Huu Ndio MudaMzuri kwako Kwenda Kufanya Kazi 
Habari za siku ya leo rafiki yangu na ndugu msomaji wa makala za songa mbele. Imani yangu umeianza siku yako kwa namna ya tofauti kabisa kwa kufanya kitu ambacho kinakutofautisha wewe na watu wengine. Kuna mambo mengi ambayo yanakutofautisha wewe na watu wengine, ila mambo mawili ambayo naamini asubuhi ya leo utakuwa umeanza nayo ni kusoma malengo yako pamoja na kujisemea kauli ambazo ni chanya. Haya ni mambo mawili ambayo ni ya muhimu sana kwako unapokuwa unaianza siku yako. Kama ulikuwa mpaka sasa hujaianza siku yako kwa kusoma malengo yako ,sasa nakushauri ukayasome lakini pia hakikisha kwamba umeweza kujisemea kauli ambazo ni chanya. Maneno kama mimi ni mshindi, nitafanya mambo makubwa siku ya leo….. unaweza kutengeneza listi kubwa sana ya maneno kama hayo na kuyaweka sehemu ambayo inaonekana na kuhakikisaha kwamba unapoianza siku yako unaianza kwa kujisemea kauli chanya kama hizi hapa ambazo zitakutoa hapo ulipo na kukupeleka hadi kileleni.Sasa turudi kwenye makala yetu ya siku ya leo ambapo tunaenda kujifunza na kuangalia ni muda gani ambao wewe unakufaa sana kuweza kufanya kazi. muda mzuri kwako kwenda kufanya kazi ambayo ni bora sana.

  

Mwingine anaweza kusema kwamba mimi kila muda unanifaa kufanya kazi zangu, lakini je hii ni kweli? Kauli hii tukiiangalia kwa jicho la kawaida tutaona ina ukweli ndani yake kwa asilimia 90% na zaidi. Lakini sasa tuje kwenye ukweli wenyewe na hapa tutapaswa kuvaa miwani. Wakati wengine wamekuwa wakiangalia kwa jicho la kawaida na kutoa maoni yao. Sisi tutaangalia kwa jicho la la kawaida pamoja na miwani na hapa tutakuja na miwani ambayo ni bora sana.

 

Swali narirudisha tena mezani. Je ni muda gani unafaa kwako kufanya kazi?  kabla hatuajaanza kuuangalia ukweli uliojificha nyuma na kujua ni muda gani ni mzuri zaidi kwako kwenda kufanya shughuli zako, naomba tutambue ukweli kwamba kila mtu huwa anafanya kazi ingawa kiwango cha ufanyaji wa kazi ndicho ambacho hutofautiana. Wapo ambao wanafanya kazi kwa saa moja, mawili na wengine wanaafanya kazi masaa nane, wakati wengine wakifanya kazi zaidi hata ya masaa kumi na mbili. Nawapongeza nyote kwa kazi nzuri ambayo mnaifanya.

 

Katika kile kitu ambacho unafanya kuna watu ambao wanafanya kazi kama wewe. Kama wenzako wanafanya kazi masaaa nane na wewe unafanya kazi hayohayo,Sasa kuna tofauti gani kati yako wewe na watu wengine?  Nyote mkichoka mnaacha na kwenda kupumuzika? Sasa hapo tunahitaji kujua utofauti ambao utakutofautisha wewe na watu wengine. Na kitu kizuri ambacho kitakutofautisha wewe na watu wengine ni kuhakikisha kwamba unafanya kazi muda ule ambapo watu wengine wanaacha. Huu ndio muda mzuri kwako wewe kufanya kazi. huu ndio muda ambao utakutofautisha wewe na watu wengine. Hapa tumeuona na kutoa maana ya muda mzuri wa wewe kufanya kazi, kwa lugha ambayo ni ya kawaida sana, na inaeleweka sana. lakini kikubwa sana ni kwamba tumetumia miwani ya dhahabu kuweza kutoa maana ya muda huu mzuri kwako kufanya kazi.

 

Wanariadha wanalifahamu hili. Huwa wakikimbia na kufikia hatua ya kuchoka hapo ndipo huwa wanaanza kuhesabu kwanza zoezi limeanza. Hali hii huwatofautisha wanariadha waliofanikiwa na wanariadha wengine. Wanariadha ambao wamefanikiwa wanajua haswa kwamba kama na wao wataendekeza kuchoka kama walivyo watu wengine hakutakuwa na tofauti kati ya wanariaddha ambao wamefanikiwa na ambao hawajafanikiwa. Ukwelli kama huu umekuwa unatumiwa na watu mbali mbali kama wanamasumbwi, waogeleaji, wachezaji wa mpira kutaja ila wachache.

