Miezi Sita Imepita! Umefanya Nini?


Habari za asubuhi Rafiki yangu na ndugu msomaji wa makala za songa mbele. Imani yangu umeianza siku yako vyema sana huku ukiwa unaenda kuweka juhudi Ku wa sana kuhakikisha kwamba kazi yako ambayo umeianza, au au unatarajia kuianza inaendelea vyema na hatimaye unaikamilisha. Hakikisha kwamba kitu chochote Kile ambacho umekianza unakikamilisha, usije ukaishia njiani hata siku moja.

Mwanzoni mwa mwaka huu watu wengi waliuanza kwa mbwembwe nyingi sana. Wengine waliuanza kwa kupiga baruti na kushangilia wakati wengine wengine waliuanza kwa mbwembwe nyingi sana na na mipango kedekede ya kufanya kazi.

 Je ulikuwa  umeazimia kwamba utaanza kufanya kitu fulani mwanzoni mwa mwaka huu? Je, ulikuwa umeweka mpango mkubwa sana mwanzoni mwaka mwaka huu? Bila shaka jibu lako litakuwa ni ndio! Je mpango wako bado unao mpaka sasa hivi? Au ndio tayari umeupoteza! Je daftari ulipokuwa umeandika malengo yako bado lipo? Je, bado una hamasa ile ile uliyokuwa nayo mwanzoni mwa mwaka huu? Basi bila shaka nitakuwa na maswali mengi sana ambavyo naweza kukuuliza juu ya hili suala la mipango na malengo yako, lakini hapa kitu ambacho ninataka kukuonesha ni kwa namna gani mtu anaweza kuuanza mwaka kwa hamasa kubwa sana, lakini baadae akaja kuipoteza hamasa ile ambavyo alianza nayo. Au mwingine anaweza kuuanza mwaka kwa kuandika malengo makubwa sana lakini baadae hata malengo yake, akayapoteza na hatimaye asikumbuke wapi alikuwa ameandika malengo yake mwanzoni mwa mwaka.

Mwanzoni mwa mwaka huu niliandika katika moja ya makala yangu kwamba hakuna kitu ambacho kimebadilika ndani ya mwaka huu wa 2017 isipokuwa tu namba ya mwisho ya mwaka ambavyo ni saba. Hakuna kilichobadilika ndani ya 2017 isipokuwa mtazamo wa mtu wala hakuna kilichobadilika ndani ya 2017 isipokuwa wewe uamue kubadilika.  Kitu kikubwa sana  kinachobadilika ni wewe na ratiba zako na jinsi ambavyo unakuwa unaziweka ratiba zako kuhakikisha kwamba umeweza kufikia malengo makubwa sana. Kinachobadilika sio mwaka anayebadilika ni wewe.

Leo hii ninapoandika makala hii ikiwa ni mwezi wa sita tarehe 01 , imani yangu ni kwamba sasa utakuwa unaendelea vyema kutekeleza majukumu yako.

Kama haukumbuki malengo yako uliyaandika wapi mwanzoni mwa mwaka huu usiogope huu ndio muda wako wa kuandika malengo yako upya. Kama uliweka mpango na ulikuwa hata haujaanza kuutekeleza, sasa huu ndio wakati wako wa kuanza kuutekeleza. Hakuna muda ambao ni safi kama sasa kuhakikisha kwamba mpango wako umeufanyia kazi.

Usikubali hata kidogo  kuyapoteza malengo yako ambayo ulipanga kutekeleza ndani ya mwaka huu.

MUHIMU SANA;
Kuna semina ya ambavyo nimeipa kichwa cha TIMIZA MALENGO YA MWAKA MZIMA NDANI YA MIEZI SITA.  Ndio namaanisha miezi sita. Ndani ya semina utapata kujifunza mambo mengi sana yatakayokusaidia sana wewe kutimiza malengo yako mwaka huu. Kikubwa zaidi katika kutekeleza na kutimiza malengo yako nimekuja na mfumo Mpya ambao binafsi nimeutumia ndani ya miezi sita na umenipa matokeo makubwa sana katika kutimiza malengo yangu. Mfumo huu unaitwa MFUMO WA NYUMBA (HUOUSE SYSTEM). Huu ni mfumo Mpya hapa duniani, na binafsi nimeutumia umenipa matokeo makubwa. Naenda kuwa nakudadafulia mfumo huu kwa undani kwenye semina hii ambayo nitaiendesha. Kiufupi kosa mengine mwaka huu ila usikose kujifunza mfumo huu ambao unaitwa MFUMO WA NYUMBA.

Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao kupitia katika kundi la waspu la HAZINA.
Hii ni kutokana na hali ya kwamba

1. mtu yeyote anaweza kuhudhuria semina hii akiwa hata nyumbani kwake bila kutumia gharama nyingi za usafiri kuja huku nilipo Mimi.

2. Lakini pia kutokana na ukweli kwamba mtu yeyote yule ambaye Yupo kwenye kona yoyote ile ya dunia anaweza kuhudhuria semina hii.

3. Gharama za uendeshaji wa semina zinapungua hivyo kukuwezesha wewe kuweza kuhudhuria semina bila kikwazo chochote kile.

JINSI YA KUJIUNGA NA SEMINA HII.
Gharama ya semina hii ni kiasi kidogo sana cha 20,000/- za kitanzania. Hii ni gharama ndogo sana kulinganisha na kitu kikubwa sana ambacho unaenda kukipata ndani ya semina hii itakayoanza mwezi wa saba tarehe 15 mpaka tarehe 19.

Jinsi ya kulipia.

Tuma pesa kupitia namba ya voda MPESA 0755848391 yenye jina la GODIUS RWEYONGEZA. baada ya hapo nitumie ujumbe wenye neno HAZINA wasapu namba 0755848391. Ili niweze kukuunganisha kwenye mundi hilo tayari kwa ajili ya semina hii.

MANUFAA MENGINE YA KUNDI LA HAZINA.
1. Kwanza kabisa ni muhimu sana kufahamu kwamba kundi la hazina ni  tofauti na makundi mengine ya wasapu ambayo umeyazoea. Kundi hili lina watu makini ambao wapo tayari kuhakikisha kwamba wanatimiza malengo yao. Watu walio katika kundi hili huwa wanalipia elfu ishirini kila baada ya miezi sita kuwa katika kundi hilo.

2. Lakini pia kuwa katika kundi hili kutakuleta karibu sana na Mimi ambapo nitakuwa tayari kukusaidia na kuongea na wewe hapo muda wowote ule kuhakikisha kwamba unafikia Kile kilichobora zaidi.

3. Lakini pia nitahakikisha kwamba tunafanya kazi bega kwa bega ili kuhakikisha kwamba unatimiza Malengo yako ndani ya miezi sita.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwa sasa siwezi kuwa kwenye kila kundi na kumsaidia kila mtu maana ninazo kazi nyingi sana ambazo zimenibana, hivyo kuwa kwako katika kundi la hazina ni kitu ambacho kitatufanya tuwe karibu sana muda wote.

4. Lakini pia utapata nafasi nzuri sana ya kuhudhuria semina ya kufungua mwaka 2018 bure kabisa. Hii ni kutokana na ukweli kwamba bado ada yako ya miezi sita itakuwa bado haijaisha hivyo utazidi kupata kilichobora sana kutoka kwangu.

Hivyo hakikisha kwamba haukosi nafasi hii adimu sana kwako kuweza kufanya mambo makubwa sana.

Hakikisha hauikosi nafasi hii adimu.

Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X