Swali Linatakaloleta Mabadiliko Makubwa Sana Maishani Mwako.


Habari za siku ya leo Rafiki yangu. Imani yangu siku yako ya leo umeishi kwa namna ambayo ni tofauti sana.

Karibu sana katika makala ya leo ili tuweze kujifunza kitu cha tofauti, sana.

Kuna swali moja ambalo Steve Jobs alikuwa anajiuliza kila siku, na katika kila hatua ambayo alikuwa anapiga.

Ni swali hili hili ambalo lilimfanya, yeye akutane na mke wake mzuri na kuishi naye maisha yake yote. Alipoenda chuo kwenye semina alitoa semina. Wakati wa semina alimwona mwanamke mzuri na kuamua kumwomba namba. Akawa anafikiria ni kwa jinsi ambavyo wangekula pamoja chakula cha jioni, lakini  lakini isingewezekana maana siku hiyo jioni alipaswa kwenda kuonana na watu kwenye mkutano wa kibiashara. Akiwa amesimama mbele ya gari lake anataka aondoke ndipo alipojiuliza swali lake la siku zote. “Je, kama leo ungekuwa usiku Wangu wa mwisho ningefanyaje?”

Alipata nguvu Mpya na kurudi ndani,  alimtafuta msichana mzuri ambaye alikuwa ameongea naye. Alimchukua wakaongea na kukaa pamoja kwa wakati huo na maisha yao yote.

Swali hili ni muhimu sana kwako kuwa unajiuliza kila siku. Anza kujiuliza swali hili katika kila hatua ambayo unapiga.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X