 

 

 

 Hivyo ni muhimu sana sana tukaufahamu ukweli huu na kuhakikisha kwamba tunatumia.  Ukwe;I kwamba muda mzuri kwako kufanya kazi ni pale unapokuwa umechoka.

 

 

 

Hatua ya kuchukua siku ya leo. Nenda kafanye kazi kwa bidii. Ikifikia hatua ambapo utakuwa unajihisi kama umechoka na huwezi kuendelea tena, anza kuhesabu moja. Ifanye hiyo hatua kuwa moja. Na uendelee mbele. Nakutakia wakati mwema rafiki na ndugu yangu.

 

Tukutane kileleni.

 
MUHIMU SANA;
Kuna semina ya ambavyo nimeipa kichwa cha TIMIZA MALENGO YA MWAKA MZIMA NDANI YA MIEZI SITA.  Ndio namaanisha miezi sita. Ndani ya semina utapata kujifunza mambo mengi sana yatakayokusaidia sana wewe kutimiza malengo yako mwaka huu. Kikubwa zaidi katika kutekeleza na kutimiza malengo yako nimekuja na mfumo Mpya ambao binafsi nimeutumia ndani ya miezi sita na umenipa matokeo makubwa sana katika kutimiza malengo yangu. Mfumo huu unaitwa MFUMO WA NYUMBA (HUOUSE SYSTEM). Huu ni mfumo Mpya hapa duniani, na binafsi nimeutumia umenipa matokeo makubwa. Naenda kuwa nakudadafulia mfumo huu kwa undani kwenye semina hii ambayo nitaiendesha. Kiufupi kosa mengine mwaka huu ila usikose kujifunza mfumo huu ambao unaitwa MFUMO WA NYUMBA.
 
Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao kupitia katika kundi la waspu la HAZINA.
Hii ni kutokana na hali ya kwamba
 
1. mtu yeyote anaweza kuhudhuria semina hii akiwa hata nyumbani kwake bila kutumia gharama nyingi za usafiri kuja huku nilipo Mimi.
 
2. Lakini pia kutokana na ukweli kwamba mtu yeyote yule ambaye Yupo kwenye kona yoyote ile ya dunia anaweza kuhudhuria semina hii.
 
3. Gharama za uendeshaji wa semina zinapungua hivyo kukuwezesha wewe kuweza kuhudhuria semina bila kikwazo chochote kile.
 
JINSI YA KUJIUNGA NA SEMINA HII.
Gharama ya semina hii ni kiasi kidogo sana cha 20,000/- za kitanzania. Hii ni gharama ndogo sana kulinganisha na kitu kikubwa sana ambacho unaenda kukipata ndani ya semina hii itakayoanza mwezi wa saba tarehe 15 mpaka tarehe 19.
 
Jinsi ya kulipia.
 
Tuma pesa kupitia namba ya voda MPESA 0755848391 yenye jina la GODIUS RWEYONGEZA. baada ya hapo nitumie ujumbe wenye neno HAZINA wasapu namba 0755848391. Ili niweze kukuunganisha kwenye mundi hilo tayari kwa ajili ya semina hii.
 
MANUFAA MENGINE YA KUNDI LA HAZINA.
1. Kwanza kabisa ni muhimu sana kufahamu kwamba kundi la hazina ni  tofauti na makundi mengine ya wasapu ambayo umeyazoea. Kundi hili lina watu makini ambao wapo tayari kuhakikisha kwamba wanatimiza malengo yao. Watu walio katika kundi hili huwa wanalipia elfu ishirini kila baada ya miezi sita kuwa katika kundi hilo.
 
2. Lakini pia kuwa katika kundi hili kutakuleta karibu sana na Mimi ambapo nitakuwa tayari kukusaidia na kuongea na wewe hapo muda wowote ule kuhakikisha kwamba unafikia Kile kilichobora zaidi.
 
3. Lakini pia nitahakikisha kwamba tunafanya kazi bega kwa bega ili kuhakikisha kwamba unatimiza Malengo yako ndani ya miezi sita.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwa sasa siwezi kuwa kwenye kila kundi na kumsaidia kila mtu maana ninazo kazi nyingi sana ambazo zimenibana, hivyo kuwa kwako katika kundi la hazina ni kitu ambacho kitatufanya tuwe karibu sana muda wote.
 
4. Lakini pia utapata nafasi nzuri sana ya kuhudhuria semina ya kufungua mwaka 2018 bure kabisa. Hii ni kutokana na ukweli kwamba bado ada yako ya miezi sita itakuwa bado haijaisha hivyo utazidi kupata kilichobora sana kutoka kwangu.
 
Hivyo hakikisha kwamba haukosi nafasi hii adimu sana kwako kuweza kufanya mambo makubwa sana.
 

 

Hakikisha hauikosi nafasi hii adimu

NI MIMI RAFIKI NA NDUGU YAKO
KOCHA GODIUS RWEYONGEZA
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X