Mambo Mawili (02) Yatakayokufanya Uiunge na Asilimia Tatu (3) Ya Wanamafanikio



Habari za siku ya leo rafiki yangu na ndugu yangu. Imani yangu siku ya leo ni njema sana. kama mpaka sasa unapumua basi una kila haki ya kuutumia uhai wako ambao unao kwa ajili ya kuhakikisha kwamba unaweza kufanya mambo makubwa sana. katika makala ya leo tunaenda kujifunza mambo mawili yatakayokufanya uweze kujiunga na asilimia tatu ya wanamafanikio wa dunia.
Mwaka 1978 katika chuo kikuu cha HAVARD ulifanyika utatiti kwa wahitimu wa chuo kikuu mwaka huo. Mtafiti alitaka kujua wahitimu wanapomaliza chuo kikuu wana mpango gani? Na ni wanachuo wangapi wana malengo?
Iligundulika kwamba asilimia 13 walikuwa na malengo ila hawakuwa na mpango kazi na hawakuweka wazi ni kwa jinsi gani wangeweza kuyafikia hayo malengo yao. Asilimia 84 hawakuwa na malengo kabisa mbali na kwamba walikuwa na matamanio ya kwamba wanataka gari zuri sana, wanataka kuwa na mke au mme mzuri na anayenijali au kupata kazi.
Kiuhalisia ni kwamba kila mtu anayo matamanio kama hayo ila wangapi wameyaweka na kuyafanya kuwa sehemua ya malengo yao. Na kuhakikisha kwamba wanayafanyia kazi kila siku ili kuweza kuyafikia? Hapo ndipo mtafiti alikuja kugundua asilimia ndogo sana ya watu ambao ni asilimia 3, ambao walikuwa na malengo. Walikuwa wameweka wazi ni kwa jinsi gani wanataka kuyafikia malengo yao, ni hatua gani watapitia ili kuweza kufikia malengo yao. Ni baada ya muda gani wanahitaji kuwa wamefikia malengo yao, na watu gani wanawahitaji ili kuweza kufikia malengo yao.
Utafiti huu ulikuja kurudiwa baada ya miaka kumi na kuwaangalia  wale wahitimu baada ya miaka kuni walikuwa wameweza kufikia hatua gani katika uwanja wa mafaniakio. Ndipo walipogundua kwamba ile asilimia 13 ambayo ilikuwa na malengo ila ilikuwa bado haijaweza kuweka kuweka wazi ni kwa jinsi gani wataweza kuyafikia, ilikuwa na mfanikio mara mbili zaidi ya iile asilimia 84.
Na ile asilimia 3 iliyokuwa imeweka wazi malengo yake na yanaeleweka baada ya miaka kumi iligundulika kwamba ile asilimia ilikuwa na mfanikio mara 10 zaidi ya watu wengine ya asilimia nyingine zote ambazo zimebaki kwa pamoja.
Kumbe kuwa na malengo ni jambo la muhimu sana.
Katika makala hi ya siku hii ya leo naenda kukudadafulia mambo mawili ambayo utayahitaji ili kuweza kufikia hatua kubwa sana katika malengo yako!
Mambo mawili yatakayokufanya uweze kujiunga na ile asillimia 3 ya watu wenye mafanikio makubwa.
Je uko tayari? Kama uko tayari basi ebu tuendelee kusafiri kwa pamoja mpaka pale tutakapokuwa tumefikia mwisho wa makala hii ya siku ya leo.
1.     UAMUZI. Uamuzi ni kitu ambacho kinawashinda watu wengi sana hapa duniani. Watu wengi hawajui wanapaswa kuamua nini juu yao. Juu ya kile ambacho wanawafikiri. Juu ya maisha ambayo wamepanga kuishi.
Cha ajabu zaidi ni kwamba watu wanashindwa kufanya hata maamuzi ya chakula gani wanapaswa kula au kunywa. Imegundulika kwamba watu wengi wanapoulizwa juu ya aina ya kinywaji ambacho wangependa kuletewa hasa pale wanapokuwa ugenini wanasema kwamba nipe chochote.
