Hiki Ni Kitu Ambacho Huwezi Kukinunua Sokoni




Habari za leo rafiki na ndugu masomaji wa makala za SONGA MBELE BLOG, imani yangu leo ni siku bora sana kwako na tayari umefanya mambo makubwa sana ndani ya siku yako ya leo. Ikiwa ni tarehe  15 June 2017. Siku kama ya leo hatutakuja kukutana nayo tena maishani mwako. Hivyo ni bora sana kujua umuhimu mkubwa sana wa kuitumia siku ya leo vizuri maishani mwako.
Katika makala ya leo tunaenda kunaona, kitu kimoja ambacho huwezi kamwe kukinunua sehemu yoyote, wala huwezi kukiazima kwa mtu yeyote. Kitu hiki mpaka ukitafute wewe mwenyewe na uhakikishe kwamba umeweza kukipata na kimo ndani yako. Kuna watu wameishi hapa duniani bila kukiona kitu hiki. Latika makala ya leo nitahakikisha kwamba ninakieleza kwa undani ili kuhakikisha kwamba unaweza kukielewa vizuri. Kuna mtu mmoja ambaye aliwahiza kusema kwamba ukienda kaburini utawakuta utajiri wa kila aina. Utawakuta watu ambao,  walikuwa wana vitabu vizuri ndani yao. Utawakuta watu ambao walikuwa na mziki mzuri ambao hawakutaka kuucheza. Utawakuta watu ambao walikuwa viongozi maarufu ila hawakuwahi kudhubutu kuchukua hatua. Hwa ni kwa sababu tu hawakukifahamu kitu hiki ambacho huwezi kukkinunua sokoni, wala huwezi kukikuta supermarket.
Ni muhiimu sana kufahamu kwamba katika maisha kuna vitu vingi sana vya kuchagua. Unaweza kuchagua mchumba, unaweza kuchagua aina gani ya nyumaba ambayo ungependa kuishi, unaweza kuchagua nchi gani unataka kuishi au kutembelea, yaani kuna vitu vingi sana vya kuchagua kiasi kwamba siwezi kuvitaja vyote hapa.
Kama ambavyo vipo vitu vingi sana vya kuchagua ndivyo ambavyo vipo vitu vingi sana vya kununua. Unaweza kununua gari ulipendalo, au wengine wanaliita gari la ndoto yako, unaweza kununua kiwanja, unaweza kununua chakula. Lakini bado kuna vitu amabvyo huwezi kununua.
Nimeanza kueleza kwa umakini juu ya suala zima la kuchagua na kununua maana vitu hivi vinaendana. Kuna vitu ambavyo ukishachagua utahitajika kuvinunua ingawa sio vitu vyote vinavyochaguliwa vinanunuliwa.
Inasemekana mwanadamu ana siku 25550  za kuishi maisha yake hapa duniani. Ndani ya siku hizi kuna kitu ambacho tunategemea aweze kukifanya bila kutumia nguvu kubwa sana. kitu ambacho tangu siku ya kwanza  alipokuja hapa duniani alikifanya. Ndio ni kitu muhimu sana, nacho ni KUSUDI LA MAISHA. Hiki ni kitu pekee hapa duniani ambacho huwezi kuchagua wala, kununua.
Tunapozungumuzia kusudil la maisha tunakuwa tunazungumzia au tunajiuliza swali
·       JE, KWA NINI NIPO HAPA DUNIANI?
·       JE, NINATAKA KUWA NANI?
·       JE, MALENGO YANGU NI YAPI?
·       NDOTO ZANDU NI ZIPI?
Kusudi la maisha ni zaidi malengo ambayo unayo. Kusudi la maisha sio kazi ambayo unaifanya. Kusudi la maisha sio kitu ambacho unafanya. Kusudi la maisha ni zaidi ya hapo.
SASA NITAWEZAJE  KULIJUA KUSUDI LA MAISHA YANGU?

