuja na mfumo Mpya ambao binafsi nimeutumia ndani ya miezi sita na umenipa matokeo makubwa sana katika kutimiza malengo yangu. Mfumo huu unaitwa MFUMO WA NYUMBA (HUOUSE SYSTEM). Huu ni mfumo Mpya hapa duniani, na binafsi nimeutumia umenipa matokeo makubwa. Naenda kuwa nakudadafulia mfumo huu kwa undani kwenye semina hii ambayo nitaiendesha. Kiufupi kosa mengine mwaka huu ila usikose kujifunza mfumo huu ambao unaitwa MFUMO WA NYUMBA.
Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao kupitia katika kundi la waspu la HAZINA.
Hii ni kutokana na hali ya kwamba
1. mtu yeyote anaweza kuhudhuria semina hii akiwa hata nyumbani kwake bila kutumia gharama nyingi za usafiri kuja huku nilipo Mimi.
2. Lakini pia kutokana na ukweli kwamba mtu yeyote yule ambaye Yupo kwenye kona yoyote ile ya dunia anaweza kuhudhuria semina hii.
3. Gharama za uendeshaji wa semina zinapungua hivyo kukuwezesha wewe kuweza kuhudhuria semina bila kikwazo chochote kile.
JINSI YA KUJIUNGA NA SEMINA HII.
Gharama ya semina hii ni kiasi kidogo sana cha 20,000/- za kitanzania. Hii ni gharama ndogo sana kulinganisha na kitu kikubwa sana ambacho unaenda kukipata ndani ya semina hii itakayoanza mwezi wa saba tarehe 15 mpaka tarehe 19.
Jinsi ya kulipia.
Tuma pesa kupitia namba ya voda MPESA 0755848391 yenye jina la GODIUS RWEYONGEZA. baada ya hapo nitumie ujumbe wenye neno HAZINA wasapu namba 0755848391. Ili niweze kukuunganisha kwenye mundi hilo tayari kwa ajili ya semina hii.
MANUFAA MENGINE YA KUNDI LA HAZINA.
1. Kwanza kabisa ni muhimu sana kufahamu kwamba kundi la hazina ni tofauti na makundi mengine ya wasapu ambayo umeyazoea. Kundi hili lina watu makini ambao wapo tayari kuhakikisha kwamba wanatimiza malengo yao. Watu walio katika kundi hili huwa wanalipia elfu ishirini kila baada ya miezi sita kuwa katika kundi hilo.
2. Lakini pia kuwa katika kundi hili kutakuleta karibu sana na Mimi ambapo nitakuwa tayari kukusaidia na kuongea na wewe hapo muda wowote ule kuhakikisha kwamba unafikia Kile kilichobora zaidi.
3. Lakini pia nitahakikisha kwamba tunafanya kazi bega kwa bega ili kuhakikisha kwamba unatimiza Malengo yako ndani ya miezi sita.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwa sasa siwezi kuwa kwenye kila kundi na kumsaidia kila mtu maana ninazo kazi nyingi sana ambazo zimenibana, hivyo kuwa kwako katika kundi la hazina ni kitu ambacho kitatufanya tuwe karibu sana muda wote.
4. Lakini pia utapata nafasi nzuri sana ya kuhudhuria semina ya kufungua mwaka 2018 bure kabisa. Hii ni kutokana na ukweli kwamba bado ada yako ya miezi sita itakuwa bado haijaisha hivyo utazidi kupata kilichobora sana kutoka kwangu.
Hivyo hakikisha kwamba haukosi nafasi hii adimu sana kwako kuweza kufanya mambo makubwa sana.
Hakikisha hauikosi nafasi hii adimu
Ni Mimi Rafiki na kocha wako
Kocha Godius Rweyongeza
0755848391
godius
Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha kutoka kwenye blogu hii