Hii ni kuonesha ni kwa jinsi gani watu wengi hawana uamuzi na hawajui ni kwa jinsi gani wanapaswa kufanya uamuzi. Kumbe moja ya vitu vya msingi sana ambavyo unavihitaji sana rafiki yangu ni kuwa mtu wa kufanya maamuzi. Anza kuamua juu ya sehemu ambazo unapaswa kwenda kuishi, kutembea, aina kipato unachohitaji kuwa nacho, aina watu wambao unawahitaji katika safari yako ya kuhakikisha kwamba unaweza kutoka hapo ulipo na kwenda hatua ya ziada. Ni muhimu sana kuwa na huu ujuzi.
Lakini pia anza kwa kufanya uamuzi mdogo kwenye maisha yako. Anza kwa kuamua aina ya siku ambayo ungependa kuishi. Ipangilie siku yako kwa kuamua kufanya vitu ambavyo unaona kwamba hivi ndivyo vinavyonielekeza kwenye ndoto yangu. Ukifanya maamuzi mazuri yatakupeleka pazuri. Ukifanya maamuzi mabaya utakuwa na mengi sana ya kujifunza. Na moja ya sifa ya watu wengi ambao wamefikia hatua kubwa sana ni uwezo wa kufanya maamuzi yote mabaya kwa mazuri. Tunajifunza kila siku kutokana na maamuzi tunayoyafanya. Maamuzi ni ujuzi ambao wewe binafsi unauhitaji sana. unauhitaji kama ambavyo unahiitaji oksijeni kwenye maisha yako.
2.      KULIPA GHARAMA. Tunapozungumzia mafaniko, kila mtu anataka kufanikiwa. Lakini siku zote kutaka hakuwezi kukupa kile ambacho unakihtaka. Ili kufikia kile ambacho unakihitaji lazima uwe tayari  kuhakikisha kwamba unalipa gaharama. Hakuna kitu ambacho unaweza kupata bila kulipa gharama. Gharama kubwa sana ambazo utahitaji kuhakikisha kwamba umellipa ni gharama ya muda, nguvu  pamoja na kutumia akili yako. Hizi ni gharama mbili ambazo utapahitaji kuhakikisha kwamba umeweza kuzilipa ili kuweza kufikia hatua kubwa. Gharama ya pesa inaweza kuhitajika katika kufikia lengo lako au inawezekana ishitajike kulingana na aina ya lengo lenyewe. Ila hizo gharama tatu zitahitajika kwa nguvu sana ili malengo yako yaweze kutimizwa. Zinaweza kulipwa zote kwa pamoja au kulipwa kwa wakati tofauti tofauti, ila lazima utazilipa kwenye sehemu ya maisha yako wakati unaelekea malengo yako.
Kubali kulipa gaharama ili uweze kupata kile unachohitaji. EARL NINGHTNGALE anasema kwamba utavuna ulichopanda. Kumbe kama utawekeza vizuri katika kuhakikisha kwamba unaelekea hatua kubwa sana lazima utakuja kupata kile unachohitaji.
Kumbe watu wanapoogopa kuweka malengo yao kwa sababu tu kuogopa jua kwamba ni uoga ambao hauna maana gharama kubwa inayolipwa sio ya pesa tu, bali pesa ni sehemu ndogo unayoiiihitaji ili kuweza kufikia malengo yako.
Ni muhimu sana kujua kwamba ukiyazingatia hayo mambo mawili hapo juu, na ukafanya kazi kwa bidii kuyaelekea malengo yako, malengo yako nayo yatakufuata, basi wewe pamoja na malengo yako mtakutana sehemu fulani.
Kazi ya kufanya leo
Fanya maamuzi juu ya maisha ambayO ungependa kuishi,
Fanya maamuzi juu ya watu ambao ungependa kuwa nao
Fanya maamuzi juu ya aina kipato unachohitaji kuwa nacho
Fanya maamuzi, fanya maamuzi, fanya maamuzi.
Anza kulipa gharama ya kile ambacho unakihitaji’
Lipa gharama kwa kuanza kufanya kidogo
Kumbuka maneno ya wahenga yanayosema kwamba haba na haba hujaza kibaba.
Kwa siku ya leo naomba niishie hapo rafiki yangu. Tukutane kesho katika makala nzuri ya kuelimisha na kuhamasisha kama hii.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X