NANI AMEKUWEKA HAPO ULIPO?
Kuna mtu mtu mmoja alikuwa anatembea mlimani akitaka kwenda mpaka kileleni. Alitembea kwa siku saba.  Baadae akawa amepotea njia. Hakuwa na uhakika na sehemu ya kupitia. Ndipo katika mahangaiko yale alimwona mtu mmoja na akaamua kumuuliza. Hivi nikitaka kufika kileleni nifanyeje? Hapo ndipo alipoambiwa kwamba ukitaka kufika kileleni huwezi kuanzia hapa. Lazima uanzie upande wa pili. Haa! Kumbe huu ni ukweli, ambao hata sisi tunakutana nao maishani mwetu! Ili uweze kuligundua kusudi la maisha yako, huhitaji kuanzia ndani mwako! Bali unahitaji kuanzia nje yako.
Najua haya maneno haya ni mapya masikioni mwako na ni mara yako ya kwanza kusoma maneno kama haya, maana siku nyingi sana umekuwa unasikia, habari kutoka kwa watu kwamba ukitaka kubadilika, na kufikia mafanikio makubwa anzia ndani yako. Lakini leo hii nakwambia hivi ukitaka kulijua kusudi la maisha yako ANZIA NJE YAKO. UKITAKA KUJUA KUSUDI LA MAISHA YAKO NI MUHIMU SANA KUANZIA KWA MUNGU. Huwezi kulijua kusudi la maisha yako kwa kuanzia ndani yako wewe mwenyewe. Huwezi kulijua kusudi la maisha kwa kuanza kujiangalia wewe mwenyewe. Ila unaanza kwa kumwangalia mtu ambaye amekuumba wewe.
 Mwanadamu ametengeneza gari akiwa anajua kusudi la gari ni nini? Hivyo ili uweze kujua kusudi la gari lazima uende kwa mtu ammbaye ametenegeneza gari na uonee naye. Hapo ndipo utaweza kulijua kusudi la kutengeneza gari. Vivyo hivyo ukitaka kulijua kusudi la kutengeneza nyumba utaenda kwa mtu ambaye alitengeneza nyumba na kumuuliza kwa nini ulitengeneza nyumba hii. Huyo mtu atakuwa na majibu ya kukupa  wewe hapo.
Ni kwa mantiki hiyo hiyo tunajua wazi kwamba ukitaka,kulijua kusudi la maisha yako lazima uende kwa mtu ambaye alikuumba wewe hapo. Hiyo ndiyo njia ya kwanza, ya kuhakikisha unagundua kusudi la maisha yako.
WATU WENGINE WANASEMAJE?
Njia nzuri sana ya kuhakikisha kwamba unaweza kuligundua kusudi lako la maisha ni kuhakikisha kwamba unawasikiliza watu wengine wanasemaje, je rafiki zako wau watu wengine wa karibu wanasemaje? Unaweza kuwasikiliza watu wengine wanasemaje juu ya kitu ambacho unakiweza, juu ya kitu ambacho wao wanaona unakiweza kwenye maisha yao zaidi ya wengine. Wasikilize hawa watu wanasemaje, ili uweze kuligundua kusudi lako la misha!
MAMBO YA KUFANYA SIKU YA LEO!
Jiulize ni ktu gani ambacho watu wanakikubali zaidi ya watu wengine?
Ni kitu gani ambacho unaweza kukifanya kwa muda mkubwa sana bila kuchoka?
Tukutane kileleni.
MUHIMU SANA;
Kuna semina ya ambavyo nimeipa kichwa cha TIMIZA MALENGO YA MWAKA MZIMA NDANI YA MIEZI SITA.  Ndio namaanisha miezi sita. Ndani ya semina utapata kujifunza mambo mengi sana yatakayokusaidia sana wewe kutimiza malengo yako mwaka huu. Kikubwa zaidi katika kutekeleza na kutimiza malengo yako nimekuja na mfumo Mpya ambao binafsi nimeutumia ndani ya miezi sita na umenipa matokeo makubwa sana katika kutimiza malengo yangu. Mfumo huu unaitwa MFUMO WA NYUMBA (HUOUSE SYSTEM). Huu ni mfumo Mpya hapa duniani, na binafsi nimeutumia umenipa matokeo makubwa. Naenda kuwa nakudadafulia mfumo huu kwa undani kwenye semina hii ambayo nitaiendesha. Kiufupi kosa mengine mwaka huu ila usikose kujifunza mfumo huu ambao unaitwa MFUMO WA NYUMBA.

Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao kupitia katika kundi la waspu la HAZINA.
Hii ni kutokana na hali ya kwamba

1. mtu yeyote anaweza kuhudhuria semina hii akiwa hata nyumbani kwake bila kutumia gharama nyingi za usafiri kuja huku nilipo Mimi.

2. Lakini pia kutokana na ukweli kwamba mtu yeyote yule ambaye Yupo kwenye kona yoyote ile ya dunia anaweza kuhudhuria semina hii.

3. Gharama za uendeshaji wa semina zinapungua hivyo kukuwezesha wewe kuweza kuhudhuria semina bila kikwazo chochote kile.

JINSI YA KUJIUNGA NA SEMINA HII.
Gharama ya semina hii ni kiasi kidogo sana cha 20,000/- za kitanzania. Hii ni gharama ndogo sana kulinganisha na kitu kikubwa sana ambacho unaenda kukipata ndani ya semina hii itakayoanza mwezi wa saba tarehe 15 mpaka tarehe 19.

Jinsi ya kulipia.

Tuma pesa kupitia namba ya voda MPESA 0755848391 yenye jina la GODIUS RWEYONGEZA. baada ya hapo nitumie ujumbe wenye neno HAZINA wasapu namba 0755848391. Ili niweze kukuunganisha kwenye mundi hilo tayari kwa ajili ya semina hii.

MANUFAA MENGINE YA KUNDI LA HAZINA.
1. Kwanza kabisa ni muhimu sana kufahamu kwamba kundi la hazina ni  tofauti na makundi mengine ya wasapu ambayo umeyazoea. Kundi hili lina watu makini ambao wapo tayari kuhakikisha kwamba wanatimiza malengo yao. Watu walio katika kundi hili huwa wanalipia elfu ishirini kila baada ya miezi sita kuwa katika kundi hilo.

2. Lakini pia kuwa katika kundi hili kutakuleta karibu sana na Mimi ambapo nitakuwa tayari kukusaidia na kuongea na wewe hapo muda wowote ule kuhakikisha kwamba unafikia Kile kilichobora zaidi.

3. Lakini pia nitahakikisha kwamba tunafanya kazi bega kwa bega ili kuhakikisha kwamba unatimiza Malengo yako ndani ya miezi sita.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwa sasa siwezi kuwa kwenye kila kundi na kumsaidia kila mtu maana ninazo kazi nyingi sana ambazo zimenibana, hivyo kuwa kwako katika kundi la hazina ni kitu ambacho kitatufanya tuwe karibu sana muda wote.

4. Lakini pia utapata nafasi nzuri sana ya kuhudhuria semina ya kufungua mwaka 2018 bure kabisa. Hii ni kutokana na ukweli kwamba bado ada yako ya miezi sita itakuwa bado haijaisha hivyo utazidi kupata kilichobora sana kutoka kwangu.

Hivyo hakikisha kwamba haukosi nafasi hii adimu sana kwako kuweza kufanya mambo makubwa sana.

Hakikisha hauikosi nafasi hii adimu



Ni Mimi Rafiki na kocha wako
Kocha Godius Rweyongeza
0755848391
godius

Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii


Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA

Kujiunga kundi la wasapu la SONGA MBELE BONYEZA HAPA

BIDEISM BLOG



Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X