Habari za siku ya leo Rafiki na ndugu msomani wa blogu yako ya songambele. Imani yangu umeianza siku yako kwa namna ya tofauti. Leo ni siku bora sana. Hakikisha kwamba hauipotezi kwa kufanya mabaya, Bali ipangilie vizuri na kuhakikisha kwamba kila dakika umeitumia kwa kufanya mambo ya tofauti sana.
Ni muhimu kufahamu kwamba kila kitu kikubwa huanza katika udogo wake.
Leo hii naanza kwa kutoa mfano wa mwanzi wa kichina. Mwanzi huu unapandwa mbegu yake na kumwagiliwa kwa mwaka mzima bila kuota wala kuonesha dalili ya kuota. Umwagiliaji huo hauishii hapo, bali huendelea kwa mwaka wa pili mzima na bado huwa hakuna dalili za mti huo kuota. Mwaka wa Tatu na nne mambo ni hayo hayo. Ndani ya miaka hii minne huwa umwagiliaji wake unafanyika kila siku bila kukosa.
Kwenye mwaka wa tano mwezi wa kwanza hadi wa nne mti huu huota kwa futi 90. Na baada ya hapo ukuaji huendelea kwa kasi Kubwa sana. Sasa swali Je, ukuaji umetokea ndani ya mwaka wa tano? Au ulianza kabla!
Nahisi mpaka hapo utakuwa umeanza kupata mwanga wa makala hii ambayo unaisoma.
Kila kitu kikubwa huanza kwa udogo wake, hakuna ukubwa ambao unatengenezwa Mara moja. Ukubwa unatengenezwa taratibu. Ushindi siku zote huwa unaanza na udogo. Udogo ukirudiwa Mara kwa Mara utazalisha ukubwa wa hali ya juu sana. Kamwe usije ukaacha kuanza na kidogo kwa kisingizio cha kwamba wewe ni mkubwa sana na huwezi kuanza na kidogo. Kama wewe unafikiri kwa namna hii ni muhimu sana kufahamu kwamba huwezi kupata ushindi bila kuanza na kidogo.
Kwa elimu ya msingi darasa la saba ni darasa la juu sana. Lakini huwezi kufika darasa la saba bila kuanzia awali na darasa la kwanza.
Zichukue fursa ndogo na zifanyie kazi kwa ajili ya manufaa Yako. Vitu huwa haviwezekani kwa sababu havijajaribiwa. Hakikisha unajaribu vitu vipya kwa kufanya kwa namna ya tofauti.
1. USHINDI WA KWELI HUPATIKANA ASUBUHI.
2. USHINDI HUPATIKANA MWANZNI
3. USHUNDI WA KWELI HUOATIKANA UNAPOANZA
USIDANGANYIKE.
Kujifunza peke yake hakuwezi kukufanya mshindi. Ushindi utakuja pale utakapoanza kufanya kitu.
Hatua ya kwanza kuelekea ushindi ni ngumu sana. Hakikisha unaipitia kwa ujasiri wa hali ya juu sana.
Tarehe ya kuanza kuuelekea ushindi ni leo. Kumbuka kwamba watu ni kama miti lazima wakue au wakauke na kuPotea. Chagua kimoja. Kukua au kukauka. ushindi huanza kwa udogo, hata wqhenga walisha sema haba na haba hujaza kibababa.
Tukutane kileleni.