Kitu Kimoja Ambacho Unakihitaji Ili Kuweza Kufaulu Katika Kazi Zako


Habari za asubuhi ya leo rafiki yangu na ndungu msomaji wa makala za blogu ya songa mbele. Imani yangu umeianza siku yako vyema sana na unaenda kufanya kitu cha tofauti.

Siku hii ya leo ikiwa ni siku njema sana tunaenda kujifunza kitu kimoja ambacho unakihitaji ili kuweza kufaulu katika kazi zako.

Bila shaka umewahi kusikia habari za lenzi ambayo ikiwekwa kwenye karatasi inaiuunguza kabisa karatasi na kuifanya kuwa majivu. Wengi sana huwa wanajiuliza hiki ni kitu gani. Wapo ambao huwa wanahusisha jaribio hili la kisayansi na uchawi. Lakini ukweli ni kwamba hapa hakuna uchawi wowote bali ni ukweli kwamba lenzi huwa inakusanya nguvu ya jua  sehemu moja na kuiweka pamoja. Kitu hiki hufanya Miali ya jua kuwa na nguvu sana kiasi cha kuweza  kuunguza karatasi.

Kuna msemo unaosema kwamba mtaka yote kwa pupa hukosa yote. Msemo huu huwa unatusisitiza juu ya umuhimu wa kutopenda kufanya kila kitu ambacho kibakuja mbele yako, bali kuchagua baadhi ya vitu ambavyo unaona vibakufaa na kuendana navyo. Numekuja kugundua kwamba katika dunia hii kuna vitu vingi sana vya kufanya, ila uamuzi wa ufanye nini au uache nini uko juu yako. Kitu cha msingi sana ni kuamua kufanya kitu kimoja na kukifanya kwa ubora wa hali ya juu sana.

Mpaka hapo utakuwa umeshaona mwanga wa kile ambacho ninataka kuongelea rafiki yangu katika makala yetu yennye kichwa cha KITU KIMOJA AMBACHO UNAHITAJI ILI KUWEZA KUFAULU KATIKA KAZI YAKO. Ndio kitu kmoja muhimu sana ambacho unakihitaji ili uweze kufaulu katika maisha yako ni kuweka nguvu yako katika jambo moja tu. basi!.

Bila shaka umewahi kusikia watu ambao wanasema kwamba mtaka yote kwa pupa hukosa yote. Hawa watu wahenga walikuwa wakweli kwa kiwango kikubwa sana. Kumbe ni vizuri sana kuamua kuchagua kitu kimoja na kuhakikisha kwamba unakifanya kwa ubora wa halo ya juu sana.

Kuna hadithi ya mbwa wa mwindaji aliyekuwa   msituni akiwinda ndege. Alimfukuza ndege kwa kazi kubwq sana kiasi kwamba alikuwa anakaribia kumkamata. Mara akatokea sungura aliyekurupushwa na mikiki mikiki ya ya mbwa na ndege. Ndipo mbwa alimwacha bdege yule na kuanza kumfukuza sungura. Sungura alikimbia kwa kazi kubwa sana ila na mbwa naye alikuwa kasi, sungura alifika kwenye bwawa la akawa amekwama akihangaika huku na kule kutafuta njia ya kuvuka. Mbwa naye alikuwa nyuma katibu yake. Pale pale alijitokeza digidigi aliyekuwa akifukuzwa na simba. Digi digi alikuwa kasi sana. Mbwa alimsahau su gura na kuanza kumfukuza digidigi. Aligukuza sana mwishowe alichoka lakini hakupata hata mnofu mmoja.   Somo la haduthi hii liko wazi sana.

1. Ni vyema sana kuamua kufanya kitu kimoja kwa wakagi na kuhakikisaha kwamba umekifanya kwa ubora wa hali ya juu sana.

2. Maliza kila kazi ambayo unaanza. Usiguse kazi hii na kuiacha iishie njiani.

3. Sio kwamba kila njia inakufaa. Lakini njia fulani rahisi ambazo utachagua, chache kati ya nyingi ndizo zinakufaa sana.

Kazi ya kufanya leo. Chagua kazi moja ambayo unaenda kufanya leo. Hakikisha kwamba ukianza kufanya kazi hii unaimalizia mpaka mwisho.  Kuna usemi wa wa wahenga ambao unasema kwamba maji ukishayavulia nguo. Sharti uyaoge.

Chagua kitu kimoja ambacho utakivulia nguo na kuhakikisha kwamba maji yake umeyaoga.

Tukutane kileleni.

Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X