Jambo Moja Ambalo Litakufanya Uzidi Kung’aa


Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa makala za songa mbele. Imani yangu kuwa umeianza siku yako kwa namna ya tofauti kubwa sana. leo hii ikiwa ni siku npya ambayo haijawahi kutokea katika dunia hii ambayo tunaishi.  Leo hii ni siku bora sana ni vizuri sana ukahakikisha kwamba unaitumia vizuri sana siku yako kwa kufanya kitu ambacho ni cha tofauti.

Kuna msemo wa kiingereza unaosema kwamba mambo yanapokuwa magumu ndipo wagumu wanapoendelea na kazi. Huu ni msemo ambao una ukweli mkubwa sana ndani yake. Maana siku zote nyakati ngumu lazima utakutana nazo katika safari yako ya kuhakikisha kwamba unaenda kileleni. Lakini kwa kuwa wewe ni mgumu basi nyakati hizi sio kitu bali ni daraja la kuhakikisha kwamba unaweza kufika unapotaka.

Maisha siku zote ni rahisi sana. illa kikubwa sio kwamba maisha ni rahisi ila ni mtazamo wako juu ya maisha ulivyo. Ukiwa na mtazamo hasi utaona kila kitu ni hasi na ukiwa na mtazamo ambao ni chanya basi kila kitu utakiona katika uchanya wake.

Katika makala ya leo tunaenda kujifunza kitu kimoja cha muhimu sana ambacho kitakufanya uzidi kung’aa katika yale ambayo unayafanya. Kitakufanya ung’ae katika kila sekta ya maisha yako.

Kwanza kabisa ni muhimu sana kufahamu kwamba tuna mahitaji mengi sana ambayo tunayahitaji katika maisha yetu. mahitaji ni vile vitu ambavyo tunataka tupate.  Vitu vyote hivi tunaweza kuvipata tukiwa na kitu kinaitwa MALENGO. Malengo ni kitu ambacho kitakufanya ung’ae kwenye maisha yako. Hiki ndicho kitu kimoja ambacho nilitaka kukwambia katika makala ya leo;Ni vizuri sana kupenda vitu, lakini ni bora sana kuwa na mpango wako maana siku zote watu huwa hawapangi kushindwa bali wanashindwa kupanga kama ambavyo alisema JOHN BECKLEY.  Kumbe wewe kama mwanamafanikio haupaswi kushindwa kupanga maana kwa kushindwa kufanya hivyo utakosa kuja kung’aa. Kupanga ni njia moja wapo ambayo itakulekeza wewe kwenye mafanikio.

Kama unataka kufanikiwa unaaweza usiwe na mpango wala malengo maana hivi vitakuwa sio vitu vya muhimu sana kwako. Lakini kama unahitaji kufanikiwa basi kuwa na malengo na mipango ya kudumu ni muhimu sana. unapokuwa makini na kile ambacho unataka kufanya lazima utaweka mpango wa kujhakikisha kwamba unakifikisha kule ambapo unataka.

Katika kuhakikisaha kwamba unaweza kufanikisha hili na unakuwa na malengo yako pamoja na mpango wako wa kudumu basi nimeamua kukuandalia semina ambayo nitaiendesaha kwa njia y amtandao kupitia wasapu. Semina nitaiendesha kuanzia tarehe 15/7 mwaka huu mpaka tarehe 19/7. Semina hii nimeipa jina la timiza malengo ya mwaka ndani ya miezi sita. BONYEZA HAPA ILIKUHUDHURIA SEMINA HII. Semina hii itakupa vitu ambavy vitakufanya uweze ung’aa na kufnay mambo makubwa sana katika maisha yako ya kila siku hivy semina hiii siyo ya kukosa.

Ni Mimi Rafiki na ndugu yako
Kocha Godius Rweyongeza
0755848391
Asante


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X