Jambo Ambalo Unapaswa Kuliepuka.


Habari za leo Rafiki na ndugu msomaji wa SONGA MBELE BLOG. imani yangu, jumapili ya leo imekaa vyema sana, na umeshaanza kufanya mambo makubwa sana..
Ndani ya siku hii ya leo, kati ya yale ambayo umepanga kufanya, hakikisha kwamba unayafanya siku ya leo bila kuacha. Ukiacha kufanya utakuwa umehairisha kazi ambayo ni ya muhimu sana. Ukiacha kufanya maana yake utakuwa umehairisha na kuhairisha ni jambo ambalo unapaswa kuliepuka. Na hili ndilo jambo ambalo tunakutaka uliepuke na katika makala ya leo, jambo la kuepuka ni kuhairisha.

“Shughuli inapokuja na kugonga mlangoni mwako, ikaribishe; ukiiambia subiri, itaondoka na kurudi tena mlangoni mwako,  ikiambatana na shughuli nyingine saba.” Hayo ni maneno ya mshairi Edwin Markum. Usihairishe kufanya kitu leo. Kile ambacho unahairisha leo, bila shaka utakihairisha na kesho. Kumbuka kwamba mafanikio yanakuja kwa mwanadamu ambaye anachukua leo, kwa Kile kitu ambacho watu wengine wanasema watafanya kesho.

Hatua ya kufanya siku ya leo. Hakikisha kwamba unafanya kazi zote ambazo umepanga kufanya bila kuhairisha. Kuhairisha ni chanzo cha kukukurudisha nyuma, usikaribishe kuhairisha kwa aina yoyote ile. Inalipa sana kufanya kitu kwa wakati wake.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X