Mambo Matatu Unayohitaji Ili Kufikia Ushindi


Habari za leo rafiki yangu na ndugu msomaji wa blogu yako pendwa ya songa mbele karibu sana katika makala yetu ya leo ambapo tunaenda kujifunza kitu kipya amabacho kitatufanya kuwa watu wa ushindi na kuweza kufanya kazi zetu kwa ubora zaidi.

Ushindi ni kitu ambacho kila mtu huwa anapenda katika kuhakikisha kwamba anatoka sifuri na kwenda kileleleni ila watu wachache sana huwa wanaweka mkazo, na kuhakikisha kwamba wameweza kufuatilia na kuhakikisha kwamba wameweza kupata ushindi katika kazi zao. Leo hii katika makala yetu ninaenda kukufundisha mambo matatu ambayo ukiyafahamu basi utakuwa unafanya mambo ya kiushindi kila siku. Kumbuka kwamba ushindi ni kitu ambacho unahitaji kukipata kila siku wala sio kitu cha siku moja au wiki moja bali ni kitu ambacho ni endelevu, yaani ushindi wako unapaswa kuwa umegawanyika katika makundi mawili.

Kundi la kwanza la ushindi wako ni ushindi wa wa masaa. Yaani kwa kutambua kwamba siku inayo masaa 24,  hivyo unahakikisaha kwamba umeweza kuutumia muda wako vizuri ndani ya hayo masaa 24. Kila sekunde kwako inakuwa yenye umuhimu mkubwa sana kwako. Haipiti sekunde kwenye siku yako ammbayo inakuwa haijapangiliwa. Kila sekunde, kila dakika na kila siku yako unakuwa umeipangilia. Ushindi wa masaa unaweza kukuzwa kuanzia kwenye sekunde, dakika, siku, wiki, mwezi na mwaka. Hakikisha kwamba umeweza kushinda ndani ya sekunde ya sasa, hakikisha kwamba umeweza kushinda ndani ya siku ya leo.

Aina ya pili ya ushindi ambao mtu anaupata ni ushindi wa nyakati. Yaani wakati wakati uliopita, uliopo na wakati ujao. Mara nyingi ushindi wa wakaati uliopita huwa sio ushindi wa kulalia sana na kuanza kufikiria sana. Wala ushindi wa wakati ujao huwa sio wa kufikiria kwa sana ingawa ni muhimu sama kuangalia mbele na kuona uzuri wake ukoje! Ushindi mzuri ambao mimi   huwa  naupenda sana ni ushindi wa sasa. Ushindi wa wakati uliopo. Ukifanya jambo kwa sasa, hakikisha kwamba umeweza kulifanya kiasi kwamba umeweza kulifanikisha kwa kiwango cha juu sana. Ushindi mkubwa ambao watu huwa wanapata ni kushinda sasa. Shinda sasa na kesho yako itakuwa bora zaidi. Ni muhimu sana kutambua kwamba ushindi wako wa kesho unatengenezwa leo, hivyo hakikisha kwamba umeweza kushinda leo kwa kufanya kitu ambacho ni bora sana.

Sasa ebu tuangalie mambo matatu ambayo yatakufanya uweze kupata ushindi kwa sasa. Kwanza kabisa ni muhimu sana kwako wewe kukumbuka kwamba ushindi mzuri na ambao ni bora sana ni ushindi ambao unapatikana sasa.

        


       USHINDI MZURI NI ULE UNAOPATIKANA ASUBUHI.

Ukiianza siku yako kwa ushindi utaimalliza kwa ushindi mkubwa sana. Kila siku asubuhi mtu unakuwa na nguvu kubwa sana ya akaili na uwezo mkubwa sana wa kufikiri. Uwezo huu unaweza kuutumia kufanya shughuli ambazo zinaonekana kuwa ni ngumu sana kwako kufanyika na hatimaye kuweza kukuinua kukutoa hapo ulipo kwenda sehemu nyingine (yaani kileleni). Kadri muda wako ndani ya siku husika unavyozidi kwenda akili yako inazidi kuchoka na hivyo kujikuta uwezo wako wa akili yako kufanya kazi ukipungua. Hivyo ni muhimu sana ukautumia muda wako wa asubuhi kila siku kuhakikisha kwamba umeweza kufanya shughuli zenye maana kubwa sana kwako. Ushindi mkubwa unapatikana asubuhi.

Hakikisha kwamba unajenga tabia ya kuamuka mapema asubuhi ili uweze kufanya jambo kubwa sana la ushindi. Huitaji kufanya mambo mengi sana ili uonekane mshindi bali unahitaji kufanya jambo moja kwa ubora sana ili uonekane mshindi. Ushindi wako uko mikononi mwako.

MAJI UKISHAYAVULIA NGUO SHARTI UYAOGE.

Kama kuna kitu umeamua kukifanya hakikisha kwamba unakifanya mpaka mwisho bila kuweka kisingizio chochote kile cha kukuzia. Inalipa sana unapofanya kila kitu na kuhakikisaha kwamba umemaliza kila kitu. Kuna umuhimu mkubwa sana wa wewe kuanza jambo ambalo ni jipya, lakini pia kuhakikisha kwamba umeweza kulimaliza. Kama ambavyo wahenga walisema “maji ukishayavulia nguo saharti uyaoge” basi hakikisha kwamba ukishaanza kufanya kazi yoyote ile unaimaliza mpaka mwisho. Hapa huhitaji kujali watu wengine wanasemaje juu ya jambo hilo ambao unafanya. Hata kama watu bilioni kumi watakukataa katika kile ambacho wewe umeamua kufanya. Usikate tamaa, hakikisha kwamba unaendelea na shughuli yako mpaka pale utakapokuwa umeweza kukikamilisha. Inalipa sana kukamilisha kila kitu unachoanza kufanya.

