HIZI NI KAULI MBIU MBILI AMBAZO KILA MWANAMAFANIKIO ANAZIHITAJIHabari za siku ya leo rafiki na ndugu msomaji wa blogu ya SONGA MBELE. Imani yangu leo ni siku bora sana kuwahi kutokea katika maisha yako bila kujali unahali gani kiafya. Kwa kuwa wewe unapumua na umeweza kusoma makala hii, basi hapo unahitaji kumshukuru Mungu kwa sababu ya zawadi hii ya kipekee ambayo unayo siku hii ya leo.
Kuna kauli nyingi sana zimeweza kusemwa na watu wengi sana juu ya mfanikio. Bila shaka utakuwa umesikia na kusoma makala mbali mbnali kutoka kwa watu mbali mbali kwamba unahitaji kuwa mtu wa kujisemea kauli chanya kila siku unapoamuka. Kauli chaya huwa zinakufanya unaianza siku yako kwa namna ambayo  ni ya tofauti. Lakini pia hukupa nguvu ya wewe kuweza kuendelea vizuri na siku yako. Maneno unayojisemea dakika chache baada ya kuamuka yana nguvu kubwa sana na madhara makubwa sana juu ya aina siku ambayo unaenda kuiishi.


Kuna siri kubwa sana ambayo huwa inaifanya serikali inakuwa na kauli mbiu mbali mbali katika shughuli mbali mbali. Mfano katika mbio za mwenge mwaka huu serikali imweka kauli mbiu yake, na ndivyo  imekuwa  ikifanya kwa siku nyingi sana. kuna kauli mbiu nyingine ambazo serikali imezitumia katika sekta za kilimo, biashara, afya, michezo kutaja ila machache. Kwa kuangalia kwa jicho la kawaida unaweza kuona kauli hizi hazina maana, ila kwa kuwa sisi tunaziangalia kwa jicho la dhahabu basi  tunaona kwamba kauli hizi hapa zina umuhimu mkubwa sana.
 Ndio maana katika makala ya leo tunaenda kujifunza kauli mbili muhimu ambazo unazihitaji  katika maisha yako ili uweze kuendelea kusonga mbele na kufanya makubwa zaidi. Kauli hizi utajisemea muda wowote na utaziandika sehemu. Na kuzifanya kuwa sehemu ya maisha yako kuhakikisha kwamba zinakuongoza katika kazi zako ambazo unakuwa unazifanya kila siku.


1.     HAKUNA MIPAKA. (no boundaries). Hii ni kauli mbiu yenye maana kubwa sana katika maisha yako. Ni muhimu sana kufahamu kwamba upo katika jamii ambayo inaamini sana katika kutokuwezekana kuliko inavyoamini katika kuwezekana. Kumbe wewe unachohitaji ni kuhakikisha kwamba unachukua hatua bila kujali jamii inasemaje na kufanya kile ambacho jamii yako inanona kama vile hakiwezekani. Kuna mfano wa mtu katika bibllia ambaye alichukua hatua za hatari na kwenda kupambana kile ambacho jamii iliona kama vile hakiwezi kuguswa. Mtu huyu ni DAUDI. Kumbe na wewe katika jamii yako umezungukwa na vitu vingi ambavyo jamii yako inaamini kwamba haiwezekani, vitu ambavyo ukianza kufanya watu watasema kwamba havijawahi kufanyika katika sehemu yoyote ile ya dunia hii. Hapo ndipo huwa napenda kuwaambia watu kwamba wasikie ila usiwasikilize.

Mwandishi ANTONY ROBINS aliandika kitabu chenye kichwa cha UNLIMITED POWER, akiamaanisha kwamba hakuna mipaka katika kile ambacho unakifanya. Unaweza kufanya kitu chochote kikubwa kwa ukubwa unaoutaka, kama utaamua.  Bila shaka msukumo huo huo ndio uliomfanya JOHN MASON  kuandika kitabu chenye kichwa cha THE IMPOSSIBLE IS POSSIBLE, akimaanisha kwanba yasiyowezekana yanawekana.

