Mambo 12 Niliyojifunza Ndani Ya Masaa 12


Habari ya siku ya leo Rafiki na ndugu yangu, imani yangu kwamba leo ni siku njema sana kwako.

Huwa Nina tabia ya kujifunza kila ninapoenda, kila ninPokutana na MTU, niwe nimemzoea au la! Huwa pia napenda kunifunza kwa vitu ninavyokutana navyo, sauti ninazosikia na vitendo ninavyoona. Jana ilikuwa kati ya siku ambazo nimejifunza mambo menfi sana na hivyo nimeona vyema nikushirikishe hayo mambo 12 hapa hili na wewe ujifunzw Kile nilichojifunza.

1. Umoja ni ushindi

2. Kila kitu ni chema
Uchafu ukipangiliwa vizuri unaweza kuwa kivutio Kizuri vha watalii. Hivyo kama kuna kitu jamii Yako inakiona ni kibaya angalia ni kwa jinsi gani utakigeuza kuwa Kizuri, angalia ni kwa jinsi gani utageuza basi kuwa chanya, angalia ni kqa jinsi gami utaifanya limau kuwa juisi.
3. Kazi ni kazi na maneno ni maneno, wala hata havina uhusiano.
Maneno hayawezi kusimama badala ya kazi, na kama maneno yatasimama kwenye kazi basi hapo hakuna kazi. Hakuna mtu anayeweza kufanya vyote viwili kwa wakati mmoja vikafanikiwa kwa asilimia mia moja. Ukiamua kuongea umepoteza kazi, ukiamua kufanya achana na maneno

4. Hakuna kazi rahisi. Usiseme kwamba kazi ya mtu fulani ni rahisi sana kuliko kazi ya MTU mwingine. MTU anayeifanya kazi yake ndiye aayeujua ugumu wake. Unaweza kusema Dj wa mziki anafurahia kupiga na kubonyeza pale anapokuwa kazini lakini yeye anaujua ugumu wake uko wapi?

5. Ugumu wa kazi usikufanye  uache. Kama ambavyo tumeona hakuna kazi rahisi. Kazi yako inapokuwa ngumu, endelea kupiga kazi. Usiache kufanya. ukiacha kufanya, watu wataona urahisi katika kazi hiyo na kuifanya kwa nguvu zao, hatimaye watafanikiwa.

5. Unachokiwaza juu ya mtu, sio anachowaza juu Yako.

6. Usidharau teknolojia
Teknolojia mpya inapokuja ikumbatie na uendane nayo maana ipo siku itakusaidia. Itumie teknolojia Mpya kwa ajili ya manufaa Yako.

7. Usipoteze muda.
Ukimaliza kufanya kitu, achana na nacho, kafanye kingine. Ila hakikisha kwamba umekifanya kwa uhakika asilimia 100.

8. Kama unaweza kufanya kitu kifanye kwa ubora wa hali ya juu sana.

9.  Kama unajua kufanya kitu usipoteze muda mwingi sana kukifanya. Kifanye kwa wakati, ukimaliza, kafanye kitu kingine.

10. Anachokifanya mtu juu yako hakina maana, mpaka pale utakapokuwa umeamua kukipa maana.

11. Usiogope kufanya kitu maana kila mtu yuko anashughulika na kazi zake

12. Kama kuna kazi kubwa ya kufanya, anza kuifanya hiyo. Ifanye kwa uhakika.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X