HAKUNA MTU AMBAYE ANAJALI USHINDI WAKO.

Ukishinda ni juu yako lakini pia ukishindwa ni juu yako. Hakuna mtu ambaye anajihusisha moja kwa moja na kazi zako. Hivyo ni muhimu sana kufahamu ni mambo gani ambayo unapaswa kufanya na mambo gani hupaswi kufanya katika kuhakikisha kamba umeweza kufikia hatua kubwa sana ya kimafanikio. Ukiacha kufanya ni juu yako. Hakuna mtu ambaye atakuja na kuanza kukubembeleza au kukuvuta ili uweze kufanya kile ambacho unapaswa kukifanya.

Hayo ndio mambo matatu ambayo unahitaji katika maisha yako kuhakikisha kwamba umeweza kutoka hapo ulipo na kwenda mpaka kwenye ushindi wako mkubwa. Hakikisha leo unakuwa mshindi mkubwa kwa kuanzakufnya kitu kikubwa asubuhi, hakikisaha umemaliza kile ambacho unaanza kufanya siku ya leo, lakini pia tambua kwamba kushinda kwako kuko mikononi mwako.

 Tukutane kileleniMUHIMU SANA;
Kuna semina ya ambavyo nimeipa kichwa cha TIMIZA MALENGO YA MWAKA MZIMA NDANI YA MIEZI SITA.  Ndio namaanisha miezi sita. Ndani ya semina utapata kujifunza mambo mengi sana yatakayokusaidia sana wewe kutimiza malengo yako mwaka huu. Kikubwa zaidi katika kutekeleza na kutimiza malengo yako nimekuja na mfumo Mpya ambao binafsi nimeutumia ndani ya miezi sita na umenipa matokeo makubwa sana katika kutimiza malengo yangu. Mfumo huu unaitwa MFUMO WA NYUMBA (HUOUSE SYSTEM). Huu ni mfumo Mpya hapa duniani, na binafsi nimeutumia umenipa matokeo makubwa. Naenda kuwa nakudadafulia mfumo huu kwa undani kwenye semina hii ambayo nitaiendesha. Kiufupi kosa mengine mwaka huu ila usikose kujifunza mfumo huu ambao unaitwa MFUMO WA NYUMBA.

Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao kupitia katika kundi la waspu la HAZINA.
Hii ni kutokana na hali ya kwamba

1. mtu yeyote anaweza kuhudhuria semina hii akiwa hata nyumbani kwake bila kutumia gharama nyingi za usafiri kuja huku nilipo Mimi.

2. Lakini pia kutokana na ukweli kwamba mtu yeyote yule ambaye Yupo kwenye kona yoyote ile ya dunia anaweza kuhudhuria semina hii.

3. Gharama za uendeshaji wa semina zinapungua hivyo kukuwezesha wewe kuweza kuhudhuria semina bila kikwazo chochote kile.

JINSI YA KUJIUNGA NA SEMINA HII.
Gharama ya semina hii ni kiasi kidogo sana cha 20,000/- za kitanzania. Hii ni gharama ndogo sana kulinganisha na kitu kikubwa sana ambacho unaenda kukipata ndani ya semina hii itakayoanza mwezi wa saba tarehe 15 mpaka tarehe 19.

Jinsi ya kulipia.

Tuma pesa kupitia namba ya voda MPESA 0755848391 yenye jina la GODIUS RWEYONGEZA. baada ya hapo nitumie ujumbe wenye neno HAZINA wasapu namba 0755848391. Ili niweze kukuunganisha kwenye mundi hilo tayari kwa ajili ya semina hii.

MANUFAA MENGINE YA KUNDI LA HAZINA.
1. Kwanza kabisa ni muhimu sana kufahamu kwamba kundi la hazina ni  tofauti na makundi mengine ya wasapu ambayo umeyazoea. Kundi hili lina watu makini ambao wapo tayari kuhakikisha kwamba wanatimiza malengo yao. Watu walio katika kundi hili huwa wanalipia elfu ishirini kila baada ya miezi sita kuwa katika kundi hilo.

2. Lakini pia kuwa katika kundi hili kutakuleta karibu sana na Mimi ambapo nitakuwa tayari kukusaidia na kuongea na wewe hapo muda wowote ule kuhakikisha kwamba unafikia Kile kilichobora zaidi.

3. Lakini pia nitahakikisha kwamba tunafanya kazi bega kwa bega ili kuhakikisha kwamba unatimiza Malengo yako ndani ya miezi sita.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwa sasa siwezi kuwa kwenye kila kundi na kumsaidia kila mtu maana ninazo kazi nyingi sana ambazo zimenibana, hivyo kuwa kwako katika kundi la hazina ni kitu ambacho kitatufanya tuwe karibu sana muda wote.

4. Lakini pia utapata nafasi nzuri sana ya kuhudhuria semina ya kufungua mwaka 2018 bure kabisa. Hii ni kutokana na ukweli kwamba bado ada yako ya miezi sita itakuwa bado haijaisha hivyo utazidi kupata kilichobora sana kutoka kwangu.

Hivyo hakikisha kwamba haukosi nafasi hii adimu sana kwako kuweza kufanya mambo makubwa sana.

Hakikisha hauikosi nafasi hii adimu

Ni Mimi Rafiki na ndugu yako

Kocha Godius Rweyongeza
0755848391
godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X