Nakubaliana na HENRY MILLER aliyewahi kusema kwamba “mtu anayetafuta usalama hata katika akili yake ni sawa na mtu anayekata miguu yake, ili awe na miguu bandia kwa ajili ya kuepuka matatizo”. Kumbe ni muhimu sana kufahamu kwamba siku zote huwa hakuna mipaka tofauti na ile ambayo huwa wewe unaiweka katika akili yako. Na “maaedeleo ambayo yametokea katika kila kizazi yametokana na ukweli kwamba kuna watu wamewekeza na kuhakikisha kwamba wanafanya yale ambayo yanaamika kwamba hayawezekani”. Alisema Russen Davenport
Kazi ya kufanya siku ya leo. Tafuta kitu ambacho watu wanasema kwamba hakiwezi kufanyika na kifanye hicho! Nenda hatua ya ziada katika kufanya kitu hicho hadi wale ambao wanasema kwamba haiwezekani waone aibu wao wenyewe.

FANYA KITU KIKUBWA ZAIDI YAKO. Kama unataka kuhakikisha uhai wa kile ambacho unaamini hakikisha kwamba unaanza kukifanya. Hakuna muda wa kusubiri sasa hivi kwa kusema kwamba nitakapokuwa tayari. Muda wenyewe ni sasa. Anza kufanya mambo makubwa sana siku hii ya leo. Yale ambayo yanaonekana hayawezekani leo hii, yatabaki bila kuwezekana miaka mitano ijayo kama hutachukua hatua leo ya kuanza kuyafanya. Lakini kama utachukua hatua basi yataawezekana.

2.      WE FANYA TU! (just do it)
Je, kuna kitu unataka kufanya? Je, kuna kitu umeanza kufanya tayari? Kama bado umesubiri nini?  Kitu gani kinakuzuia? Kama umeaza mpaka sasa hivi umefikia hatua gani? Je, hatua gani ya ziada ambayo ungependa kupiga katika kitu kile ambacho unakifanya? Haya ni maswali ya muhimu sana ambayo unahitaji kujiuliza haswa unapokuwa unapaswa kupiga hatua kubwa sana.na baada ya hapo kinachofuata ni kuchukua hautua kubwa sana.
Wewe fanya tu! Hakuna mtu ambaye amekaa chini na kuanza kukuangalia au kukukcheka, ukiona unafikiri hivyo jua kwamba anayekucheka ni mtu mmoja tu! Na mwenyewe ni wewe.
Je unataka kufanya biashara? Wewe fanya tu! Hata kama utakuja kushindwa utasema nilikuwa nafanya tu!

MUHIMU SANA KUZINGATIA: kauli hii usije ukaitumia kwa kufanya vitu kwa makosa na mazoea hata pale unapoona kuna uwezekano wa kufanya kwa ubora wa hali ya juu sana ila bado unakazan kusema kwamba mimi nafanya tu! Na unafanya bila kuongeza thamani, WEWE FANYA TU! ILA FANYA KWA UBORA
KUMBUKA KWAMBA UNAPASWA
·        Kufanya zaidi ya kuwepo………….ISHI
·        Kufanya zaidi ya kusikia……………SIKILIZA
·        Kufanya zaidi ya kukubali………….KUSHIRIKIANA
·        Kufanya zaidi ya kuongea………….KUWASILIANA
·        Kufanya zaidi ya kutumia…………KUWEKEZA
·        Kufanya zaidi ya kufikiri……………KUBUNI
·        Kufanya zaidi ya kushirikisha…………KUTOA
·        Kufanya zaidi ya kusamehe…………..KUSAHAU
·        Kufanya zaidi ya kufikiri ………….KUPANGA
·        Kufanya zaidi ya ndoto…………….KUFANYA
·        Kufanya zaidi ya kusoma ………………KUTENDA
·        Kufanya zaidi ya kuongeza………….KUZIDISHA
Tukkutane kileleni


