Habari za siku ya leo rafiki yangu na ndugu msomaji wa blog wa songambele, imani yangu siku ya leo ni siku njema sana. Na umeianza tayari kwa kufanya mambo makubwa sana, ambayo yanakutoa katika sehemu ya chini na kukupeleka kileleni.
Kumbuka kwamba kesho bora inatengenezwa siku ya leo.
Kesho bora haiji mpaka pale utakapokuwa umeitengeneza wewe mwenyewe kwa matendo na kuhakikisha kwamba unatimiza wajibu wako wa kila siku.
Ili uweze kutengeneza kesho bora unapaswa kutimiza wajibu wako, leo hii, bila kuhairisha. Mambo mazuri ya kesho yanatengenezwa leo.
Kuna mtu akiwahi kusema kwamba “kazi ngumu duniani ni kazi ambayo ingepaswa kuwa umefanya jana”. Kazi ya Jana ambayo imehairishwa ni kazi ambayo ni ngumu sana kufanyika. Kazi hii ishapitwa na wakati wake, wa kufanyika. Hivyo ni muhimu sana kutambua kwamba, kazi ya leo haipaswi kuhairishwa hata kidogo.
Nakubaliana na William Hasley alidokeza kwamba “matatizo yote ni rahisi kama hutayawekwa kiporo”. Kwa maoni yangu watu wenye maneno mengi sio watu watendaji bali watu wanaohairisha. Ni muhimu sana kuyafahamu maneno ya Mark Twain anayesema “kelele haizalishi kitu. Kuku akiyetaga yai anatetea kama vile kataga kimondo”.
Acha jambo lakufanyika leo lifanyike leo. Maana kama ambavyo anasema John Mason “kesho ni siku pekee ambayo haimo kwenye siku za wiki”. Siku za wiki ni jumatatu, jumanne, jumatano, alhamisi, ijumaa, jumamosi, na jumapili. Kati ya hizo siku hakuna siku ambayo una jina la kesho. Kama mtu atakwambia tufanye, kesho hakikisha kwamba unamg’ang’ania hili akuambie siku husika. Akwambia kama mtafanya ukiwa ni siku ya jumatatu, jumanne au jumatano. Namalizia kipengele hiki kwa kusisitiza na maneno ya Jimmy Lyons anaposisitiza kwamba “kesho ni siku katika mwaka ambayo kila mzembe anasogeza kazi zake”.
Haya hapa mambo mawili ambayo unapaswa kuyafanya ili kuepuka kuhairisha.
1. Ondoa sababu za kutofanya.
Je, kuna sababu ambazo, inaonekana inakurudiasha nyuma? Achana na hiyo sababu na hakikisha kwamba umeifanya kazi yako?
2. Kamilisha kidogo kidogo.
Hakikisha kwamba unakamilisha kitu kidogo kidogo kwenye ile kazi yako kuu ambayo umepanga kufanya . anza Leo
Tukutane kileleni
MUHIMU SANA;
Kuna semina ya ambavyo nimeipa kichwa cha TIMIZA MALENGO YA MWAKA MZIMA NDANI YA MIEZI SITA. Ndio namaanisha miezi sita. Ndani ya semina utapata kujifunza mambo mengi sana yatakayokusaidia sana wewe kutimiza malengo yako mwaka huu. Kikubwa zaidi katika kutekeleza na kutimiza malengo yako nimekuja na mfumo Mpya ambao binafsi nimeutumia ndani ya miezi sita na umenipa matokeo makubwa sana katika kutimiza malengo yangu. Mfumo huu unaitwa MFUMO WA NYUMBA (HOUSE SYSTEM). Huu ni mfumo Mpya hapa duniani, na binafsi nimeutumia umenipa matokeo makubwa. Naenda kuwa nakudadafulia mfumo huu kwa undani kwenye semina hii ambayo nitaiendesha. Kiufupi kosa mengine mwaka huu ila usikose kujifunza mfumo huu ambao unaitwa MFUMO WA NYUMBA.
Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao kupitia katika kundi la waspu la HAZINA.
Hii ni kutokana na hali ya kwamba
1. mtu yeyote anaweza kuhudhuria semina hii akiwa hata nyumbani kwake bila kutumia gharama nyingi za usafiri kuja huku nilipo Mimi.
2. Lakini pia kutokana na ukweli kwamba mtu yeyote yule ambaye Yupo kwenye kona yoyote ile ya dunia anaweza kuhudhuria semina hii.
3. Gharama za uendeshaji wa semina zinapungua hivyo kukuwezesha wewe kuweza kuhudhuria semina bila kikwazo chochote kile.
JINSI YA KUJIUNGA NA SEMINA HII.
Gharama ya semina hii ni kiasi kidogo sana cha 20,000/- za kitanzania. Hii ni gharama ndogo sana kulinganisha na kitu kikubwa sana ambacho unaenda kukipata ndani ya semina hii itakayoanza mwezi wa saba tarehe 15 mpaka tarehe 19.
Jinsi ya kulipia.
Tuma pesa kupitia namba ya voda MPESA 0755848391 yenye jina la GODIUS RWEYONGEZA. baada ya hapo nitumie ujumbe wenye neno HAZINA wasapu namba 0755848391. Ili niweze kukuunganisha kwenye mundi hilo tayari kwa ajili ya semina hii.
MANUFAA MENGINE YA KUNDI LA HAZINA.
1. Kwanza kabisa ni muhimu sana kufahamu kwamba kundi la hazina ni tofauti na makundi mengine ya wasapu ambayo umeyazoea. Kundi hili lina watu makini ambao wapo tayari kuhakikisha kwamba wanatimiza malengo yao. Watu walio katika kundi hili huwa wanalipia elfu ishirini kila baada ya miezi sita kuwa katika kundi hilo.
2. Lakini pia kuwa katika kundi hili kutakuleta karibu sana na Mimi ambapo nitakuwa tayari kukusaidia na kuongea na wewe hapo muda wowote ule kuhakikisha kwamba unafikia Kile kilichobora zaidi.
3. Lakini pia nitahakikisha kwamba tunafanya kazi bega kwa bega ili kuhakikisha kwamba unatimiza Malengo yako ndani ya miezi sita.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwa sasa siwezi kuwa kwenye kila kundi na kumsaidia kila mtu maana ninazo kazi nyingi sana ambazo zimenibana, hivyo kuwa kwako katika kundi la hazina ni kitu ambacho kitatufanya tuwe karibu sana muda wote.
4. Lakini pia utapata nafasi nzuri sana ya kuhudhuria semina ya kufungua mwaka 2018 bure kabisa. Hii ni kutokana na ukweli kwamba bado ada yako ya miezi sita itakuwa bado haijaisha hivyo utazidi kupata kilichobora sana kutoka kwangu.
Hivyo hakikisha kwamba haukosi nafasi hii adimu sana kwako kuweza kufanya mambo makubwa sana.
Hakikisha hauikosi nafasi hii adimu
Ni Mimi Rafiki na kocha wako
Kocha Godius Rweyongeza
0755848391
godius
Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha kutoka kwenye blogu hii