MUHIMU SANA;
Kuna semina ya ambavyo nimeipa kichwa cha TIMIZA MALENGO YA MWAKA MZIMA NDANI YA MIEZI SITA.  Ndio namaanisha miezi sita. Ndani ya semina utapata kujifunza mambo mengi sana yatakayokusaidia sana wewe kutimiza malengo yako mwaka huu. Kikubwa zaidi katika kutekeleza na kutimiza malengo yako nimekuja na mfumo Mpya ambao binafsi nimeutumia ndani ya miezi sita na umenipa matokeo makubwa sana katika kutimiza malengo yangu. Mfumo huu unaitwa MFUMO WA NYUMBA (HOUSE SYSTEM). Huu ni mfumo Mpya hapa duniani, na binafsi nimeutumia umenipa matokeo makubwa. Naenda kuwa nakudadafulia mfumo huu kwa undani kwenye semina hii ambayo nitaiendesha. Kiufupi kosa mengine mwaka huu ila usikose kujifunza mfumo huu ambao unaitwa MFUMO WA NYUMBA.

Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao kupitia katika kundi la waspu la HAZINA.
Hii ni kutokana na hali ya kwamba

1. mtu yeyote anaweza kuhudhuria semina hii akiwa hata nyumbani kwake bila kutumia gharama nyingi za usafiri kuja huku nilipo Mimi.

2. Lakini pia kutokana na ukweli kwamba mtu yeyote yule ambaye Yupo kwenye kona yoyote ile ya dunia anaweza kuhudhuria semina hii.

3. Gharama za uendeshaji wa semina zinapungua hivyo kukuwezesha wewe kuweza kuhudhuria semina bila kikwazo chochote kile.

JINSI YA KUJIUNGA NA SEMINA HII.
Gharama ya semina hii ni kiasi kidogo sana cha 20,000/- za kitanzania. Hii ni gharama ndogo sana kulinganisha na kitu kikubwa sana ambacho unaenda kukipata ndani ya semina hii itakayoanza mwezi wa saba tarehe 15 mpaka tarehe 19.

Jinsi ya kulipia.

Tuma pesa kupitia namba ya voda MPESA 0755848391 yenye jina la GODIUS RWEYONGEZA. baada ya hapo nitumie ujumbe wenye neno HAZINA wasapu namba 0755848391. Ili niweze kukuunganisha kwenye mundi hilo tayari kwa ajili ya semina hii.

MANUFAA MENGINE YA KUNDI LA HAZINA.
1. Kwanza kabisa ni muhimu sana kufahamu kwamba kundi la hazina ni  tofauti na makundi mengine ya wasapu ambayo umeyazoea. Kundi hili lina watu makini ambao wapo tayari kuhakikisha kwamba wanatimiza malengo yao. Watu walio katika kundi hili huwa wanalipia elfu ishirini kila baada ya miezi sita kuwa katika kundi hilo.

2. Lakini pia kuwa katika kundi hili kutakuleta karibu sana na Mimi ambapo nitakuwa tayari kukusaidia na kuongea na wewe hapo muda wowote ule kuhakikisha kwamba unafikia Kile kilichobora zaidi.

3. Lakini pia nitahakikisha kwamba tunafanya kazi bega kwa bega ili kuhakikisha kwamba unatimiza Malengo yako ndani ya miezi sita.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwa sasa siwezi kuwa kwenye kila kundi na kumsaidia kila mtu maana ninazo kazi nyingi sana ambazo zimenibana, hivyo kuwa kwako katika kundi la hazina ni kitu ambacho kitatufanya tuwe karibu sana muda wote.

4. Lakini pia utapata nafasi nzuri sana ya kuhudhuria semina ya kufungua mwaka 2018 bure kabisa. Hii ni kutokana na ukweli kwamba bado ada yako ya miezi sita itakuwa bado haijaisha hivyo utazidi kupata kilichobora sana kutoka kwangu.

Hivyo hakikisha kwamba haukosi nafasi hii adimu sana kwako kuweza kufanya mambo makubwa sana.

Hakikisha hauikosi nafasi hii adimuNi Mimi Rafiki na kocha wako
Kocha Godius Rweyongeza
0755848391
godius
Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii


Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA 
Kujiunga kundi la wasapu la SONGA MBELE BONYEZA HAPA

BIDEISM BLOG


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X